Friday, April 30, 2010

JINSI YA KUANDAA CHAKULA CHA MTOTO SIKU YA ALHAMISI KUTOKA KATIKA RATIBA

CHAKULA CHA ASUBUHI

CHAPATI MAJI YA MDALASINI NA VIPANDE VYA APPLE,

250 gram Unga wa ngano
1 yai
50 gram vipange vya apple chemsha viive
5 gram mdalasini
100 gram maziwa ya maji
20 gram mafuta ya mahindi
10 gram baking powder

Jinsi ya kuandaa chapati maji changanya vitu vyote katika bakulikisha piga na mchapo mpaka upate mchanganyiko safi na laini kabisa kama mchanganyiko bado mzito ongeza maji kiasi.

JUISI YA KAROTI NA EMBE

Jinsi ya kuandaa juisi ya Karoti na embe. Menya embe na caroti safi kabisa kisha kata vipande vidogo vidogo iwe rahisi kusagika katika mashine tumia chombo maalumu cha kusagia juice saga embe pamoja na karoti mpaka upate rojo safi kumbuka kuongeza maji kidogo iwapo mchanganyiko wako bado ni mzito kisha hifadhi katika friji bila kuweka sukari ili ikae kwa muda isiharibike kumbuka kuweka sukari wakati wa kunywa.
CHAKULA CHA MCHANA

BATA MZINGA PARACHICHI NA BACON,

Chukua nyama ya bata mzinga au nyama ya kuku au nyama ya bata kisha ipake chumvi kiasi na limao kwa ladha kisha izungushie Bacon mbichi ya ng’ombe kaanga kiasi kisha weka katika oven iweze kukauka tayari kwa kuliwa. Kata vipande vya nyanya na matango pamoja na parachichi ulilomenya safi kabisa kisha kata vipande vidogo vidogo mpatie mtoto ale pia unaweza mpatia mayonaisi tomato sauce ili kulainisha chakula hiki.

GLASI YA MAZIWA

Mpatie mtoto 200 gram glasi ya maziwa.

Kwa mtoto mdogo asieweza kutafuna vizuri pika nyama ya bata pamoja na bacon kisha saga katika mashine weka maziwa na parachichi uwe uji mzito kisha mpatie mtoto itakua chakula safi kabisa.

KITAFUNWA CHA JIONI

POP CORN ZA ASALI NA MCHANGANYIKO WA MATUNDA

Chukua popcon kisha zichanganye na asali na matunda mchanganyiko uliyokata vipande vidogo vidogo iwe rahisi kwa mtoto kula chagua kati ya matunda haya itataegemea na mwanao anapenda matunda yapi Embe, Ndizi, Chungwa, Apple, Papai, Nanasi, Tikiti maji, na mengine mengi. Kisha mpatie mtoto ale atafurahia sana mseto huu.
CHAKULA CHA USIKU

(COTTAGE PIE) NYAMA YA KUSAGA NA VIAZI VYA KUPONDA NA MAZIWA

MAHITAJI

Mchuzi mzito wa nyama ya kusaga ( Bolognese)
200 gram nyama ya kusaga
50 gram kitunguu chopchop
50 gram caroti
150 gram nyanya ya kopo
50 gram pili pili hoho chop chop
50 gram mafuta ya kupikia
5 gram pili pili manga ya unga

Jinsi ya kuandaa
Weka mafuta katika kikaango kisha weka nyama ya kusaga kaanga mpaka iive kabisa kisha weka kitunguu maji, karoti na pili pili hoho kaanga kwa dakika 3 tu kisha weka nyanya ya kopo koroga vizuri kwa dakika 3 zingine weka na chumvi na pili pili manga kwa mbali mchuzi wako utakua umeshaiva.
KISHA ANDAA VIAZI VYA KUSAGA
MAHITAJI

300 gram viazi ulaya
100 gram maziwa ya maji
10 gram chumvi
Chemsha viazi katika maji mpaka viive kabisa kisha vitoe na uviponde ponde kama picha inavyoonyesha hapo chiki kisha weka chumvi na maziwa koroga mpaka upate mchanganyiko laini kabisa.
KIsha chukua bakuli yako safi inayoweza kutumika kupikia kwenye oven weka mchuzi wa nyama ya kusaga nusu ya bakuli kisha weka juu yake hivyo viazi vyakusaga unaweza weka kawaida au ukatumia mfukowa kurembea ( Piping bag) ukapa mapambo mazuri kwa juu kama picha hapo chini kwenye mafunzo jinsi ya kutengeneza cotage pie inavyooonekana viazi vina mvuto. Ukimaliza weka chedah cheese kiasi kwa juu.


2 comments:

  1. Chef Issa, kuna ratiba ya mlo wa watoto umeandika hivi:
    """Chukua nyama ya bata mzinga au nyama ya kuku au nyama ya bata kisha ipake chumvi kiasi na limao kwa ladha kisha izungushie Bacon mbichi ya ng’ombe"""

    nijuavyo mimi bacon ni nyama ya nguruwe, wewe umeandika bacon ya ng'ombe, hakuna kitu hicho. bacon ni nguruwe!

    ReplyDelete
  2. Thanks Issa kwa mafunzo ya Jinsi ya Kuandaa vyakula vya watoto kutoka katika ratiba. Je kuna ratiba planned ambayo imeaonyesha hivi vyakula kwa kila siku sasa ndio unatoa maandalizi ya kila siku au we have to make a schedule from hayo maelezo. Am just curious to know and of course it would be glad to have that ratiba if its there.

    Thanks again and Goodluck.

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako