ASILI YA CHAKULA HIKI NI UBELGIJI NA HULIWA KWA CHAI ASUBUHI AU KAMA KIKATA HAKU YA KULA MCHANA AU USIKU KWA KUONGEZEWA LADHA NA NAKSHI YA MATUNDA AINA TOFAUTI INAPENDEZA SANA.
MAHITAJI
2 mayai
480 gram unga wa ngano
120 gram mafuta ya mahindi au siagi (butter)
420gram maziwa ya maji
1 sukari kijiko kikubwa cha chakula
1 kijiko kikubwa cha chakula baking powder
1/4 chumvi kijiko kidogo cha chai
JINSI YA KUANDAA
JINSI YA KUANDAA
Washa mashine ya waffle ipate moto
Chukua mayai piga kwa kutumia mchapo mpaka ya lainike na kuweka povu
kisha weka katika mayai mchanganyiko wa vitu vyote vilivyobakia piga kwa mchapo mpka vichanganyike vizuri kabisa kama mchanganyiko wako ni mwepesi sana jitaidi kuonegza unga kidogo ili uwe mzito.

Weka mafuta ya mahindi au siagi iliyoyeyushwa kati kati ya mashine ya waffle wafuta yatasambaa yenyewe kuzunguka mashine yote ope pole.
kisha mimina katika mashine mchanganyiko wa waffle na choma kwa dakika 5 tu itakua imeiva na kuweka rangi nzuri ya kahawia ila mashine nyingi za siku hizi zinapika kwa dakika 3 tu na ukiiwasha ikawana moto safi inawaka taa nyekundu waffle yako ikiiva ile taa inazima ujue tayari na uitoe.
kumbuka mashine hii inafutwa tu na kitambaa haisafishi kwa maji wala stell wire maana utaharibu ule utando mweusi wa mashine unaosaidia isigandie na iive safi kabisa.

Huu ni muonekano wa waffle mashine na mchanganyiko wa waffle pembeni
Mimina mchanganyiko wa waffle katiakti ya mashine kisha utasambaa wenyewe mashine nzima kumbuka usijaze kabisa maana ina baking powder kumbuka itaingezeka wakati wa kuiva. ukimaliza funika mashine acha waffle yako iive pole pole.
Huu ndi muonekano wa waffle ikiwa imeiva na inarangi safi kabisa ya kahawiaWATENGENEZEE FAMILIA YAKO WAFURAHIE KILA SIKU KWA KUBADILISHA LADHA YA KITAFUNWA BADALA YA CHAPATI NA MAANDAZI KILA SIKU AU MKATE MASHINE HII NI NAFUU SANA MADUKA YA VYOMBO INAUZWA SH 15,000/= TU. NA MNAOSHI UGAIBUNI NENDA DUKA LOLOTE LILE LA VYOMBO VYA NYUMBANI UTAZIPATA KWA URAHISI SANA GHARAMA NI ILE ILE DOLA 15- 20 TU.
nimeipenda sana ila waffle machine nitaipata wapi niko uk naomba nijulishe
ReplyDeleteWaffle machine zipo Argos or even comet wewe uliza utapatiwa,ila mbona hizi waffle zako kaka zipo nyeupe sana,tofauti na ninazo zijua au ndio tofauti wa upishi?
ReplyDelete