BISCUIT HIZI NI TAMU SANA NA RAHISI KUTENTENEZA KWA YEYOTE ATKAEZIONJA BASI ITAKUA NDIO BITE YA KILA SIKU
MAHITAJI
MAHITAJI
240 gram unga wa ngano
1 kijiko kikubwa cha chakula sukari
2 kijiko kikubwa cha chakula maji safi
2 kijiko kikubwa cha chakula Mafuta ya samli (kama hutumii basi weka mafuta ya mahindi)
Chumvi nusu kijiko kidogo cha chai
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA CHINI NA MAELEZO YAKE
Changanya vitu vyote kwa wakati mmoja katika bakuli
Kisha weka maji safi na anza kukanda mchanganyiko wako mpaka uwe mgumu kama utakua laini ongeza unga kidogo.
Mchanganyiko wako unatakiwa uwe na uwiano sawa usinate sana na usiwe laini sana.
Mwaga unga juu ya meza, KIsha sukuma unga wako uwe flat kabisa – Isiwe nyembemba sana na isiwe pana sana iwe wastani tu. Kwa kutumia kisu kata mistari safi iliyonyooka.
Kisha kata tena kwa upande wa pili ili upate maumbo ya pembe nne . Hii ni pendekezo tu sio lazima unaweza tumia kifaa malumu cha kukatia biscuti na ukatengeneza maumbo yeyote unatotaka.
KIsha tumbukiza vipande hivyo ndani ya mafuta yamoto na ukaange mpaka upate rangi ya kahawia (brown) . Mafuta yataacha kutoa mapovu baada ya biscuti zako kuiva kisha zitoe.
Toa kwa kutumia kijiko kikubwa chenye matundu ili mafuta yabaki katika kikaango chao na biscuti zitoke kavua.
Acha zipoe kwa muda kisha ruksa unaweza kula. Ukisha kula mara moja basi unanogewa utataka kula kila siku. Zihifadhi katika chombo utakachoweza kufunika na hewa isiingie. Unaweza kuzihifadhi kwa mwezi mzima lakini nakuhakikishia ukishaanza kuzila hazitafika hata uo mwezi utazimaliza maana ni tamua sana na hazikinai.
FURAHIA
No comments:
Post a Comment
Tunaheshimu sana maoni yako