Friday, June 18, 2010

TENGENEZA KEKI YA TUNDA TUFAA ( APPLE)

HII NI KEKI NZURI YA TUFAA AU APPLE SAFI KULA BAADA YA CHAKULA AU UNAWEZA KULA NA CHAI YA SAA 10 JIONI

MAHITAJI

170 gram siagi
170 gram sukari
1/2 kijiko kidogo cha chai kwaruza ganda la limao
4 mayai mabichi sawa na (210 gram)
275 gram unga wa ngano
1 kijiko kikubwa cha chakula baking powder
100 gram maziwa ya maji au cream
ca. 20 lavender leaves
3 au 4 apple kata vipande vidogo vidogo
3 kijiko kikubwa cha chakula
60gram majani ya mchai chai (lemon grass)

JINSI YA KUANDAA

Changanya sukari na siagi kwa uwiano wa uzito sawa ile ya gram 170 mpaka ichanganyike vizuri.

Kisha weka chenga za limao ulizokwaruza pamoja na mayai endelea kuchanganya

Kisha weka unga wa ngano na baking powder enedela kuchanganya kiasi

kisha ongeza maziwa na mchai chai ulikatwa vipande vidogo vidogo

kisha mimina mchanganyiko wako kwenye chombo unachotumia kuokea

kisha chomeka katika mchanganyiko wako vipande vya apple safi vienee

mwisho chukua vile vijiko vitatu vya sukari juu ya mchanganyiko wako

choma katika oven kwa moto wa nyuzi joto 175°C kwa dakika 45 mpaka 55 mpaka iwe rangi ya kahawia safi kisha itoe ipoe tayari kwa kuliwa.



Huu ni muonekano wa mmea wa mchai chai na majani yake


Huu ni muonekano wa shina la mchai chai na ndio inahitajika kwajili ya keki yako kata vipande vidogo vidogo sana kisha tumia katika mchanganyiko wako wa keki kwa harufu na ladha safi

Huu ni muonekano wa rangi nzuri ya juu safi wa keki yako baada ya kuiva



Huu ni muonekano safi kabisa baada ya kuikata keki yako unaona vipande vidogo vidogo vya mchai chai na tunda tufaa au apple. Unaweza kula ikiwa ya moto au ikiwa imepoa yote sawa pia unaweza kuhifadhi katika friji kwa muda wa wiki moja tu.





1 comment:

  1. Assalam aleykum kaka Issa,
    mh yaani mate yananitoka baada ya kuiona keki hiyo itabidi nijaribu kuipika ,asante kwa mafunzo na ndoa zetu zinazidi kushamiri kwa kubadilisha mapishi, tunakushukuru sana,big up

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako