Saturday, February 27, 2010

KEKI YA MACHUNGWA NA ZABIBU KAVU

KUNA MPENZI WA MAPISHI AMEULIZA JE UKITUMIA SELF RAISING FLOUR KUNAHAJA YA KUTUMIA BAKING POWDER? UKITUMIA SELF RAISING FLOUR HUNA HAJA YA KUWEKA BAKING POWDER TENA

 
KEKI HII NI TAMU SANA NA UNAWEZA KUIPIKA KATIKA KILA UMBO NA UKAFURAHIA NA FAMILIA AU HOTELINI WATEJA WAKO WAKAFURAHI SANA










MAHITAJI

• 1 kilo ya unga wa ngano

• 2 kijiko kidogo cha chai baking powder

• 2 Kijiko kidogo cha chai mdalasini ya unga (cinamon powder)

• 1 kijiko kidogo cha chai kungu manga ya unga (Nutmeg)

• 240 gram siagi (butter)

• 480 gram sukari

• 2 Mayai

• 300gram korosho iliyokaangwa ukaikata kata vipande (chopped Cashewnuts)

• 480gram zabibu kavu (raisins)

• 200 gram Maji ya machungwa


JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA

Washa oven yako katika moto wa 325 degree F au 165 degree C paka siagi chombo chako unachotumia kuokea keki kisha weka pembeni.

Changanya unga wa ngao, baking powder, unga wa mdalasini, na unga wa kungu manga kisha weka pembeni.

Chukua bakuli nyingine chukua sukari na siagi kisha piga mapaka ilainike na kua safi kabisa kisha chukua ulemchanganyiko wako wa unga na uchanganye katika mchanganyiko huu wa mayai mimina unga wako kidogo kidogo mpaka umalize wote kisha changanya zile korosho na zabibu kavu na maji wa machungwa ndani ya mchanganyiko wa unga. Kama unga utakua mzito ongeza maji ya machungwa mpaka upate mchanganyiko safi.

Kisha mimina mchanganyiko wako kwenye chombo chochote kile ulichoanda kwa kuokea keki yako. choma keki yako katika oven tayari inamoto kwa dakika 40 hadi 45 chukua kijiti cha kutolea nyama katika meno toothpick choma katikati ikitoka kavu basi keki yako imeiva ikitoka na maji maji bado acha kidogo katika moto iive vizuri.

Toa keki yako katika oven iache ipoe tayari kwa kuliwa.

4 comments:

  1. Chef, kama nikitumia self raising flour kuna haja ya kuweka baking powder? thanks.

    ReplyDelete
  2. I'm still waiting jibu langu

    ReplyDelete
  3. Habari Ruky!

    Nimekujibu siku hiyo hiyo hapo juu ya recipe ya keki kwa faida ya wana blog wote na nimeweka kwa maandishi mekundu na nimefafanua vizuri sana. Ukitumia self raising flour huna haja ya kuweka baking powder nashukuru kwa swali zuri nakutakia mapishi mema.

    Chef Issa

    ReplyDelete
  4. thanks Issa mungu akubariki

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako