Thursday, March 11, 2010

SALAD SAAFI YA WALI NA MBOGA MAJANI

JINSI YAKUTENGENEZA SALAD SAFI YA WALI NA MBOGA MAJANI IKISINDIKIZWA NA KALI MAYONAIZI ( curry mayonnaise dressing)

MAHITAJI

250 gram Pili pili hohoo

100gram kitunguu

150 gram Nyanya mbivu

500 gram wali uliopikwa

Kata kata katika umbo dogo sana mboga zote hizi kisha changanya na wali pamoja na chumvi kidogo kulingana na ladha yako pamoja na mafuta ya mahindi weka kwa dakika 20 katika friji acha ipoe tayari kwa kuliwa.


JINSI YAKUTENGENEZA KALI MAYONAIZI DRESSING

300 gram nanasi lililomenywa likakatwa vipande vidogo

200 gram embe la kuiva menya kata vipande vidogo

1 kijiko kikubwa cha unga wa binzali

2 ndizi mbivu

3 kijiko kikubwa cha mayonaise ( American garden)

2 Maji ya limao kijiko kidogo cha chai

2 kijiko kikubwa mafuta ya mahindi

Chukua mchanganyiko wa matunda yote pamoja na maji ya limao na mafuta ya mahindi saga kwenye blender mpaka upate mchanganyiko mzito.

Kisha toa weka katika bakuli changanya na mayonaise kwa kutumia kijiko mpaka ichanganyike vizuri sana  kama unatumia itakua tayari kukumia kwa wakati huo au unaweza funika vizuri na kutumia siku nyingine inakaa kwa muda mrefu sana.

unaweza kutumia kwenye salad yeyote ila au kwa kulia aina yeyote ile ya kitafunwa au bite.




Muonekano wa salad ya wali ikiwa imeshachanganywa na mchanganyiko wa mboga




Huu ni muonekano wa kali mayonaise dressing ikiwa tayari imekamilika



Kata nyanya kwa mshazari kama ionekanavyo kwenye picha pamoja na slice za matango



Weka vipande viwili vya nyanya kisha slice moja ya tango katika sahani kama muonekano wa picha



Kisha Tumia kijiko kuchota wali na weka katikati ya sahani kama picha inavyoelekeza



kumbuka usifunike nyanya na slice ya tango vinaongeza muonekano mzuri katika sahani



Kisha chukua kijiko chota ile kali mayonaise dressing na weka kati kati ya mboga zako tayari salda yako itakua imekamilka na tayari kwa kuliwa ni safi sana na inaliwa kabla ya chakula kamili. Unaweza kula mchana kwakua kawaida mchana unakula chakula chepesi.

IBADILISHE FAMILIA YAKO KWA WATENGENEZEA CHAKULA SAFI NA SALAMA KWA AFYA YAO KIKIWA KATIKA MUONEKANO SAFI












3 comments:

  1. Asante kaka, sasa kama sisi tunaotaka kuanza kupungua tutumie salad ipi?


    disminder.

    ReplyDelete
  2. Habari dada yangu Disminder! nashukuru kwa swali lako zuri salad zote nazozitoa hapa ni safi kwa afya kula kila siku hazita kuongeza uzito namalizia kuaandaa mafunzo na ratiba ya chakula kupunguza uzito utafurahia soon na itakusaidia sana tu na wadau wote nakutakia siku na kazi njema.

    Chef Issa

    ReplyDelete
  3. Asante sana.


    disminder.

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako