Classic Italian Egg and potato Gnocchi
MAHITAJI
800 gram viazi ulaya
1 yai bichi
200 gram unga wa ngano
Kisha weka mafuta kidogo tu katika kikaango kilicho chemka sana ili uzikaange gnocchi kuongeza ladha ya kau kau pia zitabadilika na kua na rangi ya kahawia nzuri. kaanga kwa dakika 2 tu.
Kisha juu yake weka mboga mboga zenye mchuzi safi kabisa wa nyanya
MAHITAJI
800 gram viazi ulaya
1 yai bichi
200 gram unga wa ngano
Kiazi hiki aina ya desiree ndio bora hasa kwa utengenezaji wa gnocchi il ukikosa unaweza tumia kiazi ulaya chochote ukinunua kiazi kiweke angalau siku 2 ili maji maji yapungue maana kikiwa fresha sana kinakua na maji na yanasababisha gnocchi iwe ngumu na nzito sana pia unaweza ukomba muuzaji sokoni akuuzie viazi ambayo sio fresha san vilivyokaa angalau siku 2 visiwe vya kuoza hahaaahahah!
Chukua viazi vyako vikiwa na maganda vioshe vizuri toa mchanga wote kishs vichemshe katika maji kwa dakika 20 hadi 25 hakikaisha vimeiva kwa kuchoma na uma au toothpick kisha vitoe vimenye maganda vikiwa bado vyamoto kisha viponde ponge viwe tope kabisa.
Kisha weka unga wako na yai changanya vizuri kama unakanda unga wa mkate au maandazi usitumie muda mwingi utaaribu mchanganyiko wako unatakiwa ukande kiasi tukama bado unamaji maji basi ongeza unga kidofo tu ili ubaki laini usiwe mgumu sana mchanganyiko ukizidi una ukawa mkavu sana gnocchi inakua ngumu n nzito pia ukisha changanyika kata maumbo madogo madogo kama picha zinavyoonyesha hapo chini.
Kata umbo dogo la duara kisha kandamiza na uma ya chakula ili upate mistar mistari inayoweka muonekano mzuri
Weka maji katika sufuri chemsha mpaka yachemke kabisha kisha weka gnocchi zako mbichi zikiiva mara moja zitapanda juu ya maji zitoe na ziweke pembeni zipoe
Huu ni muonekano wa gnocchi zikiwa zimeiva na ziko pembeni zipoe
Weka kwenye kikaango chenye mafuta yaliyopata moto kisha kaanga
Huu ni muonekano wa gnocchi zilizokwisha kaangwa na kua na rangi nzuri ya kahawia
Huu ni mchanganyiko wa mboga za karoti, kitunguu na pili pili hoho kwajili ya kulia gnocchi
Weka mboga kwenye kikaangao chenye mafuta kiasi yaliochemka kisha kaanga kiasi tu kisha weka mchuzi wa nyanya safia kaanga kwa dakika 3 kisha itakua tayari kumbuka kuweka chumvi
Pakua zile gnocchi zilizokaangwa weka kwenye sahani
Huu ni muonekano wa gnocchi tayari ikiwa na muonekano safi kabisa wa mchuzi wa nyanya na mboga mboga tayrai kwakuliwa kumbuka kumpa mlaji bado ikiw na moto.
Hii ndio GNOCCHI yenyewe imeshapambwa na nynya ya kuchoma na jani la parsley inapendeza sana machoni na ladha yake ni safi sana.
Chakual hiki kinaweza kuliwa na mtoto na mtu mzima na wote wakafurahia pia ni rahisi sana kutengeneza.
Tunakaanga kuongeza ubora na kubadilisha ladha lakini unaweza zitoa katika maji baada ya kuchemsha na ukaziwekea mchuzi ukala safi kabisa bila kuzikaanga ili kubadilisha ladha.
Unaweza kula na nyama aina yeyote ile na ukafurahia sana sana.
IJALI FAMILIA YAKO KWA CHAKULA BORA NA SALAMA
Sawa kaka tunasubiri maelekezo
ReplyDeletehiyo chakula inaonyesha ni tamu sana!nangoja recipe kwa hamu sana.
ReplyDeleteSawa Chef Issa mi nasubiri kwa hamu hiyo recipe,nilishawahi kula hii gcocchi ila nilinunua supermarket!!sasa hii ya kutengeneza mwenyewe naamini itanoga zaidi!kazi njema.
ReplyDeleteASANTE KWA MAPISHI YA AINA MBALIMBALI..........ME NAOMBA KUWEKEW MAPISHI YA KABABU,KACHORI,KATLESS,EGGCHOP NA SAMBUSA.
ReplyDelete