Sunday, November 7, 2010

JIFUNZE KUTENGENEZA SUPU YA KAROTI


 RECPE SAFI KABISA NA UMUHIMU WA CAROTI KATIKA MWILI WAKO

 Kwanza kabisa ina rangi safi sana ya chungwa, yenye mvuto kwa mlaji, pia utamu wa carrot unakwenda sambamba na mchanganyiko wa viazi ulaya, celery na saffron. Umuhimu ni  virutubisho ndani ya mwili, Inaongeza hamu ya kula, ubora wa macho kuona vizuri na afya ya mwili kwa ujumla – Huu ndio ubora wake supu ya caroti tutayojifunza jinsi ya kuiandaa.

MAHITAJI

2 kubwa carroti, katkata vipande (ikwangue tu na uioshe vizuri usiimenye karoti)
1 kiazi kikubwa, katakat vipande (osha vizuri acha kiwe na ngozi yake)
1 jani la celery, (katkata na majni yake yote usitupe)
120 maziwa ya maji
1 kitunguu kikubwa, katakta vipande
5 gram kitunguu swaumu cha kusagwa
3 gram saffron
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
Majani ya corienda kwajili ya kupambia supu


JINSI YA KUAANDAA FATILIA PICHA NA MAELEKEZO HAPO CHINI



Chemsha kwa mmvuke ( Steam) carrots na viazi ulaya kwa dakika 4 . Mboha hizi hazitakiwi ziive zipondeke zinatakiwa ziive wastani tu kiasi uweze kusaga katika blenda.



Chukua maziwa ya uvugu vugu kisha weka saffron ( Zafarani). Weka pembeni katika bakuli. Maziwa yanasaidia kuongeza protein katika supu yetu.


Weka kijiko kimoja katika sufuria yako yapate moto kisha weka  kitunguu maji, kitunguu swaumu,chop celery na chumvi.




Kaanga mpaka ilainike kwa dakika 2.




Chukau mchanganyiko wote na uhamishie katika blenda tayari kwa kusaga, ongezea na zile mboga ulizochemsha kwa mvuke (steamed vegetables).



Saga vizuri katika blenda.



Baada ya kusaga safi kabisa rudisha katika sufuria, acha ichemke tena kwa dakika 2 – Kisha punguza moto ichemke kwa dakika 3 wakati huo huo unatakiwa umimine maziwa yale uliyochanganya na saffron.


 
Hakikisha unakoroga vizuri maziwa na mchanganyiko wako wa supu vichangayike safi kabisawakati supu yako bado ikiwa jikoni.



Huu ni muonekano wa supu safi kabisa ikiwa imeshaiva pamba kwa juu na janai la giligilani ( coriender) kwa harufu safi na ladha safi




Hakikisha unampatia mlaji supu ya moto. Ni supu safi kwa afya ya mlaji, tamu sana na ni nzito. Kama unaona ni nzito sana kwako basi ongeza maji kiasi au maziwa mpaka ufikie uzito unaopenda wewe. unaweza pia mwagia pili pili manga kwa juu na ukafurahia!

1 comment:

  1. asante kwa recipe nzuri ya supu, yafaa sana hasa kipindi hiki cha baridi.

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako