KUKU NA NDIZI MSHALE NI SAFI SANA KWA MLO KAMILI USIKU AU MCHANA PIA UNAWEZA WEKA KARANGA AU TUI LA NAZI FATA MAELEKEZO NA PICHA HAPO CHINI
Kwa ndugu zangu mliopo ughaibuni ndizi si nzuri san kama ndizi inayotoka Moshi, Arusha au bukoba kwahiyo njia hii ya upishi itakufanya ufurahie sana na usione tofauti ya ladha na kula ndizi laini na safi kabisa
Menya ndizi zako kisha zipake mafuta ya kupikia na chumvi kisha ziweke kwenye oven kwa dakika 15 hadi 20 zitakua zimeiva na laini za kutosha
Pia kuku ipake kitunguu swaumu, pili pili manga, chumvi kisha iweke kwenye oven bila maji itajipika safi na kutoa mchiz kiasi pia utautumia kwenye pishi lako la ndizi oven inasaidia kupika vizuri bila nyama kurojeka na hupotezi vile viuongo kama huna one basi chemsha katika sufuri kwa moto mdogo bila ya kuweka maji ili maji yatakayojichuja toka kwa kuku yataweza kuivisha nyamachunga yasikauke.
Weka kitunguu maji kwenye sufuria yenye mafuta moto kisha weka binzali koroga kwa dakika moja kisha weka nyanya ya kopo koroga kiasi kisha weka kuku na ule mchuzi wake kwenye sufuria kisha mimina zile ndizi acha ichemke kwa dakika 5 hadi 7 ndizi yako itakua safi na imelainika kabisa utafurahia chakula kitamu na rahisi kupika usisahau kuweka chumvi.
Muonekano wa ndizi na kuku ndani ya sufuri zikichemka
Hiki ndi chakula kimeshaiva unaweza kula na salad mchanganyiko au parachichi ohhhh safi sana siku inapita ukiwa na furaha.
Wow! I will try this pishi tomorrow likitoka vizuri nitakujulisha
ReplyDeleteI hope lazima kiwe chakula kitamu sana
ReplyDelete