Tuesday, July 27, 2010

JINSI YA KUANDAA KACHORI AU KATLESS

 KACHORI  HUTUMIKA KAMA KITAFUNWA KWAJILI YA PICNIC, CHAI YA ASUBUHI AU SAA 10 JIONI HUPENDWA SANA NA WATU WA LIKA ZOTE. KACHOLI HII NI MAALUMU KWA WALE WENYE MATATIZO WASIOTUMIA UNGA WA NGANO.

MAHITAJI

300 gram nyama ya kusaga
1 kilo ya viazi ulaya (5-6)
1 kijiko cha chakula Mafuta ya kupikia
½ kijiko kidogo cha chai Cumin seeds (Jeera) 
1 ½ kijiko kidogo cha chai Coriander powder (Dhaniya) 
2 pili pili mbuzi au ndefu za kijani 
1 ½ Tangawizi mbichi
¼ Kijiko cha chai Garam Masala
4 kijiko kikubwa cha chakula maji ya limao au ndimu
 ½ chumvi
10 gram kitunguu swaumu
5 mayai ya kuku
Mafuta kwajili ya kukaangia

 
JINSI YA KUTENGENEZA

Chemsha viazi kwenye pressure cooker au sufuria vikiwa na maganda yake.

Chemsha nyama ya kusaga na maji 50 gram, kitunguu swaumu 10 gram na vijiko 4 vya mai ya limao mpka iive kisha weka pembeni.

Kisha menya viazi ulivyochemsha kisha kata katika vipande vidogo. Pasha mafuta ya kupikia kijiko kimoja kwenye kikaango.

Kisha weka mbegu za cumin kwenye kikaango. Mbegu za cumin zikishapasuka, ongeza coriander powder, pili pili mbuzi, Tangawizi, Kisha weka chumvi na viazi. Kaanga kwa dakika 2-3 itakua imeiva vizuri.
Kisha ponda mchanganyiko wako mpaka uwe laini kabisa

Kisha chukua mchanganyiko huo laini wa viazi na tengeneza maumbo madogo ya mviringo ukubwa kama limao kisha bonyeza kwa kutumia kidole kati kati ya umbo hilo utapata nafasi ya kuweka kijiko kimoja cha chai nyama ya kusaga iliyoiva kisha funika kwa kutumia viazi na jitaidi kuviringisha tena kwa kutumia mikono yako miwili ili upate umbo zuri.



Baada ya kumaliza kuandaa maumbo safi kabisa ya duara na yenye nyama ya kusaga kwa ndani, piga mayai pembeni kwenye bakuli na chovya umbo moja moja na weka kwenye kikaango chenye mafuta ya moto kaanga ukishapata rangi tu ya kahawia toa maana viazi na nyama vimeshaiva unachotafuta ni kau kau na rangi safi ya kahawia pande zote.

MPATIE MLAJI KACHORI HII IKIWA YAMOTO PIA UNAWEZA USIWEKE PILI PILI NA TANGAWIZI HASA KWA WALE WANOSUMBULIWA NA VIDONDA VYA TUMBO AU MATATZIZO YA GESI TUMBONI NA BADO KACHORI YAKO IKAWA SAFI SANA. UNAWEZA KULA NA TOMATO SAUCE, MAYONAISE, CHACHANDU AU ACHALI.


KITAFUNWA SAFI SANA KWA FAMILIA YAKO

MAJIBU YA MASWALI KUHUSU KATLESI AU KACHORI???
KACHORI NI STAILI YA UPISHI WA CHAKULA CHA WATU WANAOTUMIA MBOGA MAJANI TU NA ASILI YAKE NI INDIA NA KAWAIDA INATENGENEZWA NA UNGA WA NGANO KISHA UNAWEKA KATIKATI MCHANGANYIKO WA VIAZI KAMA HAPO JUU KWENYE RECIPE YATU KISHA UNATENGENEZA MAOMBO SAFI YA DUARA. UNACHOVYA KWENYE UNGA WA DENGU ULICHANGANYWA NA MAYAI NA UNAKAANGA KWENYE MAFUTA MAPAKA UPATE RANGI YA KAHAWIA.

KATLES KWA WATU WENGI NI MCHANGANYIKO HUU WA VIAZI KAMA HAPO JUU KWENYE RECIPE NA KISHA UNAWEKA KATI NYAMA YA NG'OMBE, SAMAKI AU KUKU NA HATA UNAWEZA WEKA MBOGA MAJANI NA BADO UTAITA KATLESI KWAKUA NAMANA YA UTENGENEZAJI NI HIYO HIYO KIKUBWA KATI KUWE NA AINA YEYOTE YA CHAKULA UNACHOPENDA WEWE.

KUTOKANA NA AINA HII YA UTENGENEZAJI WA VYAKULA VYOTE HIVI VIWILI KWA WALE WASIOTUMIA UNGA WA NGANO BADO WANAWEZA KUITA KACHORI INGAWA HAWAJATUMIA UNGA WA NGANO. NA KWA WALE WANAO KULA UNGA WA NGANO INGAWA WAMETUMIA VIAZI TU HII WATAITA KATLESI. HAIBADILISHI MAANA INGAWA UHALISIWA WAJINA NA UPUNGUFU WA RECIPE UNATEGEMEA WEWE MLAJI MAJINA YOTE NI SAHIHI.

NASHUKURU SANA KWA MASWALI YENU NAIMANI MTAKUA MMENIELEWA VIZURI.


5 comments:

  1. Asante sana Chef Issa!
    Mungu azidi kukubariki sana kaka yangu!. Ninashukuru kwa kujali maombi ya wasomaji wako.
    Mama Jeremiah

    ReplyDelete
  2. Hii kachori au catles. Maana kachori haiwekwi nyana katikati. Inakuwa ni viazi tu na huchomwa kwa kupakazwa unga wa dengu uliopigwa kwa mayai

    Chef issa hebu nisaidie au nimajina tu
    Mdau
    Hongera kwa mapishi

    ReplyDelete
  3. nimekuelewa ila nina swali moja hizi ni kachori au katlesi samahani sina nia mbaya nauliza tu kwa kule kwetu znz huwa kachori hatuweki nyama ni katlesi ndo tunaweka nyama
    samahani lakini yote nauliza tu ili nijuwe zaidi
    asante kaka isa kwa upishi

    ReplyDelete
  4. apo kaka isa umekosea hizi si kachori ni katlesi kachori haziwekwi nyama ila hebu tuwekee kachori zenyewe

    ReplyDelete
  5. Hizi mbegu za cumin na coriander ni nini kwa kiswahili maanA nataka kupika nasijui hivyo vitu nitapata wapi

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako