MAHITAJI
3 Mayai
300 gram cheddah cheese ikwaruze
30 gram unga wa binzari
200gram mafuta ya kupikia
1 kijiko kidogo cha chai chumvi
JINSI YA KUPIKA FATA MAELEZO CHINI KAMA PICHA ZINAVYOELEKEZA
Chukua cheese aina ya chedah ikwaruze vizuri
kata nyama ya kuku toa mifupa na ukate vipande vidogo kama umbo la kidole kwa urefu
Changanya mayai na cheese pamoja na chumvi na nyama ya kuku
Kisha ongezea unga wa binzali changanya vizuri upate rangi safi ya manjano
weka mafuta ya kupikia katika kikaango chako kisha chukua kipande kimoja kimoja weka kwenye kikaango au griller choma mayai ya kauke vizuri
Huu ni muonekano wa nyama ikiwa na mayai kwenye kikaango
Hapa ni muonekano baada ya mayai kukauka vizuri kweney nyama
Toa nyama ya ko na weka katika sinia ili uiweke katika oven ikauke kama huna oven tumia microwave iweke kwa dakika 3 tu itakua tayari kwa kula
Kaka sasa unauwa band!
ReplyDeleteTumbo lishaanza kukoroma hapa.
Kuku? mtu asiyekula kuku kakatazwa na daktari au huyo ni strong veg.
Nitajaribu pishi hili siku mbili hizi Inshallah.
disminder.
hi issa pole sana na kazi za hapa na pale na mm napenda sana mapishi na kila siku lazima nianglie blog yako sasa kaka hapo kwenye rec yako naomba msaada kidogo tu kwenye mahitaji ulisema mafuta ya kukaangia je unayatumia wapi hayo mafuta
ReplyDeletemdau
Kaka issa asante sana kwa kuanzisha blog hii, nina pendekezo moja unaonaje kama ukiweka labels kwenye posts zako (kwa mfano angalia http://changamotoyetu.blogspot.com/
ReplyDeleteau
http://www.mamanamwana.blogspot.com/)
hii itatusaidia sana wadau wako kuweza kupata recipe hizi wakati tunapozihitaji kuliko ilivyo sasa kwani ni lazima ukumbuke pishi unalolitafuta lilipostiwa wakati gani
ni hayo tu asante sana kwa kazi nzuri.
Wewe ni mkali!!!!
ReplyDeleteKwa jinsi nilivyoona hizo kuku, na nipendavyo burger ya kuku, nimejaribu kuweka mayonise, salad na mooooose bado kidogo nijitafune vidole nikidhani ni burger.
ReplyDeleteNi kawaida yangu kutunga tunga mapishi.
welldone.