Friday, March 26, 2010

CRUNCH FISH DIPPER

HAPA MWANAO AU MUMEO LAZIMWA AKUOMBE UIPIKE KILA BAADA YA SIKU MBILI NI NZURI SANA UNAKULA NA BBQ SAUCE NA TARTARE SAUCE PAMOJA NA POTATO BLOCKS HAINA MAFUTA UNAPIKA KATIKA OVEN KILA KITU NI SAFI NA SALAAMA KWA MLAJI MHHHH YAM YAM YAM!!!




Hivi ni vizi vya kawaida kabisa kata mikato mikubwa kupita kidogo said ta kidole iwe katika umboa la pembe nne kama tofali ( Block) kisha vipake mafuta ya kula kidogo na chumvi kisha viweke kwenye oven mafuta yanasaidia viive na rangi nzuri pia visishike kwenye tay uliyobekia.


 Huu ni muonekano wa fillet ya samaki ikate nayo katika muonekano kama kwenye picha umbo la urefu wa kidole na upana pia. Kumbuka kuiwekea viungo samaki yako maji ya limao au vinega pamoja na tangawizi na kitunguu swaumu kilichosagwa na chumvi.



Kisha chovya kwenye unga wa ngano kipande hicho cha samaki kung'uta unga huo kisha chovya kwenye mayai yaliopigwa



ukishatoa katika mayai weka kwenye unga mkavu wa mikate hakikisha samaki wako ameenea unga wa mikate pande zote safi kabisa. ( jinsi ya kuandaa unga wa mikate chukua vipande vya mikate kisha weka kwenye oven mapaka mikate yote iwe ya kahawi isiungue kisha itoe tumia kwaruzo au greater kwaruza na utapata unga huo safi kabisa na utaweza kutumia kupikia vyakula vingi tu)



Huu ni muonekano safi kabisa wa samaki wako baada ya kuwatia unga wa mikate safi kabisa wachukue na kuwaweka katika oven kwa dakika 15 - 20 inategemea na moto wa oven yako



Kisha watoe na chukua brush wapake mafuta ya kula kidogo sana ili kusaida kuleta rangi nzuri na harufu nzuri na kulainisha samaki yenyewe pia. kisha rudisha kweney oven kwa dakika 3 - 5  kisha toa tayari kwa kuliwa.



Huu ni muonekano wa viazi vyako tayari vikiwa vimeisha iva  baada ya kuviweka katika ovena pia kwa dakika 15 - 20 vitoe tayari kwa kuliwa.



Panga katika sahani yako kwa staili hii kama huna kile kibakuli kidogo cha kuongezea utanashati maana kumbuka watoto wanapenda sana kula vitu vilivyonakshiwa huu ni mtego tosha wa kumnasa mwano asie penda kula vyakula vikavu watoto wanapenda sana sana.



Unaweza kula samaki huyu akiwa na BBQ sauce zinauzwa madukani ni nafuu sana, pia na tartare sauce



Furahia chakua hiki na familai yako weekend hii





2 comments:

  1. Hii nitaipika kaka yangu.
    kipindi kirefu niliacha kupita katika chumba hiki nikipendacho lakini sasa nimerudi kwa kasi mpya.
    Siku hizi ni tupe siri ya mapishi yako. Natoa tu blog adrss.
    Wewe ndiye siri ya mapishi kwangu siku hizi.
    Asante sana.


    disminder.

    ReplyDelete
  2. Sikuwahi kuingia blog hii ya mapishi najuta kwa muda nilioukoda! mimi ni mpishi tu yule wa hobby na sio proffesional ila ningetamani kuwa proffesional siku moja. nashukuru sana kwa mazuri unayotuletea katika lugha inayoeleweka

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako