SAMOSA NI KITAFUNWA MAARUFU SANA DUNIANI KOTE KINAPENDWA NA WATU WA RIKA ZOTE WAKUBWA KWA WATOTO
MAHITAJI
1/2 Unga wa ngano
1 kilo nyama ya kusaga
1/2 kilo ya kitunguu
1 carroti
1 pili pili hoho
1/2 maji baridi
1/2 kijiko cha chai chumvi
MAHITAJI
1/2 Unga wa ngano
1 kilo nyama ya kusaga
1/2 kilo ya kitunguu
1 carroti
1 pili pili hoho
1/2 maji baridi
1/2 kijiko cha chai chumvi
Huu ndio muonekano a mahitaji yako
kata kitunguu,pili pili hoho na carroti kwa vipande vidogo
huu muonekano wa mboga zilizokatwa
Kaanga vitunguu vikisha iva weka pembeni
Kaanga nyama ya kusaga kisha weka chumvi ili iive na nyama mpaka ikauke maji yote ili samosa iwe na ladha nzuri
kisha weka karoti baada ya nyama kukauka vizuri
kisha weka pili pili hoho
kisha weka vile vitungu vilivyokwisha kaangwa mchanganyiko utakua safi
kisha weka kitunguu swaumu kaanga kiasi na chukua mchanganyiko huu weka pembeni upoe ili nyama na manda visiharibike
chukua unga nusu kilo weka maji nusu kikombe
kanda mchanganyiko wa maji na unga mpaka uwe ngumu ikiwa laini itakatika katika
sukuma mduara mdogo kisha paka mafuta ya kula juu yake
mwagia unga kiasi kuzunguka mduara wote kusaidia manda zisishikane baada ya kuchomwa
kumbuka kusukuma kisha paka mafuta halafu nyunyizia unga kisha zipandanishe kwa juu mpaka zifike
miduara 5 zitatoa samosa 20kisha usukume mduara huo wenye samosa 5 mpaka upate chapati moja nene na pana usawa wa kikaango chako
choma katika kikaango kwa moto wa wastani ili usiunguze choma dakika 2 kila upande kisha geuze
kisha toa ikiwa ya moto anza kuzibandua kwa haraka kabla hazijapoa moja baada ya nyingine
kisha kata kati kwa kati pande nne kwa usawa
kisha kata kuzunguka manda hiyo ili kuweka mzunguko sawa
kisha chukua unga kiasi na maji changanya iwe nzito itatumika kama gundi angalia picha jinsi gundi ilivyopakwa kwa juu
kisha kunja upande wa kuli hakikisha unaandamiza ili gundi ikamate
kisha kunja upande wa kushoto kandamiza pia ili gundi ishike
huu ndio mkunjo wa manda ukiwa na umbo la v
chukua kijiko kisha weka nyama katika manda yako
paka gundi kwa juu kisha funga manda yako
huu ndio muonekano wa sambusa mbichi
choma katika mafuta yenye moto wa wastani ili zisiungue na ziwe kaukau
samosa zkiwa katika moto kumbuka kuzigeuza mara kwa marazisiungue upande mmoja
Nusu kilo ya nyama yakusaga inatoa samosa 40 - 50 kwa matumizi ya nyumbani
Kwa biashara nusu kilo ya nyama ya kusaga na kilo ya vitunguu, karoti 5 napili pili hoho 5 unapata samosa 100
Maandalizi sio magumu sana ila samosa huwa inauzwa ghali sana kokote duniani
HUU NDIO MUONEKANO WA SAMOSA IKIWA IMESHAIVA SAMOSA HII NI SALAMA ANAWEZA KULA MTU YEYOTE KWA WALE WANAOPENDA PILI PILI UNAWEZA WEKA PILI PILI MBUZI AU PILI PILI MANGA ILI KUONGEZA LADHA ZAIDI FURAHIA NA FAMILIA YAKO. UNAWEZA KUZIHIFADI KATIKA FREEZER KWA MIEZI SITA.
Tutafurahi sana ukitupa maelekezo ya sambusa,hapo umetugusa sababu nikitu tunachokula kila leo na twakipenda.
ReplyDeleteYaani hizo nazipenda kuzila tatizo ngozi yake kutengeneza ndio utata.
ReplyDeleteKaka tunasubiria kwa hamu
ReplyDeletekaka umenimaliza na hasa ukiniwekeya shurba ndo tena sina mchezo wa mbali na jiko
ReplyDeletelini utatungenezea ili tujue....tunahamu sana..plz
ReplyDeletekaka hii tupe haraka, duh.
ReplyDeletemama yangu kanifundisha za manda ya chapati za kumimina, nimejaribu tamu sana na rahisi kutengeneza.
Samahani
ReplyDeleteLakini nafikiri una matatizo ya temperature ya mafuta unayotumia kukaanga sambusa. Sura ya sambusa hizi ni kama chapati, rangi yake ingependeza kuwa nice brown.
Nisamehe mimi ni mlaji sio mpishi
Wakatabahu
tunasubiri kaka maana ni mpenzi sana wa kula sambusa lakini sinavyotengenezwa sijui. hivyo nasubiri kwa hamu kubwa sana.
ReplyDeleteMie napenda sana sambusa ila kasheshe kwenye kutengeneza manda hapo ndio kazi. I will try this weekend to make samosa.
ReplyDeletekaka tunakushukuru sana kwa kuokoa jahazi zima la menyu mungu akubariki uzidi kudumu inshaalah.
ReplyDeletemie ni mpenzi saana wa sambusa kababu na catles na bites nyingine lakini swala zima la manda ni ishu, for the first time zilikataa lakini sikuchoka kesho nikazama kweye blog kumbe ulituwekea angalizo kwamba unga uwe mgumu kwani ukiwa laini zitakatika kwa kweli niliporudia kwa mara nyingine it was wonderful. big up bro.
Hi Kaka issa.
ReplyDeletenimependa blog yako ya mapishi! watu wale msosi mtamu..
mie napenda sana samosa lakini kwa bahati mbaya nina alergy na nyama je unaweza post maandalizi ya samosa kwa ajili ya Vegetarians? tafadhali.. na pia ukipata nafasi ya kupost ki2 kipya jaribu kupitia comments za watu, baadhi wana maswali,mapndekezo n.k Asante.
Hi, maelekezo yako ya kina yamenifaa sana kwa mapishi ya sambusa. big up kaka.
ReplyDeleteNice Nimependa
ReplyDeleteDuh, Pishi saaaaaaafi hizo sambusa noma. BIG UP
ReplyDeleteAsante sana...
ReplyDeleteNapenda mno sambusa ila kutengeneza manda ndio ilikuw tabu yangu....wacha nijaribu leo na mie familua ifurahie