MAHITAJI
3 Mayai
240 gram unga wa ngano ( Self raising flour)
120 gram castor sugar
1 Kijiko kikubwa cha chakula castor sugar
1 Kijiko kikubwa cha chakula maji ya vugu vugu
120 gram apricot jam, au trawberry jam au chocolate au custard
1 Kijiko kikubwa cha chakula icing sugar
Siagi kidogo iliyoyeyushwa kwajili ya kubrushia
JINSI YA KUANDAA
Pasha oven kwa moto 200º C. Paka siagi iliyoyeyushwa kwenye chombo utakachotumia kuokea keki yako (flat baking tray) Kisha weka karatasi isiyopitisha mafuta kama huna basi tumia karatasi nyeupe isiyo na mistari kumbuka nayo kuipaka siagi vizuri na uiweke katika chombo utakachotumia kuokea.
Chukua mayai pamoja na sukari tumia mashine ya kuchanganyia changaya mpaka mchanganyiko wako uwe laini na utoe mapovu kabisa.
Baada ya mchanganyiko huo kua laini safi na mapovu chukua unga na anza kuchanganya safi kwa kutumia kijiko fatilia picha hapo chini.
Kisha mimina mchanganyiko wako safi kabisa na usambaze vizuri uenee sehemu zote kwa usawa.
Choma kwa dakika 8 - 10 mpaka sponge iwe imeiva safi
Kisha chukua karatasi mpya isiyopitisha mafuta (baking paper) kisha ilaze juu ya meza safi. Nyunyiza juu ya baking paper kijiko kimoja cha castor sugar. Pole pole itoe cake yako kwenye chombo ulichookea na ihamishie kwenye baking paper mpya kisha nyunyiza tena castor sugar.
Hatua inayo fata ni kuweka mchanganyiko wa ladha yeyote ile unayopenda na ndio itakayo beba jina zima la chakula chako hichi mfano ukiweka jam itaitwa jam swiss roll na ukiweka chocolate itaitwa chocolate swiss roll au ukiweka custad itaitwa custad swiss roll.
Baada ya kuweka ladha ya chochote ukipendacho wewe hakikisha tendo hili unafanya haraka haraka kabla cake yako haijapoa itakua vigumu kuikunja, anza na pindo dogo dogo mpka uikunje yote iwe duara kwa kuzungusha na kumbuka karatasi lazima ibaki nje. Acha na karatasi mpaka ipoe ndani ya freezer ili ishikane kabisa ikisha poa kabisa a kushikana toa karatasi.
Unaweza nyunyizia kwa juu icing sugar. Kwakutumia kisu kikali kata slice saafi kabisa tayari kwa mlaji kufaidi.
Chukua mayai na sukari weka kwenye bakuli
Tumia machine ya mkono kwa kuchanyania mpaka iwe safi na laini
Mayai na sukari vimeanza kuchanganyika vizuri na rangi ya kiini cha yai inabadilika toka kwenye njano kali na kua njano iliyofifia
Hapa rangi inazidi kufifia na mchanganyiko unachanganyika safi kabisa
Hapa imechanganyika bado kidogo tu itakua tayari
Sasahapa ipo safi na imekua laini na imeweka mapovu imeshapanda na kuongezeka
Weka unga ndani ya mayai haya na unaze kuchanganya pole pole
Changanya kwakutumia kijiko cha chuma au mwiko wa mbao poe pole ili mayai yenye sukari na unga viweze kuchanganyika safi bila kuweka mabonge bonge
Pole pole endelea kuchanganya
Mpaka mchanganyiko wako sasa unakua laini na umechanganyika safi kisha mimina kwenye chombo cha kuokea na choma kwa dakika 8 - 10 kisha toa
Hapa imeiva safi na inaonekana na rangi nzuri ya kahawia itoe haraka kabla haijapoa na weka kwenye karatasi mpya ya kuokea ukiwa umesha nyunyiza sukari yako nyeupe ya chenga
Sasa hapa ipo safi unaweza kuweka mchanganyiko wa ladha yeyote uipendayo na uanze kukunja
Kama nilivyoelekeza awali kua kunja kwa kuanzia kunjo dogo mpaka unamaliza mduara wote hakikisha karatasi inabaki nje kama picha hii inavyoonyesha ili swiss roll yako ikamilike
Kumbuka usikunje kama picha hii inavyoonyesha karatasi ikabaki ndani ule mchanganyiko wako wa ladha ulioweka ndani utashikana na karatasi na hautaweza kuitoa ukiitoa inamana utakua umesha ikunjua swiss roll yako na haitaweza kurudi katika umbo lake tena na utakua umepoteza maana halisi. Na mlaji itabidi ale na karatasi hahahaaaaaaaaaa!
Ukifata maelekezo vizuri swiss roll yako baada ya kupoa vizuri kwenye freezer na ukatoa karatasi ya juu itakua na muonekano huu na hiii ni swiss roll yenye mchanganyiko wa srawberry na custard.
Tumia kisu kikali kata slice safi wapatie familia wafurahie baada ya chakula au chai ya jioni saa 10
Hii ni swiss roll ya ladha ya machungwa na mchanganyiko wa karanga kati kati.
Huu ni muonekano wa chocolate swiss roll
SIO NGUMU KUTENGENEZA NI UFATILIAJI MZURI TU WA JINSI YA KUANDAA HAICHUKUA MUDA MREFU KUANZIA KUANDAA MPAKA KUPIKA NA KUIVA NI DAKIKA 45 TU IFURAHISHE FAMILIA YAKO KWA UBUNIFU.
ENJOY
please andika the recipe, i will love to try it out...they look tamu!...
ReplyDeleteyum yum, du ntajaribu kaka
ReplyDeleteyani hapa nimejaribu nikishakula ftari mida mida nishushie ila bro vp mbona hujasema yale maji ya vuguvugu ni ya nini na je moto naweka ngapi 350 au 250 na je jinsi ya kuweka hayo matunda au jam hiyo kuipaka tuoneshe kwa picha
ReplyDeleteilv culinaryarchamber
kaka mi napenda sana kujaribu kupika swiss rall lakini kunakitu sielewi caster sugar ni sukari ya aina gani?naomba nieleweshe manaake na kutana nayo kwenye kila kitabu cha mapishi
ReplyDeletebasi chef nikupe mchapo wa jikoni nikajaribu hiyo swiss roll aina hiyo hiyo ulio tengeneza wewe. basi ilivyokuja kutoka wakati naikunja nishaweka jam na castard sijui wai haikunjiki kama yako hapo pichani yangu inakatika kastard na jam inachuruzika basi nikajitahidi hivyo hivyo nikaiweka kwenye friji kuja itoa yaani chapeless!
ReplyDeletenipe siri nini nilikosea
ilv culinarychamb
vipi brother issa man you look like like somebody i know just want to ask if you been around mass before any way mimi ni chef katika hoteli yangu ya KITANZANIA HAPA VERMONT INAITWA MARIAM'S NA I JUST WANT TO SAY AS A NEW OWNER AND CHEF I FOUND YOUR BLOG VERY EDUCATING AND nilikuwa naomba kama una tips zozote za biashara hizi kwani its not easy special wakati huu and any advise sio watu wengi ambao wana jua na vyakula vyetu so i have been ask if i can make ethiopian food wich its not my area yes i know there food but not like i konw ours any idea can help im in WINDSOR VT a small town not many black but im close to dartmouth college and hospital and there are african student and doctors around any way anything can help to keep this TANZANIAN RESTAURANT GOING THIS IS MY INFORMATION MARIAM'S RESTAURANT @YAHOO.COM AND ANY BODY AROUND BOSTON,NH, SPRINGFIELD PLEASE COME AND SUPPORT US WERE 70 main st windsor vt thank you by the way my name is ibrahim
ReplyDeleteHey namsaidia alieuliza kuhusu castor sugar.
ReplyDeletenikua inakua kama unga na ukienda madukani utaiona kabisa imeandikwa jina hilo ila niliwahi kumuuliza mpishi mmoja kama nikiwa sina inakuaje akaniambia chukua sukari ya kawaida isage iwe kama unga uitumie. Hope nimekusaidia tumsubiri na chef tuone atatuambia nini..
mdau USA CALIFORNIA
Wow! Soo sweetyy
ReplyDelete