KUKU HUYU NI RAHISI SANA KUPIKA, UNAWEZA HIFADHI KATIKA FRIJI KWA MUDA WA MWEZI NA CHAKULA BADO KIKAWA NA LADHA SAFI KABISAWAANDALIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE
MAHITAJI
1 kitunguu kikubwa
1/2 kuku au 1 kuku mzima
4 nyanya zilizoiva vizuri katakata au saga katika blenda
2 vijiko vikubwa vya chakula nyanya ya kopo
2 vijiko vikubwa vya chakula nyanya ya kopo
3 ufuta mkavu kijiko kikubwa cha chakula
4 kijiko kikubwa cha chakula karanga ya kusaga iwe mbichi au ilyokaangwa sawa tu
2 kijiko cha chakula mafuta ya kupikia maana karanga inamafuta mengi
1 chumvi kijiko kidogo cha chai
2 fungu la majani ya girigilani ( corrender leaves)
1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu
weka mafuta ya kupikia na kitunguu katika sufuri kaanga kidogo kisha weka kitunguu swaumu
Kisha weka nyanya ya kopo endelea kukaanga
kisha weka kaanga iliyosagwa endelea kukoroga vizuri
baada ya kukorogasafi na mchanganyiko wako kua mzito na safi kabisa huu ndio muonekano wake kisha weka chumvi
kisha weka majani ya girigilani au corriender leaves na ukoroge vizuri
kisha weka nyanya uliyokua umesaga
koroga na acha ichemke vizuri ili nyanya iive vizuri
Hapa sasa nyanya imeiva safi na imechemka ya kutosha imeshabadilika rangi na mchuzi wote umekua na ladha ya karanga
Kisha weka vipande vya nyama ya kuku inapendez kama utakua umeichemsha ika iva pia usimwage ule mchuzi au maji uliyochemshia huyo kuku utayatumia hapa badala ya kuongexza maji unatumia mabaki ya mchuzi ulio chemshia huyio kuku ili kulinda ladha ya chakula hik
MWISHO KABISA PAKUA KUKU NA WEKA KATIKA CHOMBO CHA MLAJI KIHA MWAGIA JUU ULE UFUTA MALAJI ATAKAPOKUA ANAKULA UTAUTAFUNA UFUTA LIVE NA KUONGEZA LADHA SAFI KATIKA CHAKULA CHAKE KAMA UNAPIKA KWA FAMILIA AKUBWA BASI BAADA YA KUKU WAKO KUIVAMWAGIA UFUTA NDANI YA MCHUZI NA KOROGA VIZURI ILI UCHANGANYIKE KISHA WEKA MEZANI FAMILIA IFURAHIE
hii nini hamu ya kui-test inaelekea ni tamu sana.
ReplyDeleteTupe recipe kaka. Asante sana.
Chef Issa tunaomba ss usiwe na haraka maana unatowa picha alafu unasema subiri recipie kama hiyo ya kuku wa ufuta mbona kama kazi inakushinda bro??? ss tunabaki tunasubiri hatutaki mambo ya picha twataka vitendo haya ona ss usharukia mandazi ya iliki hujamaliza chapati yaaaaaaak!!!!!!!
ReplyDelete