Sunday, March 14, 2010

JINSI YA KUPIKA SHREDED BEEF

OOoohh hii nyama ni tamu sana sana tafadhali pika familia yao itakusifu kupita maelezo

MAHITAJI

1/2 kilo ya nyama
1/2 kilo ya pili pili hoho
1/2 kilo ya ya kitunguu maji
80 gram soya sauce
300gram unga wa ngano

JINSI YA KUPIKA FATA MAELEZO NA PICHA HAPO CHINI



Kata fillet ya ngombe kwa mtindo wa slice kisha iwekee chumvi, pili pili manga, kitunguu swaumu na tangawizi ya kusagwa pamoja na soya sauce kidogo iache kwenye friji kwa masaa 3 viungo viingie vizuri kwenye nyama.



Kata mtindo wa urefu mwembamba kitunguu na pili pili hoho ya kutosha maana hii ubeba ladha halisi ya chakula hiki kisha weka pembeni tayari kwa kupika




Baada ya masaa3 chukua nyama kisha andaa unga kwenye sahani au sinia kisha ipakaze unga wa ngano hiyo nyama fanya kipande kimoja kimoja kama picha inavyoonyesha kisha kung'uta ibaki na unga kiasi



Kumbuka kuweka unga pande zote mbili na ushike vizuri



Kisha tumbukiza nyama kwenye mafuta ya moto kwa dakika moja tu isiive tafadhali yaani ni kuweka tu na kutoa hakikisha mafuta yako nyanamoto wa kutosha sana




Kisha weka nyama katika bakuli safi na isiwe na mafuta kabisa. Baada ya hapo chukua kikaango na mafuta kaanga mboga zote kwa pamoja nyama kisha weka soya sauce na maji maana ule unga uliotumia kukaangia nyama utafanya mchuzi uwe mzito pika kwa dakika 3 tu toa nyama yako itakua imeiva na harufu safi kama watoto wanacheza nje basi watakuja mbio kweli ndani kwakua harufu imewaita hahahahahahahaaa!!!






Huu ndio muonekano wa chakula chako baada ya kuiva kinavutia sana na nikitamu kupita melezo unaweza kula na chapati, ugali wali au chips.





4 comments:

  1. Mh udenda unanitoka, nimeshaanza kuhisi njaa sasa.
    Yani nikitoka ofisini naenda kujaribu hili pishi.


    disminder.

    ReplyDelete
  2. duuuh yaani unatisha kaka Issa kwa kweli mambo ya msosi unitoi kwakweli uko juu sanaaaaaaaaaaa kaka hongera.

    ReplyDelete
  3. Wow! Yamm! will try tonight

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako