Tuesday, June 29, 2010

SPAGHETI NA NYAMA YA KUSAGA MHHHH YAM YAM!!!!

SOON UTAPATA RECIPE SAFI YA NYAMA YA KUSAGA NA SPAGHETI SAFI KABISA KAA TAYARI

MAHITAJI


1 Kilo nyama ya ng'ombe ya kusaga
2 nyanya kubwa ya kuiva katakata vipande vidogo

1kitunguu kikubwa kata kata vipande vidogo vidogo
1karoti kata kata vipande vidogo vidogo
50 gram kitunguu swaumu
1 leeks kata vipande vidogo vidogo

1 kijiko kikubwa cha chakula unga wa ngano
2 mafuta ya kupikia kijiko kikubwa cha chakula
5 gram chumvi na pili pili manga

1 kopo la nyanya ya kopo


Huu ni muonekano wa kitunguu, leeks na karoti katika mkato wa maumbo madogo


Pasha kikaango au sufuria tayari ukiwa umeshaweka mafuta. Kisha ongeza kitunguu, kitunguu swaumu, karoti na leeks kaanga mapaka zilainike kiasi.

Kisha weka pili pili manga, chumvi na nyama ya ng'ombe iliyosagwa kaanga katika moto mkali zaidi na kumbuka kukoroga koroga marakwa mara ili nyama isishikane na kujibumba madongo madonge hakikisha unakaanga mpaka inaiva.

Kisha weka nyanya ya kopo na kijiko cha unga wa ngano kaanga na koroga ichanganyike vizuri. Mwisho weka nyanya fresh endelea kukoroga. Punguza moto na funika sufuri, pika kwa dakika 10 ukiwa unachungulia na unakoroga pole pole.


Unaweza kupakua na kumpa mlaji spagheti hii kwa staili mbili toafauti moja ni hii chukua spagheti zako ulizochemsha kisha zichanganye katka sufuri uliyopikia nyama ya kusaga kisha pakua weka kwenye sahani tayari kwa kumpatia mlaji ikiwa tayari umeshachanganya vizuri kumbuka kupamba kwajuu kuongeza muonekano thabiti na chakula kivutie.



Staili ya pili ni hii hapa chukua spagheti ulizo chemsha zikaiva vizuri kisha weka katika sahani halafu chukua nyama ya kusaga kisha weka juu ya spagheti hakikisha unaweka staili kama ya mlima na juu ya nyama ya kusaga iliyoiva weka jani la giligilani au parsley au mint au basil ilimradi uwe na mchanganyiko wa rangi nzuri na chakula chako kivutie.

5 comments:

  1. pia naomba naomba siku uje uelekeze jinsi ya kupika mkate au skonsi na keki.thanks

    ReplyDelete
  2. asante
    nilipika hii kitu ingawa mimi sikuweka unga wa ngano...
    kuipika hii nyama ni rahisi sana na inanoga sana

    endelea kutupa mavituz mkuu!!

    ReplyDelete
  3. Jamani kwa kweli hii site mimi naipenda sana. Imenifundisha mapishi mengi ambayo nilikuwa siyajui..Nakupongeza sana ndugu Issa, endelea kutuletea mapishi moto moto..

    ReplyDelete
  4. Ahsante CHIEF...Leo nataka nianze na hii nyama ya kusaga,unajua nn Issa,nataka nitengeneze story kama ya JULIE&JULIA..............BT HII ITAKUWA ISSA&RAHMA.
    Ntakuinbox FEEDBACK.

    ReplyDelete
  5. Nashukuru sana kaka Issa kwa mapishi mazuri...Ila naomba kuuliza, kwa nini tunaweka unga wa ngano katika hayo mapishi yetu?

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako