Monday, May 10, 2010

SAMAKI MCHEMSHO NA VIAZI VYA KUPONDA

SAMAKI HUYU SAFI SANA KWA AFYA YA MTOTO NA MTU MZIMA HAPIKWI KWA MAFUTA

Huu ni mchanganyiko wa mboga mboga karoti, zucchini, pilipili hoho, kitunguu, kabechi kata kaa inavyoonekaa katika picha

Chemsha viazi viive sana kisha viponde changanya vipande vya mboga zilizochemshwa kidogo weka kiasi kama inavyoonekana katika picha



Kisha chukua fillet ya samaki iweke katika maji uliyochanganya na zile mboga ulizokata mwanzo pia weka limao au vinega na chumvi ili samamki wako awe na ladha safi. chemsha wa dakika 10 - 15 atakua ameiva safi



Huu ndio muonekano safi wa samaki wako aliesisha iva weka viazi vya kuponda ponda vilivyo na mchanganyiko wa mboga kisha pembeni weka samaki wako safi juu yake unaweza weka chuzi wa ladha yoyote ile uipenday wewe iwe mchuzi wa nyanya kawaida au mchuzi wa nazi au mchuzi wa binzali itapendeza sana na kufurahia na familia yako.


4 comments:

  1. Asante sana Shef Issa na mama . Kwa kweli mnatufurahisha na kutusaidia sana sisi kina mama ambao hatujui kupangilia vyakula kwa familia zetu.

    Pia mnatusaidia tujue kuwa chakula kizuri sio gharama. Ila ni kupangilia tuu vyakula ulivyo navyo.. Mungu awabariki sana kwa upendo wenu kwa sisi Watanzania wenzenu... Mimi nimefaidika sana kwenye hii Blog na kila siku najifunza kitu kipya...

    Tena picha za vyyakula mnazoweka zinasaidia kweli tuweze kuelewa.

    Nawatakia kazi njema.
    Ni mimi mama Jeremiah

    ReplyDelete
  2. Chief habari yako, hongera tele kwa kutufunza mapishi haya, ila mie nina haya ya kusema. Je wewe unatoa mafunzo haya sehemu yoyote kuacha ktk blogu yako? unaoneje ukifungua chuo chako cha mapishi na watu tukaja kujifunza wajua mapishi yanataka practice na baadhi ya spice unazoweka hapa wengine hatuzijui na wala hatujui zapatikana wapi, tatu jaribu tafuta ktk TV za hapa bongo upate rusha hewani haya mambo kwani sio wote wana access na internet naamini wapo ambao hawajui haya mambo kabisa, mie nimevutiwa sana tu na ningependa kusikia mkakati wako juu ya hili. samahani mie nimeona matangazo yako shamimu ana kwa michuzi ila kama upo sehemu nyingine sijui kwahiyo ni wazo binafsi na naamini hutochikizwa na maoni yako, mbali na hivyo basi utaniwia radhi. kazi njemaaa


    By Ashura

    ReplyDelete
  3. Mungu wangu mbona icho chakula ni kitaamu sana hadi kwenye picha ,,asante sana kwa kutuwekea ilo pishi lazima nilifanyie kazi thnx

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako