Wednesday, March 24, 2010

WAJUA KUTENGENEZA SUPU YA MAHINDI MABICHI YA NJANO??

MUMEO AU MTOTO ANASUMBUA KULA?? HAHAAAA HAPA NDIO PA KUMKAMATA USIMLAZIMISHE MTOTO UJI MTENGENEZEE SUPU HII OHHHH ATAIPENDA NA ATAKULA SANA SANA.

MUMEO MTENGENEZEE ANYWE KABLA YA CHAKULA OHHH LAZIMA AKUSIFIE SANA NA HATAKUA NA KISINGIZIO TENA KWANINI ASILE NYUMBANI NA ATAWAHI KURUDI NYUMBANI AKIJUA MLO SASA UKO MAHALA PAKE

KWA HOTELINI SUPU HII ITAKUA NI GUMZO KWA WATEJA WAKO NA TEGEMEA MGAHAWA WAKO KUA MAARUFU KWAJILI YA SUPU HII

MAHITAJI

1 kopo mahindi mabichi ya njano
200 gram karoti
100 gram kitunguu
150 gram leeks
1 lita maziwa
150 unga wa ngano
100 gram blueband au butter( siagi)




Hii ndio picha leeks inavyoonekana sokololote lile ukienda mjini utazipata kwa urahisi sana na kwajina hili hili



Mchanganyiko wa mboga zikate katika umbo dogo sana karoti, kitunguu na leeks.


Haya ni maindi mabichi ya njano ndani ya kopo kama umelima mahindi haya sio vibaya ukitumia fresh ila sio makavu.



Maziwa katika bakuli ukiwa umeshaanda na mchapo kwajili ya kukorogea


Weka mafuta na mchanganyiko wako wote wa mboga kweny sufuria



Hapa tayari mboga zimeisha iva na hazijaungua kumbuka wala hazina rangi ya kahawia



kisha weka unga wa ngano ndani ya sufuria yenye mchanganyiko wa mboga





koroga vizuri unga ushikame na mboga zote


kisha mimina maziwa kidogo kidogo kumbuka kukoroga kwa kutumia mchapo koroga kwa kasi bila kuachia ili mchanganyiko wako uwe sawa na usiweke madonge madonge ya unga



Baada ya kukoroga maziwa yote na kupata mchanganyko safi na mzito weka aromati ( inapatikana kwa urahisi sana duka lolote liel la chakula na nirahisi sana) inaladha safi sana na huna haja ya kuweka chumvi ukitumia kiungo hiki mhhhh!!!



Mwisho kabisa mimina mahindi yote na kopo libaki tupu acha ichemke vizuri kwa dakika 5 hadi 7 kisha itakua tayari kwa kunywewa ikiwa yamoto.


Huu ni muonekano wa supu ikiwa imepambwa vizuri katika bakuli na jani la minti na vipande viwilivya nyanya muonekano tu ni kigezo cha kumvutia mnywaji ukiacha ladha safi sana ya supu hii.

Kwa mtu mzima au mtoto aliepoteza uzito atarudisha uzito wake haraka sana, na kwa mtoto ambaye hajaanza kula vyakula vigumu baada ya supu hii kuiva iweke kwenye blenda na msagie mwanoa ohhhhh jamani atakunywa na yeye ndio atakua anakukumbusha mama ile supu tamu bado haijaiva tu ????

FURAHIA NA FAMILIA YAKO PAMOJA NA WATEJA WAKO.



3 comments:

  1. MBONA HAKUNA MAELEZO!

    DA LUCY

    ReplyDelete
  2. asante ila tunaomba utuonyeshe jinsi ya kupika supu/mchemsho wa ng'ombe,wa kuku na wa samaki.Hizi supu tumezizoea sana ukitufundisha tutafaidika sana.

    ReplyDelete
  3. Hi Chef Issa, pole na kazi, Hii leek unapoitumia unatumia ile sehemu nyeupe au kule kwenye majani?

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako