Thursday, August 5, 2010

DONUT DONUT MHHHHHH SUPER DUPER!!!!!!

KITAFUNWA SAFI SANA HIKI KAA TAYARI RECIPE SAFI KABISA KWA MTINDO TOFAUTI KAMA UONAVYO KATIKA PICHA HAPO CHINI

MAHITAJI

2 Kijiko kikubwa cha chakula white vinegar
480 gram maziwa ya maji
2 kijiko kikubwa cha chakula siagi yeyote ile
120 gram sukari
1 yai
1/2 kijiko kidogo cha chai vanilla esence
480 gram unga wa ngano
1/2 kijiko kidogo cha chai baking powder
1/4 kijiko kidogo cha chai chumvi
1.5 lita mafuta kwajili ya kukaangia 
120 gram sukari ya unga kwajili ya kunyunyizia kwa juu

JINSI YA KUANDAA

Mimina vinega kwenye maziwa, acha kwa dakika 5 hadi 10 maziwa yakatike na yawe mazito

Katika bakuli la wastani, changanya siagi na sukari mpaka vilainike kabisa kisha endelea piga yai na vanilla navyo vichanganyike vizuri kabisa.



Huu ni muonekano safi kabisa baada ya mchanganyiko wako kua laini kisha changanya kwa kutumia mchapo unga wa ngano, baking powder, na chumvi; Kisha chukua mchanganyiko wa maziwa na vinega mimina kwenye mchanganyiko huu wenye unga na siagi.



Huu ni muonekano wa mchanganyiko safi kabisa umeshakua mzito na umelainika safi sana


Sukuma mchanganyiko wako kama inavyooonekana kwenye picha na kisha kata miduara safi ya umbo la donut na kati kati toboa pia. Acha ya kae katika joto la chumba kwa dakika 10 iumuke.
Pasha mafuta kwenye kikaango chako kwa 375 degrees F (190 degrees C).



Kaanga donut zako kwenye mafuta moto mapaka upate rangi nzuri ya kahawia, Kumbuka kugeuza mara kwa mara ili yasiive upande mmoja tu. Toa katika kikaango na weka katika wavu au towel ili inyone mafuta.



Kwakutumia unga ule ule unaweza ukatengeneza hizi donut za mviringi (donut rolls) kisha kaanga na ukimaliza kabla hazijapoa zimwagie sukari ya unga zitakua tamu sana na muonekano tofauti


Huu ni muonekano safi sana wa donut yako iliyoiva na isiyo na mafuta kabisa ndani na juu ina gamba safi gumu litakalo kufanya ufurahie sana na usikinai kula hata zikiwa 10.

RECIPE HII NI SPECIAL NAINANI WENGI WENU HAMUIJUI WAPIKIE FAMILIA WAFURAHIE PIA UNAWEKA WEKA CHOCOLATE JAM YA LADHA YEYOTE ILE KATI KATI YA DONUT YAKO ILI KUONGEZA LADHA. MAFUNZO YAJAO NITAONYESHA JINSI YA KUONGEZA LADHA HIZI TOFAUTI.

NAWATAKILA RAMADHANI NJEMA WAPENZI WOTE WA BLOG AMIIN!!!


8 comments:

  1. jamani tunasubiri donut kwa hamu si unajua ramadhani hyo

    ReplyDelete
  2. chef jamani naisubiri kwa hamu sana hii recipe,plz naomba uilete sasa.

    Thanx.

    Mariam

    ReplyDelete
  3. Mhh, naona tunafunga karibuni, sijui utafanyaje ili usitutamanishe

    ReplyDelete
  4. habari... wow asante sana na hongera nimekuwa natumia sana receipe zako ktk chakula kwa familia yangu


    sasa nawezaje kupima maziwa ya maji kwa grm. unaweza ukanimbia kwa lita?

    asante sana

    ReplyDelete
  5. nimejaribu hii recipe haikuwa kama ulivyo saggest maana maziwa yamekua mengi kupita unga matokeo yake ikabidi niongeze unga ebwana hapoo ndipo lilipotoka andazi si andazi mauzauza matupu nilijuta kuchezea unga na vitu vyangu na fikiri ulikosea chefu wewe mwenyewe angalia unga gram 480 na maziwa 920gm mhhhhhhhhhhh.

    ReplyDelete
  6. Habari yako chef,kaka aliyosema mdau hapo juu nikweli kabisa hata mimi nimejaribu kwa kutumia hivyo vipimo vyako ni diseaster,tunaomba ucheki tena na hivyo vipimo ulivyotupa haviendani kabisa na huo muonekano wa hapo juu.

    1.Ushauri kama inawezekana kaka tuwekee vipimo vya kilo moja ya unga hiyo itakuwa rahisi.

    2.Pia kama inawezekana mimi binafsi ningeomba kama ungeweka video yako unapotengeneza hizo donats kuanzia stage ya kwanza kabisa mpaka mwisho ili tuweze kufuatilia vizuri hatua moja mpaka ya mwisho,nina hamu sana ya kujua kutengeneza hii kitu.

    3.Asante sana kwa kazi yako nzuri umekuwa ni msaada wangu mkubwa katika kujifunza mapishi tofauti tofauti nisiyoyafamu kupika,nimejaribu mengi na nafuata vipimo vyake yanatoka bomba,utazni nimepitia chuo cha mapishi, ila kwa Donats nimegonga mwamba.

    Please, please tunahitaji msaada kwa hili.

    Kazi njema kaka,mungu azidi kukupa afya njema.

    ReplyDelete
  7. pole na kazi chef wetu, tunakupenda.
    hii hakuna hamira kabisa?

    ReplyDelete
  8. habari kaka ninaomba uwe unaandika hivi vipimo kwa size ya vikombe au vijiko ni rahisi kuelewa kwa gram kidogo ngumu wengine hatuna vipimio vya gram naomba urudie tena resepi ya donut naomba sana uandike kwa vikombe au vijiko asante kaka kwa muda wako

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako