Tuesday, March 23, 2010

FISH FILO PASTRY WRAP

HII NI BITE NZURI SANA NA UNAWEZA KULA KAMA MLO KAMILI PIA NA WALI UGALI AU VIAZI VYA KUKAANGA AU UKALA YENYEWE TU KWA JUISI AU SODA.

MAHITAJI

1 Yai
150 gram Kitunguu
100gram Pili pili hoho
100gram Caroti
5 matone ya Tabasco sauce
1 kilo Fillet ya samaki
1 Limao
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
1 kijiko kidogo cha chai Unga wa binzali
Filo pastry/ manda ( inategemea na wingi wa mchanganyiko wa samaki na ukubwa wa bite yenyewe)
100 gram Unga wa ngano




Kata kata kitunguu, pili pili hoho, caroti kama inavyoonysha katika picha kisha changanya pamoja na chumvi na unga wa binzali hii husaidia kupunguza shombo ya samaki na kuongeza rangi nzuri ya chakula


Kisha chemsha kwa dakika 10 tu fillet ya samaki aina yeyote ile ya samaki uipendayo.


Kisha chukua samaki iliyokwisha chemshwa kwa wastani itakua haijaiva vizuri incharange charange mpaka isagike kabisa kisha iweke ndani ya mchanganyiko wako.



Kisha weka yai moja ndani ya mchanganyiko huo


Kisha weka unga wa ngano ndani ya mchanganyiko huo



 kisha changanya na ule mchanganyiko wa mboga mboga safi kabisa mpaka uchanganyike vizuri na kubadilika rangi kisha kamulia limao ili kuongeza ladha safi 




Kata filo pastry yako kwa umbo lolote lile upendalo



Kisha ongezea matone 5 ya tabasco sauce kuongeza kali ya pili pili hii huchangamsha sana mdomoni kama wanakula watoto jaribu kupunguza.



Kisha tumia kijiko kuchota mchanganyiko wako na kuuweka kati kati ya filo pastry ili uweze kukunja na kuufunika mchanganyiko wa samaki na mboga



Baada ya kuchota mchanganyiko wa samaki huu ndio muonekano



Anza kukunja kama picha inavyooonyesha



Endelea kukunja kama picha inavyoonyesha



Hapa sasa unaelekea kunjo la mwisho kama picha inavyoonyesha ukimaliza geuza chini iwe juu na juu iwe chini ili hii mikunjo yako ikandamizwe kwa chini kitafunwa chako kisije kikafunguka

Kisha chukua mafuta na brusha kipake hicho kitafunwa chako chote ili kulaini na kusaidia iwe laini pindi utakapo pika katika oven isiwe kau kau na iwe na rangi nzuri itakapo iva.

Choma kwenye oven kwa muda wa dakika 30 hadi 40 kulingana na moto wa oven yako.



Ukitaka kujia imeshaiva inakua ngumu na nzito zaidi na rangi ya kahawia, huu ndio muonekano baada ya kuva na unaipanga vizuri tu katika sahani na wali na mcuhi pembeni.



Usisahau ukiipamba vizuri kumbuka kuweka na limao pembeni au juu yake mlaji atakapo itaji kuongeza ladha zaidi katika kitafunwa hiki kizuri cha samaki

UFAFANUZI ZAIDI

Filo pastry inatengeneza kutokana na unga wa ngano na inatengenezwa kiwandani na ni laini kweli kumbuka kutumia leya 4 au nne ili iwe ngumu na nzito wakati wa kukunja ili isi vunjike au kuchanika na ni bei rahisi tu ukienda katika maduka ya chakula utaipata kwa urahisi kabisa

Kama hukubahatika kabisa kuipata madukani bado unananfasi kubwa sana tu ya kufurahia kitafunwa hiki kwa kutumia manda ya kutengenezea sambusa na usione utofauti na ikapendeza kabisa.

WAFURAHISHE WATOTO NYUMBANI KWA KUWAANDALIA SAMAKI HUYU MTAMU KABISA KUMBUKA WATOTO WENGI HUPENDA VYAKULA VIKAVU KULIKO VYA MCHUZI



6 comments:

  1. Kaka Issa mbona hakuna maelezo?

    ReplyDelete
  2. asante sana kaka issa kwanza pole sana na shughuli za hapa na pale jamani hii lazima nikajaribu kupika inaoneka tamu sana

    ReplyDelete
  3. Nahisi hii kitu ndiyo nilikula Menai Beach katika harusi ya mdogo wangu. Maana nilishaulizia walitengeneza vipi na maelezo yanaendana kabisa, lakini wao walikaanga.
    Asante sana.


    disminder.

    ReplyDelete
  4. hiyo filo pastry ni nini

    ReplyDelete
  5. DAH HIKI KIDUDE NAMEZA MATE TU HAPA. ALAFU UKIZINGATIA NI CHA KUOKA SI KUKAANGA YANI MAFUTA MINIMUM KWA MIMI NAETAKA KUPUNGUA

    KEEP IT UP CHEF

    ReplyDelete
  6. naomba unipe somo la kupika chapati za kusukuma,
    nikipika zinakuwa ngumu,zinanyambuka,ukikunja inakatika .pls help

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako