MAHITAJI
1 paketi ya spaghetti au tagliatelle
1 Kijikokikubwa cha chakula olive oil
8 vipande vya bacon ( ya nguruwe au ya ngombe au Bata mzinga) chop chop
1 tablespoon olive oil
1 Kijikokikubwa cha chakula kitunguu maji chop chop
5 gram kitunguu swaumu kilichosagwa
30 gram dry white wine (Sio lazima)
100 gram fresh cream
4 mayai
120 gram Parmesan cheese ya unga
10 gram ya pili pili manga na chumvi
2 Kijikokikubwa cha chakula chopped fresh parsley
2 Kijikokikubwa cha chakula Parmesan cheese ya unga pia
JINSI YA KUANDAA
Weka chumvi katika maji kisha chemsha, yakisha chemka weka pasta yako iive wastani isirojeke. Kisha chuja vizuri maji yote na weka kijiko kimoja cha olive oil changanya vizuri hii husaidia pasta isishikane, iweke pembeni.
Wakati huo huo pika chopped bacon katika kikaango chenye mafuta kiasi mpaka iwe crisp; Kisha itoe na tumia kitambaa kuikausha kutoa mafuta. Chukua kijiko kimoja cha olive oil kilichoakia, kisha weka kwenye kikaango juu ya moto. Ongeza chopped kitunguu maji, kisha pika katika moto wa wastani mpaka vitunguu vilainike. Kisha ongezea kitunguu swaumu, kaanga kwa dakika moja tu. Kisha weka wine kama unapenda; pika kwa dakika moja tena.
Baaada ya hapo chukua ile bacon iliyoiva weka kwenye kikaango; Kisha weka pasta yako pia. , ongeza tena olive oil kisai kama inaonekana kukauka au inashikana . Vunja mayai yapige pige na cream kwa mchapo na kisha mwagia ndani ya pasta pole pole huku ukichanganya kwa kutumia uma au tongs mpaka mayai yachanganyikane na pasta yako saafi. QHaraka haraka ongeza 120gram Parmesan cheese, kumbuka kuchanganya tena. Ongeza chumvi na pili pili manga kwaajili ya ladha safi (Kumbuka kua bacon na Parmesan zina chumvi).
Kisha itakua imeiva mpatie mlaji haraka sana rushia kwa juu chopped parsley pamoja na ile Parmesan cheese iliyokua imebakia.
Huu ndio muonekano wa pasta tagliatelle
Huu ni muonekano wa bacon na brocoli
Huu ni mchanganyiko wa mayai na fresh cream
Huu ni mchanganiko wa mayai yaliyopigwa na cream kisha yakamwagiwa kwenye kikaango chenye vitunguu na bacon chop chop
Huu ni muonekano wa mchanganyiko mzima wa pasta na viuno vyote pia imeongezewa na brocoli kuongeza ladha zaidi unaweza tumia mboga aina yeyote ile
Huu ni muonekano wa pasta tagliatelle imeshaiva na tayari kwa kuliwa juu imerushiwa chop parsley na parmesan cheese ukweli ni tamu sana sana.
Kwa kutumia recipe hii unaweza ukatumia aina yeyote ile ya pasta na ikaiwa jina la aina hiyo ya pasta mfano katika picha hiyo hapo juu inaitwa spaghetti carbonara ukitumia pene pasta itaitwa pene pasta carbonara.
ENJOY NA FAMILIA YAKO CHEERS!!!!
MIMI MPENZI WA PASTA NASUBIRI KWA HAMU.
ReplyDeleteIssa,
ReplyDeleteHapa, hii mix ya mayai, je ni yai zima au ni yoke pekee?