Friday, October 29, 2010

JIFUNZE KUTENGENEZA SUPU YA MABOGA NA KARANGA (peanut butter)


 RECIPE SAFI KABISA NA RAHISI KUTENGENEZA

Kwa kuchemsha maboga pembeni kisha unayasaga kwenye blenda,Pia bila ya kusahau viazi vitamu na peanut butter. Unapata mchanganyiko wa supu safi sana na tofauti kuliko supu nyingi ulizozizoea. Pia supu hii inavirutubish vingi sana katika mwili. Jenga tabia ya kunywa supu hii itakusaidia sana kujenga mwili na kukupa joto la kutosha hasa majira ya baridi (winters).

MAHITAJI

240 gram maboga yaliyomenywa yakachemshwa  pamoja na kitunguu maji kimoja na kusagwa katika blenda
1 kiazi ulaya kikubwa
60 gram Karanga ya kusaga (peanut butter) laini kabisa
1 kijiko kikubwa cha chakula siagi
480 gram za maji safi na salama
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
Majani ya chives au yeyote yale kwajili ya kupambia


JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO NA PICHA HAPO CHINI


 
Safisha na katakata viazi vitamu kisha visteam katika chombo maalum kama huna basi chemsha tu kawaida katika sufuria.


Vikisha lainika safi toa katika combo hicho. Mi binafsi huwa napendelea sana ku steam badala ya kuchemsha.



Kisha weka katika blenda na uvisage pia unaweza menya ngozi mimi huwa napendelea kuiacha ngozi ili kupata harufu na ladha halisi ya kiazi. 



Katika kikaango, yeyusha siagi na ukaange ule mchanganyiko uliosagwa wa maboga, mchanganyiko wa viazi vitamu pamoja na peanut butter.


Kisha ongezea maji kufanya mchanganyiko wako uwe laini na uweke chumvi na pili pili manga kupata ladha safi. Koroga mpaka iwe laini na imechanganyika vizuri hakikisha unachemsha kwa dakika 10 tu inakua tayari kwa mlaji kumpatia.


 Juu kabisa baada ya kumimina katika bakuli pamba na chives na cream.




MUONEKANO HUU NI SAFI SANA LAZIMA MNYWAJI AVUTIWE HASA NA UKINYWA SUPU HII MARA MOJA TU BASI UTATAKA KUNYWA KILA SIKU. KWA WALE MLIO NA WATOTO MAPATIE SUPU HII MARA KWA MARA MTOTO ATARUDISHA AFYA HARAKA SANA. PIA MLIO KATIKA NCHI ZA BARIDI PATA SUPU HII KABLA YA CHAKULA ILIKUONGEZA JOTO MWILINI.






JIFUNZE KUTENGENEZA SUPU KWA KUTUMIA MBOGA AINA YA CERELY


KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA

MAHITAJI

1 Kitunguu maji kikubwa
 6 au 7 miti ya  celery, safisha na kata ndogo ndogo
3 viazi ulaya vya umbo la kati
1 lita ya maji
1 kijiko kidogo cha chai aromati
1 kijiko kikubwa cha chakula unga wa binzali (curry powder) 
10 gram chumvi na pili pili manga
 5 gram kitunguu swaumu kilicho sagwa

JINSI YA KUTENGENEZA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

    weka katika kikaango kijiko kimoja cha siagi, kisha kaanga kitunguu maji na unga wa binzali (curry powder).


    Kisha ongeza celery na viazi ulaya kaanga kwa dakika 5 pia weka aromati na chumvi.


    Kisha ongezea maji. halafu funika sufuria yako kwa dakika 10 mpaka 15.



    Chukua mchanganyiko wako huu na weka katika blenda saga mpaka upate uji mzito kabisa



    Kisha mimina tena katika sufuria, mwisho kabisa weka pili pili manga na ukoroge.





    Hakikisha unampatia mlaji ikiwa yamoto kabisa toka jikoni ili kupasha tumbo na kuamsha hamu ya kula mlo kamili kisha pamba na majani ya celery.




    JIFUNZE KUTENGENEZA SUPU YA BEETROOT


     RECIPE SAFI KABISA YA SUPU HII ADIMU YA BEETROOT, SUPU HII INAFAIDA TATU KATIKA MWILI WA BINADAMU MOJA INASAIDIA KULINDA MWILI JUU YA KUPATWA NA KANSA, PILI INASAIDIA UTENDAJI KAZI MZURI WA MAINI, TATU NI KUPUNGUZA HATARI YA CHOLESTROL KATIKA MWILI JENGA TABIA YA KUNYA SUPU HII ANGALAU MARA 1 KWA WIKI NDANI YA FAMILIA YAKO.


    MAHITAJI

    2 beetroot, Kisha zisafishe na uzimenye vizuri 
    1 kubwa carrot
    1 celery
    1 kitunguu maji kikubwa
    5 gram kitunguu swaumu
    60 gram nyanya iliyosagwa
    1 bay leaf ( sio lazima)
    3 mbegu za karafuu
    5 mbegu za pili pili manga
    720 gram za maji baridi safi na salama
    5 gram ya chumvi
    90 gram maji baridi safi na salama
    3 kijiko kidogo cha chai juisi ya limao


    JINSI YA KUANDA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI



    Huu ndio muonekano wa mboga aina ya beetroot ikiwa mmbichi



    Katika kikaango weka kijiko kimoja kikubwa cha mafuta ya kula kisha weka vitunguu maji kaanga mpaka vilainike (Kumbuka kukatakata vitunguu katika muonekano huo).




    KIsha chukua kwaruzo au greater na ukwaruze beetroot moja, chukua 90 grama za maji baridi changanya na juisi ya limao kisha chemsha. Usiweke jikoni weka pembeni na ufunike kwa dakika 30.


    Kisha kataka beetrooth, celery na carrot katika maumbo madogo madogo kama muonekano katika picha, kisha weka katika kikaango chenye vitungu na uongezee kitunguu swaumu.Kaanga kwa dakika 2 hakikisha unaweka na chumvi pia.



    Kisha weka ile nyanya ya kusaga na ukaange kwa dakika 2 tena.



     
    Ongezea mbegu za pili pili manga na mbegu za karafuu. Kisha weka maji 720 gram, Kisha pika kwa dakika 20 mpaka 30 mpaka mboga zote ziive na kua laini.




    Kisha toa mfuniko na weka ile beetroot uliyokwaruza pamoja na ju, Acha ichemke kama dakika 1 tu toa mpatie mlaji ikiwa ya moto kabisa na unaweza ukapamda juu na majai yeyte yale ya kijani kuongeza utanashati.
     
     KAMA NILIVYOKUSHAURI WAPATIE FAMILIAYA YAKO ANGALAU MARA MOJA KWA WIKI SUPU HII KULINDA AFYA YA MWILI 

    Thursday, October 28, 2010

    JIFUNZE KUTENGENEZA CHATNEY YA NYANYA


    NI RAHISI KUPIKA NA INAKAA MUDA MREFU KATIKA FRIJI BILA YA KUHARIBIKA

    MAHITAJI

    3 Nyanya kubwa zilizoiva
    4 kitunguu maji katakata
    3 pilipili kavu au ya unga
    1 tangawizi imenye na uiponde ponde
    3 kijiko kikubwa cha chakula tui la nzai (sio lazima)
    1 fungu la majani ya gili gilani
    1/2 kijiko kidogo cha cha mixed spice
    10 gram chumvi
    10 gram kitunguu swaumu
    3 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya mahindi
    1/2 1/2 kijiko kidogo cha cha mbegu za mustard
      1/2 kijiko kidogo cha chai dengu
      1/2 kijiko kidogo cha cha manajano (turmeric)
      3 majani mabichi ya binzali

      JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA CHINI



      1.weka katika sufuria au kikaanga mafuta ya mahindi kisha kaanga pamoja na kitunguu, kitunguu swaumu na tangawizi mpaka vilainike na kuweka harufu nzuri. Kishaongezea nyanya, chumvi, turmeric,pilipili,sunga wa mix spice, majani ya giligilani kisha kaanga kwa dakika 5 mpaka upate harufu nzuli na mchanganyiko wako ulainike na kua kahawia.
       

       
      2.Huu ni muonekano wa nyanya na vitunguu vikiendele akuiza ndani ya sufuria kisha ongezea tui la nazi.



      3.Kisha chukua unga wa manjano, majani ya binzali na dengu zilizochemshwa weka juu ya ule mchanganyiko wa nyanya kisha chemsha katika moto mdogo kwa dakika 5 kisha weka katika blenda na usage mpaka upate mchuzi mzito kabisa.




      Ni rahisi sana. Chatney hii inasaidia sana kuoneza ladha katika chakula chako na pia inaongeza sana hamu ya kula hasa kwa watu wasiopenda kula akishakula hii basi hatawea kula bila ya kua na chatney hii maana nitamua sana na inaoneza harufu nzuri na mvuto katika chakula.


      KAWAIDA UNAPOANDAA CHAKUA CHAKO SIO WALAJI WOTE WATAKUA NA HAMU YA KULA KWA KUONGEZEA CHATNEY HII MLAJI ATARUDISHA HAMUA YAKE NA ATAKULA CHAKULA CHAKUTOSHA.



      JIFUNZE KUTENGENEZA CHATNEY YA KITUNGUU

       HII NDIO CHATNEY YA KITUNGUU NI SAFI SANA NA INAONGEZA LADHA KWA CHAKULA CHOCHOTE KILE UTACHOPENDA KUITUMIA

      MAHITAJI

      120 gram dengu
      2 au 3 pili pili nyekundu kavu (dried red chillies)
      2 au 3 mbegu za pili pili manga
      2 vitunguu vikubwa cheupe au chekundu kata kata
      3 mbegu za ukwaju 
      4 majani  mabichi ya binzali (curry leaves) sio lazima
      10 gram chumvi
      2 kijiko kidogo cha chai limao
      1 kijiko kidogo cha chai unga wa kitunguu swaumu au iliyosagwa
      3 kijiko kikubwa cha mafuta ya mahindi au ya olive


      JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI



      Weka mafuta katika kikaango acha yapate moto kisha weka dengu, pili pili kavu, pili pili manga, kisha kaanga kwa dakia 2 mpka harufu nzuri ikianza kunukia.



      Kisha ongeza kitunguu maji, kitunguu swaumu, kitunguu swaumu na chumvi kisha kaanga mapak kitunguu kiwe laini. Baada ya hapo oongewa mebu za ukwaju, maji ya limao na majani mabichi ya binzali kisha kaanga kwa dakia 1 tu na zima jiko.



      Kisha weka mchanganyiko huu atika blenda na saga mpaka upate uzito kabisa na iwe imesagika yote.



      Muonekano wa uzito huo katika blenda ndio kipimo sahii cha chatney yako. inaharugu safi sana na inavutia na inaongeza hamu ya kula sana.



      HUU NI MUONEKANO SAFI KABISA BAADA YA CHATNEY YAKO KUA TAYARI KWA MLAJI KUITUMIA

      FURAHIA NA FAMILIA YAKO



      Thursday, October 21, 2010

      JIFUNZE KUPIKA WALI WA UKWAJU


      WALI HUU SI MAARUFU SANA INGAWA SIKU UKIUJARIBU UTAPENDA KUULA KILA SIKU HAHAHAHAAAAAAAA !!!!


      MAHITAJI

      Mahitaji kwajili ya mchuzi wa ukwaju unauwezo wa kukaa katika friji bila kuaharibika kwa miezi 2
       
      200 grams za ukwaju jitaidi utoe mbegu
      2 au 5  pili pili nyekundu zilizokauka
      50 grams choroko
      1 kijiko kidogo cha chai mbegu za mastad
      240 gram mafuta ya ufuta kwajili ya kupikia (sesame oil) 
      10 gram chumvi
           
        Mahitaji Kwajili ya unga 
         
        5 kijiko kikubwa cha chakula mbegu za giligilani (coriander seeds) 
        5 -10 pili pili kavu au dried red chillies (sio lazima) 

         
        Mahitaji ya wali wakati wa maandalizi
          240 gram wali uliopikwa (wali uliokwisha pikwa unapendeza zaidi hata wali uliopikwa ukalala pia unafaa)
          1 kijiko cha chai choroko
          120 gram za karanga
          120 grama za korosho
          5 majani ya binzali curry leaves 
          2 kijiko cha chai mafuta ya mawese (sesame oil)
          5 gram chumvi

            JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI





            Loweka ukwaju ndani ya maji kiasi cha 480 gram kwa muda wa nusu saa au dakika 30.




            Kumbuka ukwaju wako unatakiwa uwe hauna mbegu, kisha weka katika blenda na saga mpaka upate uzito kama uji kabisa




            Kisha chuja katika chujio ili kutoa vipande vya maganda ya ukwaju.




            Baada ya kuchuja hakikisha mchanganyiko wako ni mzito wa wastani kama ni mzito sana ongeza maji ya moto kiasi na kisha rudisha katika blenda saga na toa tena chuja na upate mchanganyiko mzito wa wastani na usiwe mwepesi sana.




            Hizi ndio mbegu za giligilani zikaushe katika kikaango tayari kwa kusaga



            Kisha ziweke katika blenda kwajili ya kusaga.




            Baaada ya kusaga na ukapata unga safi kabisa weka pembeni katika chombe kwajili yamatumizi ya wali kumbuka ukizidisha unga huu utaleta ladha ya uchungu katika wali wako.
             



            Sasa tunatengeneza mchuzi mzito. chukua kikaango weka mafuta yakishapata moto weka pili pili kavu nyekundu, mbegu za mastad na dengu au choroko



            Kisha weka ule mchuzi wa ukwaju au ( sauce!)




            Sasa tunaanza kupika pole pole. weka moto mdogo na pika kwa muda mrefu kiasi. kisha harufu ya ubichi ya ukwaju itapotea, maji yatakauka na ukwaju utakua umejipika na mafuta yatakuja juu. ngezea kijiko kimoja kidogo cha chai unga wa mbegu za giligilani kuongeza harufu safi na ladha ya kuvutia.




            Kisha toa katika moto, mchanganyiko huo wa ukwaju hifadhi katika chombo na iache ipoe. Ikipoa safi inakua tayari kwa matumizi ya wali.

            KUMBUKA
            TKiaasi cha uzito wa mchuzi wako wa ukwaju ndio ubora zaidi pia kumbuka mafuta yakiwa mengi kiasi yanasaidia kuihifadhi kwa muda mrefu, ikiwa na mafuta kiasi itaharibika mapema maana mafuta yakiwa yanaelea kwa juu yanazuia wadudu kupenya na kuozesha mchuzi wa ukwaju .
            Sasa hapa ndio tunapika wali wenyewe, 1 kijiko kidogo cha chai mafuta ya kupikia, weka dengu, kama mpenzi wa pili pili weka pamoja na majani ya binzali, kisha ongeza karanga na korosho.




            Kisha ongezea kijiko kimoja cha mafuta ya ufuta, mchuzi wa ukwaju  2 kijiko kikubwa cha chakula pamoja na chumvi, Kisha weka wali na koroga mpaka vichanganyike safi kabisa . Kisha mpatie mlaji chakula kikiwa cha moto.



            Huu ni muonekano safi wa wali huu ukiwa tayari umeshaiva na tayari kwa mlaji kufurahia




            Viungo ni viingi lakini sio kazi kuandaa chakula hiki na familia yako ikafurahia utamau wa wali huu

            ENJOY WITH YOUR FAMILY


            

            UBUNIFU WA KUPIKA WALI WA NAZI


             RECIPE SAFI KABISA YA WALI HUU MAARUFU MIJI YA PWANI YA BAHARI YA HINDI


            MAHITAJI

              480 gram nazi iliyokunwa
            240 grama za mchele ( Basmati), loweka katika maji kwa dakika 20. Au wali uliokwisha pikwa ukaiva ila uwe umechambuka pia nao unafaa.
            2 kijiko kikubwa cha chakula dengu au choroko loweka katika maji kwa dakika 10
            1 au 2 pili pili mbuzi kuongeza ladha lakini sio lazima
            1 kijiko cha chakula ( mbegu za mastad) mustard seeds
            5 majani fresh ya binzali (curry leaves)
            100 gram za korosho au karanga ziwe zimekaangwa
            5 grama chumvi
            2 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia



            JINSI YA KUANDAA FATILIA MAELEZO NA PICHA HAPO CHINI




            Kabla hatujaanza kupika tunatakiwa kukuna nazi, unatakiwa kuvunja nazi zako ziwe katika vipande viwili kama inavyoonekana katika picha.



            Hii ndio mashine ya kukunia nazi ukienda katika duka la kuuzia vyombo utapata tu kwa be  nafuu inatumia umeme na inarahisisha kazi.




            Unatakiwa uwashe kwanza mashine kisha ndio uchukue kipande kimoja cha nazi na uweke kwenye mashine ili ianze kukwaruza na kupata machicha na muonekano katika picha ndio njia sahihi ya kukuna nazi kwa mashine.



            Unaona jinsi kikwaruzo cha nazi kinavyozunguka kwa kasi katika picha jitaidi usiongee na simu au kupiga stori ukajisahau mashine hii ni kali sana itakutoboa vidole jitaidi kuna nazi yako haraka kisha endelea na mambo yako.





            hapa umeshamaliza kukuna nazi yako saafi kabisa na umepata machicha ya kutosha kwajili ya wali wako. Machicha haya ni matamu sana sana ukila mabichi.




            Weka vijiko 2 vya mafuta kula katika sufuria, weka mbegu za mastard zikianza tu kupasuka, ongeza dengu, pili pili mbuzi, korosho , majani ya binzali (curry leaves) . Kisha endelea kukaanga kwa dakika 2.



            Baada ya dengu kua za kahawia na korosho kukaangika, Kisha ongeza machicha ya nazi na kaanga kwa dakika 5 hadi 10 au mapka machicha ya nazi yaange kugeuka rangi na kua kama kahawia.



            Sasa weka wali wako uliokua umelowekwa kwa dakika 20.



            Hakikisha unakoroga vizuri mpaka wote uchanganyike vizuri kwa dakika 10 tayari utakua umeiva hakikisha unakoroga tu ili wali wako usiungue na kushika chini. Wali huu haupikwi na maji maana uliloweka mchele kwa dakika 20 kwahiyo unakua umemeza maji pia kumbuka unaweza tumia wali uliokwisha iva.



             Muonekano wa wali wako ukiwa tayari umeisha iva tayari kwa mlaji kufaidi!




            Inapendeza sana kua mbunifu kifuu kile kile cha nzai ulicho kuna unaweza kukitumia kama bakuli ya kupakulaia wali wako na ikapendeza sana.




            (Samahani wapenzi wa blog sikuahinisha Mchele uliotumika hapa ni aina ya basmati, kawaida mchele huu ukilowekwa katika maji kwa dakika 20 na ukaukaanga kwa dakika 10 unakua umeiva kabisa tayari kwa chakula jumla ya muda wako wa maandalizi inakua dakika 30 na zinatosha bakisa kuivisha wali wako. Endapo utatumia aina nyinge ya mchele bora tumia ulioisha iva ili usikosee recipe ukala wali mbichi)

            MUONEKANO WA KUMUHUDIMIA MLAJI NDANI YA KIFUU CHA NAZI NI KIVUTIO CHA KIPEKEE SANA. WALI HUU UNAPIKWA KWA MUDA MFUPI SANA HAUPOTEZI MUDA WAKO NA LADHA YAKE NI OOHHHH YAMY YAMY!!!!