Thursday, March 25, 2010

WASHANGAZE FAMILIA KWA KIPAPATIO CHA KUKU NA NYAMA YA NG'OMBE

CHAKULA HIKINI KIZURI SANA KWANI UNAPATA LADHA YA NYAMA MBILI KWA WAKATI MMOJA NA NIRAHISI SANA KUANDAA.





Kata kipapatio cha kuku kama inavyoonekana kwenye picha



Hiki ndio kipapatio cha kuku




Kikate tena nusu kama kinayooneka katika picha





Kisha kata mwisho kabisa wa ncha ya mfupa ili uweze kuimenya nyama iachane na mfupa



Hiki ni kipapatio kikiwa tayari kwa kuokwa katika oven kipake kitunguu swaumu na tangawizi,chumvi na mafuta ya kupikia kidogo kisha kiweke kwenye oven kiive



Katika sahani weka viazi vya kusagwa ( mush potato) jinsi ya kutengeneza chemsha viazi ulaya katika maji na chumvi mpaka viive kabisa viwe laini kisha viponde kwa mchapo wa chuma weka kungu managa kidogo na maziwa ya maji na siagi kidogo.



Katika picha huo ni muonekano wa sahani tayari ikiwa na viazi vya kusagwa na mboga zilizochomwa na nyama ya ngombe iliyokatwa vipande vidogo ikaangwa mapka ikaiva kisha ikawekewa mchuzi mzito wa nyanya unakaanga tena mpaka ukauke kabisa katika nyama.




Kisha toa vipapatio katika oven na uviweke juu ya nyama iliyokwisha kaangwa



Huu ni muonekano safi wa mchanganyiko wa kipapatio cha kuku na nyama ya ngombe ya kukaanga pamoja na viazi ulaya vya kusaga.



1 comment:

Tunaheshimu sana maoni yako