Friday, July 30, 2010

JINSI YA KUPIKA PRAWNS MASALA

MAHITAJI
1 kg Prawn
5 vitunguu vikubwa chop chop
3 nyanya kubwa za kuiva chop chop
3 kijiko kikubwa cha chakula Ginger-garlich paste
6-7 kijiko cha chakula mafuta ya kupikia
1 kijiko cha chakula Turmeric powder
1 kijiko cha chakula Coriander powder
1/2 kijiko cha chakula Garam Masala
2 kijiko cha chakula maji ya limao
10 gram chumvi
240 gram maji ya baridi
majani ya Coriander chopped kwajili ya kupambia

JINSI YA KUPIKA
1. Safisha prawns  toa magamba kisha iwekee ladha kwa kuchanganya cumvi 10 gram,1/2 kijiko cha chakula turmeric powder, 1 kijiko cha chakula ginger-garlic paste, na maji ya limao kwa dakika 30.
2. Kisha pasha moto sufuria weka mafuta ya kupikia, weka kitunguu maji na endelea kukaanga. Kisha weka  ginger-garlic paste endelea kuchanganya mpaka iwe rangi ya kahawia.
3. Kisha weka garam masalas, na nyanya endela kukaanga mpaka ziive na mafuta yaanze kuonekana kwa juu.




Kisha weka wale prwans waliokua umewaandaa na kisha koroga vizuri ichanganyike na funika na mfuniko kwa dakika 4 mapaka 5 kwa moto wa wastani ili isiungue



Kisha weka maji na koroga vizuri tena ichanganyike safi kabisa funika kwa dakika 4 na funua ukishaona mchuzi unakua mzito na mafuta yanakuja tena juu itakua imeshaiva



Huu ni muonekano safi kabisa wa prawns masala yako ianvutia kwa rangi na inatamanisha sana kwa harufu



Hapa ni muonekano imeandaliwa kwa mlaji kwa kula na wali pamoja na mboga majani.

MAPISHI HAYA HAYA UNAWEZA TUMIA KWA KUWAPIKIA FAMILIA AU HOTELINI WAGENI WAKO. MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI, NYAMA YA KUKU, NYAMA YA MBUZI AU KONDOO NA PIA NYAMA YA NG'OMBE ILA KWA KUPIKA NYAMA HIZO NILIZOTAJA CHEMSHA KWANZA ZIIVE KISHA NDIO UWEKE KWENYE MCHANGANYIKO WA MASALA SAUCE YAKO. USITUMIE MAJI KUMBUKA KUTUMIA MCHUZI UTAKAO BAKIA KWENYE SUFURIA BAADA YA KUCHEMSHA NYAMA YAKO. NI RAHISI SANA NA INAPENDEZA.


No comments:

Post a Comment

Tunaheshimu sana maoni yako