Friday, February 26, 2010

JINSI YAKUTENGENEZA CROISSANT SAAFI







MAHITAJI

240 siagi (Butter au Magarine yeyote kama blue band)

60 gram maziwa ya maji baridi

180 gram sukari

1/2 chumvi kijiko kidogo cha chai
2 mayai mabichi chapa katika bakuli yachanganyike

720 gram unga wa ngano

1.5 amira ya chenga kijiko kidogo cha chai

60gram Maji ya barafu

 
JINSI YA KUTENGENEZA

Chukua maziwa baridi changanya na maji baridi katika bakuli moja lengo la kutumia maji na maziwa baridi yakusaidie wakati unaanda unga wako amira isiumuke kirahisi.

Chukua unga kiasi sio kwenye mahesabu ya huo hapo juu chukua toka nje kabisa ya mahesabu hayo juu kiasi cha gram mia kisha changanya na siagi ya hapo juu kwenye mahitai kiasi cha gram 120 yaani nusu kisha changanya na huo unga hii itakusaidia wakati unasukuma mchanganyiko wako siagi na unga visiachane ili upate urahisi wa kusukuma. ikishachanganyika safi weka katika freezer igande.

Kisha chukua unga, sukari, amira, chumvi na siagi gram 120 kisha changanya kama unamashine kama hauna kanda kwa mkono mpaka upate mchanganyiko safi kabisa na laini.






 
Maji baridi ya barafu

 


Mchanganyiko wa siagi na unga itoe katika freezer tayari kwa kutumia


 

Ipakaze juu ya mchanganyiko wako wa unga baada ya kusukuma na kupata usawa mzuri



Baada ya kusambaza funika upande wa kwanza kama picha inavyoonyesha



Kisha funika upande wa pili kama picha inavyoonyesha



Kisha funika kwa mara ya tatu utapata umbo kama hili


 

Geuza vizuri unga wako ili usukume upate usawa mzuri zaidi


 

Kisha sukuma na upate usawa safi kabisa



Baada ya kusukuma na kupata usawa safi



Kama kawaida funika upande wa kwanza kama inavyoonyesha picha sasa hapa unaanza kuzitafuta kurasa au layers wakati ukakula croissant unaona huwa kama inakurasa  basi hapa ndio unazipanga zipangike



Kisha funika upande wapili kama kawaida



Funika upande wa tatu kisha weka katika freezer kwa muda wa nusu saa toa nje unga wako fanya kama mwanzo sukuma upate usawa na kisha funika unga wako mara 3 na rudisha tena kwenye freezer baada ya hapo rudia tena zoezi hilo kwa mara ya tatu na ya mwisho kisha uache unga wako kwenye freezer kwa masaa 4 siagi ikamate vizuri.




Baada ya masaa hayo kupita toa nje na iache iyeyuke kidogo kisha sukuma kupata usawa na anza kukata katika umbo maalumu la croissant

 

Huo ndio muonekano wa hatua ya kwanza ya mkato wa croissant




Baada ya kukata safi pia hapo kwa nyuma lazima ukate kidogo ili kupata unafuu wa kukunja upate umbo halisi la mkunjo wa croissant.



Jinsi ya kukata kwa nyuma



Shika mwisho hadi mwisho kunja pole pole mpka umalize mzunguko



Hapa ndio mwisho wa mzunguko wa croissant yako




Unaweza kuiacha katika umbo hili pia ni sawa tu na itakua saafi kabisa



Wengi tumezoea umbo hili halisi sasa ipo tayari kwa kuchomwa ipake ute wa yai ulichanganywa na maji kidogo ili kuongezea nakshi na mng'aro baada ya kuiva




Hii ni croissant iliyoiva na haikupakwa mayai kabla ya kuchomwa imepakwa siagi baada ya kuchomwa



Hii ni croissant safi iliyopakwa mayai kabla ya kuchomwa katika oven inang'aa laini na ni kau kau kwa juu'

FURAHIA NA FAMILIA YAKO AU KAMA NI MPISHI HOTELINI TENGENEZA KWA KIWANGO SAFI WATU WAFURAHI.


1 comment:

  1. AAhh hapa chef umenifikisa love this bread nitajaribu tu. One question what oven temperature intatakiwa na kwa muda gani approx??? Asante

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako