RECIPE HII NI RAHISI SANA KUANDAA HAICHUKUI MUDA WALA HAITAJI UBUNIFU MKUBWA KWAHIYO SIO KWAJI YA WATU WENYE MATATIZO YA KULA MAYAI MTU YEYOTE ANAWEZA KULA NA UKAIPENDA SANA KEKI HII.
MAHITAJI
240 gram unga wa ngano
200 gms maziwa ya maji
60 gram siagi iliyoyeyushwa
1 na nusu kijiko kidogo cha hai baking powder
1/2 kijikokidogo cha chai baking soda (soda bi-carb)
1 kijiko kidogo cha chai vanilla essence
75 gram maji barid safi na salama
JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO HAPO CHINI
Iwashe oven kwa moto wa 400F (200C). Kisha changanya unga wa ngano pamoja na Baking powder na bicarbonet Soda pamoja katika chujio kisha chekecha kama unawasi wasi na ubora wa unga wako kama unauhakika basi changanya moja kwa moja katika bakuli.
Katika bakuli jingine safia chanyanga, siagi iliyoyeyushwa, vanilla essence pamoja na maji. Koroga vizuri hakikisha imechanganyika vizuri sana.
KIsha chukua mchanganyiko wako wa maziwa changanya kwenye mchanganyikowa unga na changanya pole pole. (Usitumie nguvu kabisa hapa tafadhali utaharibu!) Mchanganyiko wako unatakiwa uwe mzito na unamiminika kwa uzito sana. Kisha mimi na katika chombo chako cha kuokea ambacho umekipaka mafuta ya siagi ili keki yako isiungue.
Itoe katika Oven. Acha ikae katika katika chombo ulichookea kwa dakika 5 kisha ipindue upande wa chini uwe juu itoe katika chombo ulichookea na iweke katika sahani.
Keki saa ipo tayari. Haikua rahisi sana? Huu ni ujanja mwingine wa kuipamba zaidi keki yako. Chukua sukari ya unga changanya na cocoa kidogo kisha nyunyizia juu ya keki yako na mpatie mlaji afurahie (Mhhhhh jamani vanilla cake bila ya chocolate?
Ukiikata kwa ndani huu ndio muonekano wake ni sponge safi kabisa
SIO KAZI KUIPIKA JITAIDI FAMILIA YAKO IFURAHIE
No comments:
Post a Comment
Tunaheshimu sana maoni yako