Mdau mmoja ameomba ushauri kwa mtoto asiependa kula, matatizo ya mtoto kutopenda kula ni mengi yanaweza kusababishwa na tabia binafsi au maradhi. Kama mtoto yuko salama hana maradhiila hapendi tu kula kazi ni ndogo sana kumbadilisha ili apende kula.
Inawezekana unandaa chakula safi sana lakini bado mtoto anasumbua kula ili kumbadilisha tabia apende kula unatakiwa kumtengenezea kwanza hamu ya kula maana bila ya kuwa na hamu ya kula hata chakula kiwe kizuri vipi huwezi kula vizuri.
Hamu ya kula inatakiwa kuanzia asubuhi unapofungua kinywa, tengeneza chai iwe ya rangi au ya maziwa weka tangawizi ya unga kwenye nusu lita ya maji au maziwa weka tangawizi kijiko kidogo cha chai mzoweshe mwanao chai hii kila siku asubuhi tangawizi ni kiungo kizuri kinachosaidia kumengenya chakula tumboni na kusababisha njaa haraka na hamu ya kula.
Hapo utakua umemtengenezea mtoto hamu ya kula mchana, kwa kumuandalia mtoto hamu ya kula chakula cha usiku tengeneza juisi ya Pasheni au Embe au Nanasi au tunda lolote lile kumbuka kuchanganya tena kijiko kidogo cha chai kilicho jaa tangawizi na usage pamoja na mchanyanyiko wako mpe mtoto glasi moja saafi kabla ya kula na mabadiliko utayaona usimpatie baada ya kula maana itamsababishia njaa.
Fata maelekezo vizuri mabadiliko utayaona ndani ya siku moja tu.
Mdau umeuliza swali zuri sana kuhusu mtoto anaweza kutumia juice yenye tangawizi?
kawaida mtoto akiwa ameanza kula chakula tofauti ingawa bado anaendelea kunyonya maziwa ya mama yake.
Katika mchanganyiko wa juice yako weka tangawizi mbichi ni nzuri zaidi weka kidogo sana ambayo haitaweza kumuwasha onja mpaka uone mchanganyiko ni sahihi kisha mpatie itafanya kazi safi sana sio lazima iwashe hata kwa mtu mzima weka kiasi tu iwe na ladha na itafanya kazi safi kabisa dada Shamimu utakua umenielewa vizuri.
I am impressed with your blog – big up brother – you are one of your kind anyway nimesoma hii advise yako nitaijaribu kwa mwanangu – he is an active six years old boy lakini kula ndio shughuli – I promise to come back to you with the outcome.
ReplyDeleteAll the best – stay blessed.
Yaani we kaka Mungu akubariki, hiki ni kilio cha wamama wengi. naona mabadiliko kwa mwanangu
ReplyDeleteinteresting...naomba jua mtoto wa umri gani ndo wampa hii...wangu ana miezi 11 na naona kama tangawizi itamuwasha au?
ReplyDeleteThanks Bro...ntaifanyia kazi hiyo
ReplyDeleteubarikiwe
Asante,wangu pia ana 11months,anaweza kupewa?
ReplyDelete