Thursday, March 11, 2010

JINSI YAKUTENGENEZA RUSSIAN SALAD

MAHITAJI

500 gram viazi ulaya ( Irish potato)
1 chupa ya mayonaise
2 vitunguu vikubwa
250 gram karoti
250 gram njegere za kijani

JINSI YA KUANDAA

Chemsha njegere ziive vizuri zisi pondeke, kisha chemsha viazi viive kiasi visipondeke ukiwa umevikata kwa umbo dogo kama la njegere, kisha chemsha karoti nazo zisiive sana zikapondeaka ziwe katika umbo dogo kama la njegere.

Kisha chukua mboga zako zote changanya na mayonaise kiasi upendacho kisha fata maelekezo hapo chini jinsi ya kupamba sahani yako.




Changanya viazi, njegere, karoti na mayonaise na chumvi kiasi mpaka upate mchanganyiko safi kama kwenye picha inavyoonekana.





Kisha weka vipande vitatu vya nyanya kwenye sahani kama inavyoonekana katika picha kisha tafuta chombo chochote cha duara kilicho wazi kua juu na chini ili kikusaidie kutengeneza umbo zuri la salad yako



Baada ya kutumia kile chombo cha duara kutengenezea umbo safi la salda yako huu ndio utakua muonekano wake safi kabisa



huu ndio muonekano wa salad yako juu yake pamba kipande cha yai la kuchemsha likate vipande 4 kisha tumia kila kipande kimoja weka juu  na slice ya pili pili hoho na slice ya kitunguu.

Kula salad hii kabla ya chakula ndugu zangu wengi huwa mnaila sana kweney maharusi nyumbani Tanzania huu ndio ujanja wake jinsi inavyotengenezwa. 



No comments:

Post a Comment

Tunaheshimu sana maoni yako