Muonekano chicken sandwich baada ya kuikata
Mchanganyiko halisi wa chicken mayonaise ukiwa juu ya jani la salad
unaweza tumia mkate wa aina yeyote ile slice au huu mrefu
Muonekano halisi wa sandwich ya kuku baada ya kukatwa tarayi kwa kula. kama unapenda kula ikiwa ya moto weka katika sandwich toaster funika ipate rangi ya kahawia toa na kula ikiwa ya moto kwa chipi na tomato sauce na salad saafi kabisa.
Mahitaji:
Jinsi ya kupika kuku ya sandwich:
1 kilo ya kifua cha kuku au miguu ya kuku toa ngozi ili kukwepa mafuta.
1 tangawizi kubwa
3 mbegu za pili pili manga
Chumvi kulingana na ladha unayotaka
Chemsha mchangayiko huo wote pamoja na kuku mpaka kuku iive vizuri na iwe laini kabisa kisha toa katika jiko na uache upoe.
Mahitaji kwajili ya sandwich:
1 loaf of wholemeal bread or French wholemeal loaf (sliced)
1 pili pili hoho iliyokatwa saizi ndogo ndogo
1 kitunguu kilichokatwa saizi ndogondogo
3 au 4 mayonaisi kijikokikubwa cha chakula
3 nyanya nyekundu kata mviringo nyembamba (sliced)
1 tango zuri kata mviringo nyembamba (sliced)
1 lettuce salad nzuri ya kijani
Jinsi ya kuandaa:
Chukua kuku aliepoa nyofoa nyofoa nyama ya kuku weka mifupa pembeni kisha weka ile nyama katika bakuli changanya mayonaise, chumvi, kitunguu, pili pli hoho na pili pili manga ya unga changaya vizuri kabisa.
Kama mchanganyiko wako ni mkavu ongeza mayonaise na lemon juice kidogo kuongeza ladha zaidi.
Chukua mchanganyiko wako wa kuku weka juu ya jani la salad panga vizuri usijaze sana ili uweze kufunika na kipande kingine cha mkate kilichobaki kisha weka slice ya tango na ya nyanya juu ya mchanganyiko wako wa kuku na mayonise.
Chukua kipande kingine cha mkate kilichobaki na funika kwa juu unaweza kula tayari au kama unapenda kau kau unaweza weka mkate wako huo kwenye toaster mashine na kuukausha kwa muda mapaka ukapata rangi ya kahawia na kua na ladha tofauti na ukala sandwich ya moto.
hapa umeniokoa, hapo kwenye MAYONNAISE ipi inafaa maana kuna aina tofauti tofauti nyingine chachuu, light
ReplyDeleteRK
Tumia mayonaise yeyote nzito kila nchi wanatumia brand tofauti za mayonaise kwa Tanzania tumieni american gadern mayonaise ni nzito na nzuri sana
ReplyDeleteHata mimi umeniokoa, thanks
ReplyDeleteSasa sisi wa diet tutumie brown bread sawa je mayonise embu nisaidie huwaga nailaga sana pale nanihiyo hii wananimaliziaga hela zangu.
ReplyDeleteSuzie
Si vibaya kutumia mayonaise mbaya ni kutumia nyingi kupiata kiasi enjoy sandwich yako
ReplyDelete