BBQ PRWANS WITH GREEN CURRY SAUCE
Mahitaji
½ kilo prawns
50 gram kitunguu swaumu
100 gram maji ya limao
15 gram chumvi
50 gram prawns masala
20 gram pili pili manga
Kumbuka kuwamenya pwans na kuwasfisha vizuri
Chukua vitu vyote hivyo kwa pamoja changanya kisha weka katika friji kwa nusu saa ili viungo viingie safi katika prawns wako.
Hawa ndio prawns baada ya kusafishwa na kuwekewa viungo vyote safi kabisa
Hapa prawns wapo katika pan wanachomwa pia unaweza tumia kikaango au ukawaqchemsha kwa dakika 10 wankua wameshaiva
Huu ni muonekano wa green curry
Mahitaji
2 majani ya mchai chai
50 gram kitungu swaumu30 gram binzali ya unga
20 gram mdalasini ya unga
20 gram binzali nyembamba ya unga
100 gram tui zito la nazi
50 gram kitunguu maji
40 gram mafuta ya kupikia
200 gram maji safi ya baridi
weka mafuta katika kikaango kisha weka kitunguu maji na kitunguu swaumu kaanga kiasi kisha weka viungo vyote vilivyobakia kaanga kidogo viive kisha weka majani ya mchai chai na maji acha ichemke kwa dakika 15 hadi 20 kisha weka tui la nazi na kama maji yamepungua basi ongezea kiasi acha ichemke tena kiasi kisha
Huundio muonekano wa prawns baada ya kuiva unaweza kuwachoma katika kkaango au ukawachemsha katika maji lakini kumbuka katika maji weka limao na chumvi ili kulinda ladha. Unaweza kula kwa viazi vya kuponda, wali au ugali
Mwisho kabisa kumbuka kumpatia mlaji na kipande cha limao kama urembo juu ya chakula pia inasaidia kuongezaz ladha kwa chakula chochote cha samaki
Nimefurahi sana leo umegusia mapishi ya prawns manake nilikuwa nikitamani sana kujua jinsi ya kuwapika.
ReplyDeleteJayjo
mmmh kaka hapa utafunga ukurusa, tupe hizo hints. Prawns jamani hatari tupu
ReplyDeletetupe kaka, mume wangu atafurahi sana, anavyopenda prawsn! uuuh
ReplyDeletemy precious delicious food prawns
ReplyDeletekitu kizuri sana hiki,me uwa nawanunua na kuwapika mwenyewe siku zote.wanapatikana kwa uzuri pale soko la samaki kigamboni.ata nikiwa mkoani lazima niwaagizie
lol
my chef issa
ReplyDeleteukisema gram wengine wala hatuelewi pliz labda waweza wekea kwa njia ya kijiko ivi vingapi
maana gram si mpaka ninunue vile vikombe vya kupimia?
tuwekee pia kwa njia ya kupimia kwa kijiko ni rahisi
PIA TUNGA KIJITABU/VIJARIDA VYENYE MAPISHI YAKO YOTE TUWEZE NUNUA,serious naitaji sana