UNAWEZA TUMIA TUNDA LOLOTE KATI YA HAYA MAWILI JINA NI MOJA LAKINI YANATOFAUTINA LADHA MOJA NI TAMU NA MOJA NI CHAHU PIA UNAWEZA CHANGANYA YOTE MAWILI NA UKAPATALADHA SAFI SANA YA JUISI YAKO
Huu ndio muonekano wa passion tunda ya ganda la zambarau ambayo huwa ni tamu sana
Na hii ndio picha ya passion tunda ya ganda la njano ambalo huwa ni chachu kiasi
MAHITAJI
4 sukari vijiko vikubwa vya chakula
4 sukari vijiko vikubwa vya chakula
3 passion tunda makubwa
1 lita ya maji baridi
1 juisi ya limao
JINSI YA KUANDAA
Kwanza kata tunda lako la passion nusu kisha toa juisi na mbegu zake zote zilizopo ndani wka katika bakuli.
Kisha chukua sukarina maji pamoja na mbegu na juisi weka katika blenda saga kwa muda wa dakika 1.5 mpaka 2 zima blenda ili mbegu zisi pondeke na kuaribu sura ya juisi yako.
kisha toa tumia chujio chuja juisi yako na weka katika bakuli au chombo chochote safi onja sukari kama inatoshakisha ongezea juisi ya limao na weka katika friji ipoe tayari kwa kunywewa.
unaweza ongeza vipande vya barafu (ice cubes) kwajua la miezi hii wakati wa mchana utafurahia kinywaji chako baridi na safi
baada ya chakula familia itafurahia kwa kuburudika na kinywaji hiki safi na baridi kwa afya
Hi Chef. Asante kwa kujibu swali langu.
ReplyDeletehe bora umerudi nilikumiss
ReplyDeletebora umeanza na juice...mie napenda saana passion iyo ya juu huwa ni tamu na ina harufu nzuri...naweza inywa hata yenyewe bila kumix
tatizo hii ya pili nikiinywa kata kama ikiwa imemixiwa na embe au na chochote naskia kiungulia saaana.
JE KUNA KITU NAWEZA MIX ILI NISIHISI KIUNGULIA
Mama Iqra
Zeze changanya na papai kwani papai huwa linasaidia kumaliza kiungulia. Hata kama umekula maharage kitaisha. @ Nagira
ReplyDeletezeze u may changanya na parachichi na chungwa walau moja inakata kiungulia kabisa
ReplyDeletepam
NAKUSHUKURU SANA ISSA, MUNGU AKUBARIKI SANA KWA ELIMU HII, NILIKUWA SIJUI MAPISHI MENGI NIMEANZA KUJIFUNZA KWA KUTUMIA HII BLOG YAKO.
ReplyDelete