DAGAA NI WAZURI NA WATAMU SANA ENDAPO UTAWAPIKA VIZURI KWA AFYA YA MLAJI
MAHITAJI
1/2 kilo ya dagaa wa Kigoma au wa Mwanza
2 nyanya kubwa
50 gram kitunguu swaumu
1 pili pili hoho kubwa
1 bilinganya saizi ya kati
35 gram mafuta ya kupikia
JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO CHINI KATIKA PICHA
Muonekano wa mahitaji yako
weka mafuta katika kikaango yakipata moto kaanga vitunguu maji na kitunguu swaumu
kisha weka nyanya fresh iliyokwisha katwa katwa
kisha funika ichemke taratibu ili nyanya iive
baada ya dakika 5 funua nyanya itakua imelainika
weka mchanganyiko wa pili pili hoho na bilinganya pamoja na dagaa walioosha safi kabisa kwa maji
badaa ya hapo koroga vizuri mchanganyiko wote uchanganyike safi kabisa
kisha weka kitunguu swaumu hicho ni kifaa maalumu cha kuponde kitunguu kinauzwa madukani
Kisha weka binzali ya kopo iliyochanganywa na tui la nazi kama huna basi kuna nazi weka tui kuongeza ladha sio lazima
Nazi kawaida huwa ina mafuta lakini mafuta haya ni salama kwa mlaji ikiwa huli mara kwa mara pia yanasaidia kukaanga mchuzi wako uwe safi na mboga zilainike vizuri
HAYA NDIO MAPISHI YA DAGAA WA KIGOMAKUCHANGANYA PILI PILI HOHO NA BILINGANYA WAPIKIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE CHAKLA HIKI UNAWEZA KULA NA MAHARAGE NA WALI AU UNAWEZA KULA NA UGALI KAMA WENGI TULIVYOZOWE NYUMBANI NA INAPENDEZA SANA SANA
Hapo sasa umetufikisha sisi waswahili.tupe vitu basi kaka.
ReplyDeleteurakoze chane. Unaturudisha UJIJI.
ReplyDeleteFUNGA KOLOMO. Asante sana.
Yaani kaka Mungu akubariki zaidi, cant wait for the recipe yake na hiyo ya sambusa.
ReplyDeletecan't wait weka vitu kaka !!!!
ReplyDeletetuna kusubiri kwa hamu kaka kwani recipe hii inatugusa sana sisi tuishio uswahilini. tupe vitu.
ReplyDeleteYaani hapa karoho kamefanya pa paaa
ReplyDeleteNimejaribu leo kupika kwa kweli ni watamu mno na familia yangu wamefurahia mno chakula hiki. Mungu akujaalie sana kaka kwa kutupa mambo mazuri.
ReplyDeleteahh yaani nimeangalia huku mate yanadondoka!!
ReplyDeleteAsante sana kaka
mmh mi hapa yani natamani ka ugali tu dah tena mida ya lunch. thanks bro mume wangu anavopenda dagaa.........
ReplyDeleteHEHEE KAKA HAPO UCPIME, HATA SISI WATANGA UMENIKUNA PALE ULIPOCHANGANYA NA BILINGANYA HAPO UMELIANZISHA BONGE LA UCHOKOZI. HONGERA SANA MUNGU AKUZIDISHIE INSHAALAH. NATUMAI TOLEO LAKO LA MAPISHI LINAZIDI KUTUTO SHAVU HASA WALE MABINGWA WA MENYU. SHUKRANI BRO.
ReplyDeleteMm ni kapera ...lol nimejaribu hii recipe imetoka vizuri....Shukrani...kila la kheri
ReplyDelete