Wednesday, June 30, 2010

UNAJUA JINSI YA KUTENGENEZA BURGER

WATOTO WENGI SANA WANAPENDA KULA BURGER HATA WATUWAZIMA PIA HUPENDA KULA SIKU MOJA KATIKA CHAKULA CHA MCHANA WATENGENEZEE
FAMILIA WAFURAHI

Kwaujumla napenda sana burger ya kutengeneza nyumbani, na ninapenda kutengeneza mwenyewe au mke wangu lengo ni kuhakikisha viungo na mchanganyikowote unakua sawa. Kwakutmia recipe hii unaweza kutengeneza 8 -10 hamburgers Inategemea utaweka upana gani wa nyama yako.Baada ya kuandaa unaweza kuhifadhi mchanganyiko huo wa nyama kwenye freezer kwa matumizi ya baadae.
MAHITAJI

 1 kg nyama ya kusaga safi 
 240 gram kitunguu kilichokatwa katwa vipande vidogo 
 60 gram bread crumbs ( Unga wa mikate)
 1 kijiko cha chakula Worcestershire sauce
 2 cloves of garlic, peeled and minced
50 gram kitunguu swaumu
 5 gram chumvi
 5 gram pili pili manga
1 lettuce
1 kitunguu
2 nyanya fresh

Katika bakuli kubwa changanya nyama pamoja na kitunguu, bread crumbs, Worcestershire sauce na kitunguu swaumu kisha weka . Kisha changanya safi na gawa katika mafungu 8 au 10 kulingana na ukubwa unaopenda wewe.
JINSI YA KUPIKA

Unaweza ukakaanga kwenye kikaango au ukapika kwa moto wa 160 degrees katika oven. Chukua mkate wa burger kisha kata katika pande mbili kisha paka mayonnaise na tonato  ketchup kwenye mkate upande wa chini, ongezea lettuce, slice kitunguu na nyanya fresh na slice ya tango la kopo. Nyunyizia chumvi kidogo mpatie mlaji ikiwa yamoto





4 comments:

  1. hi,asante kwa mapishi mbalimbali unayotupatia,nimeelewa jinsi ya kupika sphageti ya nyama,na sasanasubiria ya nyama ya kusaga pamoja na burger,ila naulizia je kama huna mboga ya giligilani ni lazima kutumia?au naweza kutumia mboga yeyote ya majani?thanks

    ReplyDelete
  2. asante sana chef kwa mapishi yako mazuri na maelezo murua kabsa na ya kueleweka,tunashukuru sana,naomba pia ikiwezekan utuonyeshe na pishi la kachori, na swali langu la mwisho je kama hutaki ku-fry samosa , kachori, kababu unaweza ku-grill! asante, siku njema

    ReplyDelete
  3. Kaka wapenzi wa chicken tandoori hujatuwekea recipe!!!!!!

    ReplyDelete
  4. si watoto tu,hata watu wazima ndiyo maradhiyetu

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako