Mahitaji basamic vinagrate
2 sukari ya kahawia kijiko kidogo cha chai
1 kitunguu swaumu cha kusagwa kijiko kidogo cha chai
½ chumvi kijiko kidogo cha chai
½ pili pili manga ya unga kijiko kiodogo cha chai
180 gram olive oil
Jinsi ya kuandaa balsamic ninegrate
Weka katika bakuli balsamic vinegrate, sukari, chumvi, pili pili manga na kitunguu swaumu changanya mpaka sukari iyeyuke.
kisha mimina mafuta ya olive kidogo kidogo huku ukichanganya na mchapo mpaka mafuata yote umimine kisha itakua tayari kwa matumizi ya salad yako.
Inasaidia kuongeza ladha katika mboga zako na
Salad hii ni safi kwa afya ya mlaji, inamchanganyiko wa nyanya, matango, karoti, pili pili hoho na zucchin ya kukwaruzwa ikachanganywa na limao, mafuta ya mahindi na chumvi.
Panga nyanya zako kama inavyoonekana katika picha
Kisha panga matango yaliokatwa kwa mduara
Kisha weka kariti upande wa kulia
Kisha weka pili pili hoho upande wa kushoto
Finyanga kwa mkono ile salad ya zucchini iliyokwaruzwa
Kisha iweke mbele ya sahani kati kati ya nyanya
Kisha chukua balsamic vinagrate mwagia juu ya matango yako pole pole
Huu ndio muonekano wa salad yako yenye mchanganyiko safi wa mboga unaweza kula kabla ya chakula au baada ya chakula safi kabisa ni rahisi kutengeneza na aihitaji muda mwingi wa kuandaa na muonekano na ladha ni safi kabisa.
Si mchezo! nimebaki namshangaa huyo bata kwa dk kadhaa
ReplyDeletembona salad yenyewe kiduuchuuu!!!
ReplyDeleteYaani hata sijui nikushuru vipi Chef kwa mambo yako, yaani mi kila weekend ni kupika misosi toka kwa recipe zako. thank you. Nitakutumia picha za mapishi yangu nami
ReplyDeleteyaani chef unatisha,swali langu balsamic vinega ndio ipi hiyo???
ReplyDelete