CHAKULA CHA ASUBUHI ( KIFUNGUA KINYWA)
SANDWICH YA MAYAI
Mahitaji
1 Yai la kuchemsha
2 vipande vya mkate
50 gram mayonnaise (American gaden)
5 gram chumvi
Chukua yai la kuchemsha kisha katakata vipande vidogo kisha chukua nyanya na kitunguu pia kata vipande vidogo (Chop chop) kisha changanya na mayonnaise na chumvi kiasi. Kisha weka juu ya kipande cha mkate kisha funika na kipande kingine cha mkate tayari kwa mtoto kula.
UJI WA MAHINDI NA MAZIWA
Mahitaji
100 gam unga wa mahindi
100gram maji
100 gram maziwa ya maji
Sukari kulingana na ladha
Chukua maji changanya na unga wa mahindi kisha chemsha mapak uchemke ukisha chemka kabisa ongeza maziwa ya maji acha ichemke mpaka uwe mzito kisha onja kama hakuna ladha ya nafaka mbichi.
NAMATUNDA MCHANGANYIKO
Chukua matunda mchanganyiko uliyokata vipande vidogo vidogo iwe rahisi kwa mtoto kula chagua kati ya matunda haya itataegemea na mwanao anapenda matunda yapi Embe, Ndizi, Chungwa, Apple, Papai, Nanasi, Tikiti maji, kiwi, zabibu na mengine mengi angalau upate mchanganyiko wa aina nne.
CHAKULA CHA MCHANA
CHEMSHA FILLET YA SAMAKI, MAHINDI NJANO MACHANGA, NA MAHARAGE
Mahitaji
200 gram Fillet ya samaki
100 gram Mahindi machanga ya njano
60 gram maharage ya kuchemsha
30 gram slice za nyanya fresh ya kuiva
30 gram za slice ya tango
10 gram juisi ya limao
5 gram chumvi
5 gram chumvi
Chukua samaki muweke katika chombo chenye maji moto katia limao moja kamua juisi kisha kata 1 karoti na kitu 1 kitunguu pamoja na 1 pili pili hoho chemsha samaki huyo kwa dakika kumi kisha mtoe weka katika sahani.
Pembeni yake weka mahindi machanga ya njano yanapatikana kwenye makopo kumbuka kulifunga vizuri baada ya matumizi. PIa chukua maharage ya moto yaliochemshwa kwa maji na chumvi tu pia weka pembeni ya sahani kisha weka slice za tango na nyanya mpatie mtoto ale chakula hiki safi sana.
Kama mtoto ni mdogo sana basi ponda mchanganyiko huu wa chakula chote hiki kwa kutumia mashine ya kusagia nyama utapata chakula laini chenye ladha safi sana na mtoto atafurahia sana.
CHAKULA CHA JIONI
MKATE WA PITA, NJUGU MAWE NAUFUTA WAKUSAGA GLASS YA MAZIWA
Mkate wa pita unauzwa madukani ni bei nafuu sana posheni moja ni sh 300 na inamtosha mtoto kwa mlo mmoja.
Chemsha njugu mawe zikisha iva chukua ufuta saga pamoja katika blenda ongezea juisi ya limao, mafuta ya mahindi,kitunguu swaumu na chumvi kisha mpatie mtoto ale mkate huo pamoja na mchanganyiko huu pia na glasi ya maziwa yamoto.
CHAKULA CHA USIKU
MBOGA MAJANI ZA KUOKA NA SAMAKI AU NYAMA YA NG’OMBE AU MAINI AU KUKU PAMOJA NA NDIZI.
200 gram aina yeyote ile ya nyama chagua hapo juu
100 gram nyanya fresh
20 gram nyanya ya kopo
5 grama chumvi
5 gram kitunguu swaumu
20 gram mafuta ya kupikia
20 gram kitunguu
20 gram kitunguu
Kata kata vitu vyote hapo juu kisha changanya vizuri na weka katika oven oka kwenye oven kwa dakika 20 – 30 kisha toa itakua imeiva
Pika ndizi zako kiasi cha gram 250 kwa mtindo wa kuchemsha tu na nyanya na kitunguu pamoja na maji na chumvi kiasi zikiiva pakua zisiwe na maji maji au mchuzi kumbuka watoto wanapenda sana kula vitu vikavu weka katika sahani na kisha pakua nyama ya kuoka weka pembeni ya sahani hiyo hiyo mpatie mtoto ale.
Kama huna oven basi unaweza kaanga nyama hiyo katika kikaango kwa moto mdogo mpaka zikaiva safi kabisa na mchuzi wote kukauka na kisha mtoto akafurahia chakula.
Pia kwa mtoto asieweza kutafuna chukua mashine ya kusagia nyama saga mchanganyiko wako utakua safi kabisa na mzito kwajili aya mtoto kufurahisa chakula hicho ukitumia blender mchanganyiko utakua rojo sana au majimaji kisha utamsumbua mtoto maana chakula hakitakua kizito kitakua chepesi sana atasikia njaa muda mfupi sana.
NA STRAWBERRY SMOOTHIE
Mahitaji
1 ndizi mbivu
30 gram stawberry syrup
100 gram mtindi halisi usio na ladha
50 gram asali fresh ya nyuki
50 gram asali fresh ya nyuki
Chukua strawberry syrup, Asali, mtindi na ndizi mbivu weka katika blender saga mpaka upate mchanganyiko mzito kisha mpatie mtoto smoothie yenye ladha ya matunda mawili pia unaweza ukachanganya na ladha ya vanilla kidogo ili kuongeza harufu nzuri imvutie zaidi mtoto. Kama hauna blender basi tumia mchapo.
Hii ndio mida halisi ya chakula kwa mtoto
CHAI YA ASUBUHI SAA 12:00 MPAKA SAA 2:00 inategemea anakwenda shule saa ngapi jitaidi sana mtoto ale asubuhiasiende shule na njaa ikibidi mfungie abebe.
CHAKULA CHA MCHANA SAA 5:30 MPAKA SAA 7:00 MCHANA
CHAKULA CHA JIONI SAA 10:00
CHAKULA CHA USIKU SAA 1:00 USIKU
Yaani kakaangu hichi unachokifanya hapa ni Kikubwa hata zaidi ya unavyofikiria, HATUNA CHA KUKULIPA ILA KWA HILI MUNGU NDO ATAKULIPA INSHALLAH....
ReplyDeleteAsante sana chef kwa hili darasa. mungu aibariki kazi ya mikono yako.
ReplyDeletetunashukuru sana!Mungu akubaliki sana na kuzidi kuongeza maarifa zaidi juu yako,azidi kukutofautisha kati ya watu uwe wa pekee.
ReplyDeletetunashukuru sana Mungu akubariki sana na kuachilia maarifa ya kutosha juu yako,akazidi kukutofautisha kati ya watu nawe ukawe wa pekee sana.Amen
ReplyDelete