Monday, March 1, 2010

JINSI YAKUTENGENEZA PILI PILI MBUZI

PILI PILI HII NI SAFI SANA NA INAKAA KATIKA FRIJI MWEZI MZIMA BILA KUHARIBIKA


MAHITAJI

1 kilo Pili pili mbuzi au pili pili ndefu mbichi
1 kilo nyanya iliyoiva
1 nyanya ya kopo
50 gram chumvi
1 binzali kijiko kidogo cha chai
400 gram mafuta ya kupikia
100 gram tangawizi iliyosagwa
300 gram maji ya limao au vinega
300 gram kitunguu swaumu kilichosagwa au ya unga


JINSI YAKUTENGENEZA

Chukua sufuria au kikaango weka mafuta katika kikaango na acha yachemke hasa mpaka yanakaribia kutoa moshi kisha weka pili plizako kaanga kwa dakika 2 zitalege na kubadilika rangi kidogo kisha weka kitunguu maji na kitunguu swaumu na tangawizi kaanga mapaka navyo vilegee.

Kisha weka binzali koroga ichanganyike kisha weka nyanya ya kopo koroga pia ichanganyike ishike pili pili yako kisha weka nyanya ya kuiva koroga mpaka upate rojo safi na nyanya yako kuiva mafuta yaonekane kuelea juu kisha weka maji ya limao au vinega na chumvi acha ichemke kwa dakika 5 kisha angalia lazima mafuta yaelee juu.

Kama mafuta hayaelei yote yamemezwa na mchanganyiko wako basi ongeza mafuta mpaka yaweke utando juu mafuta haya yataweka utando juu ya pili pili yako hata baada ya kuitoa katika jiko na kuiacha ipoe ili uweke kwenye friji utando huo unasaidia wadudu wasiingie katika pili pili yako kuiharibu ioze pila ladha ya chachu ya limao hufanya pili pili yako kua na ladha nzuri na kuleta uchangamfu zaidi.

Wakati wa kutumia pili pili yako kumbuka kuchota pili pili tu kisha tenganisha na mafuta ni hatari kwa afya yako na familia yako.



4 comments:

  1. mbona hapa sijakupata sasa wadudu wakiingia katika pilipili itakuwaje si itaoza na kunukuu:utando huo unasaidia wadudu waiingie katika pili pili yako uiharibu ioze pila ladha ya chachu ya limao hufanya pili pili yako kua na ladha nzuri na kuleta uchangamfu zaidi.

    ReplyDelete
  2. Annony hapo ju nafikiri hukusoma vizuri.Hebu rudia tena kusoma huenda ulikuwa na haraka...

    ReplyDelete
  3. Hapa unasema nyanya ya kopo, je unamaanisha tomato paste au tin chopped tomatoes. naomba jibu tafadhali nikamilishe pishi hili.

    ReplyDelete
  4. yambo bwana, the pilipili ya mbuzi for me it's the habanero chili and not the cayenne chili. I am right?
    Marie Claire from SHABA and from http://undemisièclederecettes.blogspot.com
    Akisanti sana

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako