JINSI YA KUANDAA VEGETABLE RATATOULA
Chukua mchanganyiko wa mboga pili pili hoho, bilinganya, Nyanya, Vitunguu na Nyanya kata mkato wa aina moja
weka mafuta mengi kwanye sufuria ili yasaidiea kukaanga mboga zako kwa muda mfupi, yakishapata moto wa kutosha mpaka yakaanza kutoa moshi weka bilinganya ndani ya sufuria
kisha koroga zisishike chini zikaungua.
Kisha weka vitunguu ndani ya sufuria na endelea kukoroga kumbuka jiko lako liwe na moto mkali ili mboga zipikike kwa muda mrefu bila kurojeka
Kisha weka vitunguu swaumu vilivyosagwa, tangawizi iliyosagwa kidogo, binzali ya unga kiasi, mdalasini ya unga kiasi, kungumanga ya unga kiasi kaanga kwa dakika 3 kisah weka nyanya ya kopo koroga isiungue mpaka nyanya ishikane na mboga kama mafuta yamekauka ongeza kidogo chakula hiki kinapikwa na mafuta mengi kiasi.
Kisha weka pili pili hoho ndani ya sufuri pika kwa dakika 2 huu ni muonekano baada ya kukoroga ikachanganyika vizuri
Baada ya hapo weka nyanya ndani ya sufuria koroga pole pole zasipondeke ila zichanganyike na mboga zingine ili kulinda umbo halisi la nyanya
Huu ndio muonekano halisi baada ya kuchanganya nyanya kisha weka chuvi kulingana na ladha yako binafsi.
JINSI YA KUANDAA NYAMA YA SAMAKI
weka maji katika kikaango au sufuria kisha kata malimao mkato wowote ule, kata kitunguu mkato wowote ule pia kata karoti makato wowoete ule weka ndani ya chombo chako cha kupikia
Kisha weka nyama yako ya samaki ndani ya chombo chako cha kupikia katika maji yaliyochemka vizuri ipike kwa dakika 5 tu kisha itoe itakua imeiva safi kabisa tayari kwa kuliwa
NAMNA YAKUPANGA KATIKA SAHANI IVUTIE MLAJI
Weka vugeteble ratatoula yako mwisho wa sahani kati kati kisha weka viazi vya kuchemsha viwili kama inavyoonekana katika picha
Kisha chukua nyama yako ya samaki weka juu ya mboga mboga zakosaafi kabisa
Mwisho weka kipande cha limao kama pambo pamoja na jani la lettuce maana hii ni nyama nyeuoe lazima ipate limao kiasi kwa kuongeza ladha.
FURAHIA CHAKULA CHAKO NA FAMILIA YAKO
S.a maashallah mwenyewe mjuzi kweli yaani unapangalia vzuri hadi raha shukran kwa kutufunza.tunakutakia afya njema. ybty
ReplyDeleteJani la letus?kiswahil.alafu hayo maji. Uliochemshia samaki yenye carot. ....umetoa samaki ukaja kuipambie jehizo carot ndo basi tena huzitumii
ReplyDeleteNashukuru sana kwa swali zuri hayo maji ya karoti hayatumiki tena nikwajili ya kuchemshia samaki tu.
ReplyDeleteChef Issa