Saturday, October 2, 2010

JIFUNZE KUTENGENZA MKATE MWEUPE RAHISI

KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA MKATE HUU KWAJILI YA KITAFUNWA CHA CHAI NYUMBANI AU KWAJILI YA KULA NA SUPU

MAHITAJI
720 gram Unga wa ngano 

 2 na 1/4 kijiko kidogo cha chai amira ya chenga
60 gram maji ya uvugu vugu
240gram maziwa ya maji
1 yai bichi piga lilainike 
3 kijiko kikubwa cha chakula siagi
2 kijiko kikubwa cha chakula sukari 
3/4 chumvi kijiko kidogo cha chai

 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI



Pasha maziwa ya maji yawe na uvugu vugu kisha weka siagi na iyeyuke ndani ya maziwa kisha weka pembeni. Kisha chukua yale maji ya uvugu vugu na uchanganye amira ya chenga, sukari na chumvi Kisha ikorogr na weka pembeni ili mchanganyiko wako uyeyuke.





Kisha chukua mchanganyiko wa maziwa na ule mchanganyiko wa hiriki na uchanganye. Kisha chukua unga wa nganoa na changanya pole pole kwenye mchanganiko wa maziwa weka unga kidogo kidogo mpaka uchanganyike vizuri.



Kawaida mchanganyiko wako utakua una nata nata usiongeze unga mpaka iwe lazima hasa. Endelea kukanda unga wako pole pole na mchanganyiko utakaa sana na kua mgumu maji maji yatapungua wakati unakanda. Kisha nyunyizia unga katika ubao au meza unayoandalia unga wa mkate wako. Kazana kukanda kwa kutumia nguvu mpaka mchanganyiko wako wote uchanganyike vizuri wote. Jitaidi kukanda kwa kutumia dakika 8 hadi 15 kama hutumiii maashine.




Baada ya mchanganyiko wako kukamilika huu ndio muonekano mkavu na mgumu tayari kwa kukata na kuchoma.




 
Kisha chukua bakuli safi na ulipake mafuta baada ya hapo weka mchanganyiko wako wa unga unaweza kufunika kwa kutumia taulo au foil ya plastic.




Hakikisha umeweka sehemu yenye joto la kutosha ili iumuke na iwe mara mbili kama inavyoonekana kwenye picha.





Kisha chukua mchanganyiko na uuuweke juu ya meza sukuma upate umbo la mstatiri.




 
Tumia kisu na kata vipande 12 vilivyo sawa.




Kisha nyonga kila kipande kiwe katika umbo la duara. Kisha weka maumbo hayo ya duara katika tray na uache upana wa inch 2 kila upande hakikisha haishikani. Kisha weka pembeni tena katika joto la chumba acha yaumuke tena. Usijale kama miduara yako haina maumbo mazuri haina neno.





Si unaona sasa yakishaumuka yanajipendezesha yenyewe safi kabisa. Yakisha umuka yanashikana na kutengeneza umbo zuri.




 
Kisha choma katika oven iliyokwisha pashwa joto la 350F choma katika oven  kwa daika 20-30 mpaka upate rangi znuri ya kahawia.




Mkate wako ukishaiva weka pembeni upoe kabla ya kumpatia mlaji.




Furahia mkate huu kwa kunywa na supu mchan au usiku pia kwa Jam na siagi siku inayofuata wakati wa chai ya asubuhi! Unaweza kutunza katika freezer kwa wiki 1 tu baada ya hapo ubora unapotea!


Inapendeza sana ukitengeneisha na kumpatia mlaji mkate mmoja mmoja.


2 comments:

  1. kweli mchele mmoja mapishi mengi, hiyo style yako nimeipenda inaelekea huu mkate ni mtamu sana

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako