Sunday, November 7, 2010

JIFUNZE KUTENGENEZA CHAKULA HIKI MCHANGANYIKO WA NJEGERE NA VIAZI MABATATA

MCHANGANYIKO HUU WA VIAZI MBATATA NA NJEGERE NI SAFI SANA KWA LADHA NA AFYA YA MLAJI PIA CHAKULA HIKI NI KIZITO NA KINA KAA SANA TUMBONI NA NI RAHISI KUANDAA.

MAHITAJI

1 Kitunguu maji kikubwa katakata
2 nyanya kubwa, chop chop
2 Kiazi mviringo au mbatata (Unaweza kumenya ua ukaosha vizuri na ukakata kata kikiwa na maganda yote sawa maganda yana saidia kupoata harufu na ladha halisi ya kiazi)
240 gram za njegere
5 gram za kitunguu swaumu
5 grama za tangawizi ya kusaga
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa mdalasini
2 pili pili mbichi
1/2 kijiko kidogo cha chi unga wa binzali (turmeric powder)
1/2 kijiko kidogo cha chai cumin powder
10 gram chumvi
1 fungu dogo la majani ya gili gilani kwa kupambia na kuleta ladha safi.
2 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia au siagi au samli.



JINSI YA KUANDAA FATILIA MAELEZO NA PICHA HAPO CHINI



Weka mafuta katika kikaango kisha weka vitunguu. Kaanga kwa dakika 1 , Kisha weka kitunguu swaumu na tangawizi ya kusagwa  , Pili pili (Kama unatumia sio lazima) endelea kukaanga mpaka vitunguu vilainike na kuiva.


KIsha weka viungo vyoote na kaanga kwa dakika 2 hadi3 viuobgo viive na kuondoa ukali utakaosababisha kiungulia kama havitaiva vizuri.



Kisha weka viazi vyako na kaanga kwa dakia 3mara nyingi mimi huwa sipendi kutoa ngozi ya kiazi ili kuoata ladha halisi ya kiazi.



Kisha weka nyanya, Kaanga kwa dakika moja na kisha weka 240 gram za maji safi sana salama funika na mfuniko acha ichemke kwa dakika 5.


Kisha weka njegere na pika mpaka maji yakauke na viazi vilainike na kuiva kabisa.


Kama unavyoona katika picha chakula chao kimeiva na mchuzi umekauka kabisa viazi na njegere zimeiva kabisa mwisho kata kata corrienda na pamba kwa juu.


Huu ndio muonekano halisi wa chakula chako na unaweza kula na ugali, chapati au wali na familia au mlaji yeyote yule akafurahia sana sana.



1 comment:

  1. kwa kweli asante sana sana kwa mapishi,mimi ni mdau mkubwa wa mambo haya,kupika kuko kwenye damu kabisa napenda kujifunza na napenda kupika kupita kitu chochote,yaani ndio hasa hobbie yangu,nafurahia mapishi na nitaendelea kujifunza kupitia kwako mapishi mbalimbali.Shukrani sana.Mama Isack wa kiseke mwanza.

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako