UTANASHATI WA UPAMBAJI WA CHAKULA HUONGEZA SANA MVUTO KWA MLAJI JITAIDI KUA MBUNIFU CHAKULA CHA BEI RAHISI SANA UNAWEZA KUKIFANYA KIONEKANE CHA BEI GHALI SANA NA WALAJI WAKAFURAHIA SANA
MAHITAJI
20 au 30 Vipapatio vya kuku
100 gram maji ya limao au ndimu
15 gram kitunguu swaumu
100 gram mafuta ya kupikia
10 gram chumvi
5 gram pili pili manga
5 gram unga wa binzali
10 gram chicken masala
JINSI YA KUANDAA
safisha vizuri vipapatio vya kuku, kisha vikaushe maji saafi kabisa
chukua mchanganyiko wa viungo vyote hivyo kisha changanya vizuri kabisa ichanganyike na kisha weka katika chombo kwajili ya kuokea kwenye oven.
Kisha funika chombo chako cha kuokea kwa kutumia aluminnium foil kwa dakika 10 kisha toa oka kwa dakika 15 mpaka 20 kwa moto wa wastani ili visiungue viweze kukauka safi na mchanaganyiko wako ushike vizuri kwenye nyama.
Baada ya hapo vitakua vimeiva safi kabisa unaweza kula kwa Ugali, viazi vya kukaanga au wali.
KUMBUKA KATIKA SAHANI YAKO PAMBA VIZURI NA UVIPANGE SAFI KAMA INAVYOONEKANA HAPO KATIKA PICHA ILI KUVUTIA ZAIDI KWA MLAJI HASA WATOTO WANAPENDA SANA MUONEKANO TOFAUTI WA CHOCHOTE KILE KAMA MWANAO HAPENDI KULA BASI MKAMATE KWA KUMPAMBIA CHAKULA ATABADILIKA NA KUPENDA KULA MARA MOJA.
No comments:
Post a Comment
Tunaheshimu sana maoni yako