Tuesday, April 13, 2010

PATA RATIBA SAFI YA CHAKULA CHA WATOTO KWA WIKI NZIMA

BABA NA MWANA WANAKULETEA RATIBA SAFI KABISA YA CHAKULA NA VITAFUNWA KWA WATOTO WENYE UMRI WA MIEZI 9.5 MPAKA MIAKA 6






ANAWASALIMU WATOTO WOTE ANASEMA WAZAZI  JITAIDINI MUWATENGNEZEE WATOTO CHAKULA KIZURI WAWE NA AFYA NA WAFURAHI





Kama umeipenda ratiba hii ya chakula kwajili ya mwanao tuma email kwa issakesu@gmail.com ili nikutumie ratiba maalumu ikiwa kweye ms word uweze kuprint pia nikutumie na maelekezo jinsi ya kuandaa vyakula vyote hivyo kwa urahisi zaidi maelekezo ni mengi hayatatosha hapa katika blog yatachukua ukurasa wote.

Naimani mtaipenda sana na familia zenu watafurahia.



20 comments:

  1. Asante kaka chef kwa shule yako ya mapishi unayotumegea maana si wote wenye moyo huyo !! na pia asante sana kwa ile njia ya kumfanya mtoto ale chakula asante niliweza na kufanikiwa!! nasubiri hiyo ratiba ya chakula kwa watoto ya wiki nzima!!
    be blessed!

    mdau Alice

    ReplyDelete
  2. Aaaaaaa! chef Issa huyo mtoto umemscan au maana si photocopy tena yaani mnafanana haulizi Nawaombea raha na baraka nyumba yakushiba daima. mwaaa! nawapenda

    ReplyDelete
  3. Afadhali, maana nina mtoto wa ndugu yangu ana miaka mitatu lakini hadi leo hajawahi kufika kilo kumi na 4 hata siku moja. Hiyo ratiba nafikiri itamsaidia maana mamie mzembe hadi basi. Your baby is cuute just like daddy.

    ReplyDelete
  4. Mashallah mungu akukuzie. nimekutumia email na mimi naihitaji

    ReplyDelete
  5. asante sana issa,jamani umenigusa,manake kila siku natafuta kwenye net vyakula vya watoto sijafanikiwa kupata ratiba iliyotulia ivo,tuelekeze jinsi ya kuandaa plz.ubarikiwe

    ReplyDelete
  6. Habari Chef Issa,

    Ratiba ni nzuri lakini umeweka vyakula vya kizungu. Mimi ninaomba kama inawezekana utuwekee vyakula vya kiswahili mfano maziwa, uji wa lishe, viazi mviringo, ugali, wali au ndizi. Itanisaidia zaidi.

    EGGY

    ReplyDelete
  7. Asante sana chef kwa kweli nimeifurahia sana ratiba yako kaka, na umependeza sana na mwanao na ana afya nzuri sana hongera sana kwa kazi nzuri sana uifanyayo sasa naisubiria utuandikie vile ya kuvipika hivyo vyakula kwa kweli hiyo ni ideas nzuri sana. Keep it up

    ReplyDelete
  8. Mi naomba nitoke nje kidogo, kaka Issa naomba utuwekee recipe ya vitumbua, na kama kuna jinsi ya kusaga mchele bila kwenda machine, maana niko nje ya Tz. Napenda sana vitumbua

    ReplyDelete
  9. Aisee..huyo mtoto umefanana nae vibaya sana yaani ni photocopy!

    ReplyDelete
  10. Mdau mwenzangu uliye nje. Tafadhali saga mchele wako katika brenda wala haina tatizo.

    Chef Issa asante sana, watoto wetu nao wapate kuongezeka uzito Inshallah

    ReplyDelete
  11. THANKS chef nasisitiza...IWEKE KISWAHILI CHAKE HASWA VITU TUNAVYOWEZA VIPATA HATA MAGENGE YA JIRANI NA NYUMBANI, ILI HATA TUWEZE MBANDIKIA DADA JIKONI.....

    ahsante na ubarikiwe saaana

    zeze

    ReplyDelete
  12. Asante Chef Issa kwa kutupa hiyo ratiba nimekutumia email hope utanijibu,mtoto wako ni mzuri sana hongera na asante kwa kuwapenda watoto wetu.
    Namuunga mkono zeze utuwekee vitu ambavyo vinalingana na maisha ya bongo na ambavyo vyaweza patikana kwa urahisi ktk masoko yetu.

    ubarikiwe sana ili uzidi kuwasaidia watoto wetu wawe na afya bora.

    Joyce.

    ReplyDelete
  13. Mama Iqra hii imemgusa, Chef Issa uko juu, unazidisha raha kati ya wazazi na watoto.

    ReplyDelete
  14. Nashukuru sana kaka. Naungana na Zeze, tunaomba utuwekee kwa kiswahili. UBARIKIWE kaka. Dorothy

    ReplyDelete
  15. Kweli Chef Issa nakazia msisitizo, tuwekee ratiba ya vyakula ambavyo huku nyumbani tunaweza kupata kwa urahisi na hata kumuelekeza dada.

    Ubarikiwe.

    Anja

    ReplyDelete
  16. ubarikiwe na mtoto wako mzuri sana na mwafafana kama mawaridi!!

    hii ratiba nzuri sana na itasaidia watoto wetu,maana kuna watoto kula kama jehanamu adi mama unaishia kulia na kufikilia vibaya labda mtoto kalogwa..kumbe ni mipangilio tu ya chakula tafauti na JINSI ya kuvipika

    ReplyDelete
  17. big up kaka.. i like the way you like what you do.All the best.
    NASISITIZA tu ungetoa version ya diet ya watoto kwa vyakula vinavyo patikana kwa mtanzania wa kawaida.
    shukrani

    ReplyDelete
  18. Kaka Issa natumai mzima.

    Mimi niko hapa marekani na najitahidi kumpikia mtoto wetu wa mwaka 1 badala ya kununua vyakula vya kopo na maboksi ambavyo nafikiri si lishe bora.

    Je waweza kunisaidia mapishi kwa ajili ya watoto? Namaanisha recipes badala ya hii ratiba uliyoweka kwenye blogi yako. Nakumbuka dada zangu wakipika uji wa karanga, samaki n.k. Mimi nimeishia kwenye wali wa maharagwe na mboga-mboga, ambavyo bwana mdogo anafurahia lakini nataka apata aina nyingi zaidi ya vyakula ili tukirudi nyumbani asione tabu! :-)

    Nakutakia kila la heri.

    ReplyDelete
  19. Nimependa sana kuhusu lishe za watoto

    ReplyDelete
  20. Naomba kuuliza kuhusu butternuts kwa kiswahil
    i ni tunda gan hili

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako