Friday, November 19, 2010

JIFUNZE KUTENGENEZA MKATE AINA YA NAAN


WATU WENGI MMEKUA MKIULA MKATE HUU KATIKA RESTAURANT ZA KIHINDI NA UKIMUOMBA AKUFUNDISHE HAWEZI KUKUBALI MAANA HUTAKWENDA TENA KUNUNUA KWAKE LEO NAKUFUNDISHA RECIPE SAFI KABISA YA MKATE HUU MTAMU SANA KWAJILI YA KULIA MBOGA ZA NYAMA AU MBOGA MAJANI.

MAHITAJI

720 gram unga wa ngano
1 kijiko kidogo cha chai amira ya chenga (Active dry yeast)
180 gram ya maji ya uvugu vugu
5 gram chumvi
1/2 kijiko kidogo cha chai sukari
1 fungu la majani ya gili gilani ( Corriender chopped)
1-1/2 siagi kijiko kikubwa cha chakula (butter)

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA  NA MAELEZO HAPO CHINI



Changanya katika bakuli amira ya chenga, maji ya uvugu vugu na sukari kisha koroga hakikisha mpaka amira inayeyuka kabisa kisha weka pemebeni kwa dakika 5


Kisha weka unga wa ngano, chumvi, majani ya gili gilani kisha changanya vizuri.


Tengeneza shimo kati kati kisha mwagia yale maji yenye mchanganyiko wa amira na uanze kukandaKanda vizuri unga wako na hakikisha umeshikana safi na ni laini.


.Baada ya kukanda safi kabisa hakikisha bakuli lako unafunika na taulo maalumu ya jikoni au nailoni kisha weka sehemu yenye joto la kutosha na acha iumuke mpaka ije katika bakuli lako kwa muda wa masaa2 au 3 tu. Hii inategemea na upo nchi gani na majira gani ya hewa.


Baada ya hapo toa mchanganyiko wako wa unga anza kuukanda tena kwa dakika 5 tu kisha gawanisha katika maumbo madogo.



Mwagia unga kidogo juu ya meza kusaidia isishike na anza kusukuma kwa kutumia mpini iwe wa mbao au wa chuma.


Hakikisha unaposukuma usitengeneze umbo la mduara tengeneza umbo la urefu. Kisha washa oven yako kwa moto wa kati ( Njia hii unatumia kama huna jiko la Tandoor) kisha chukua mkate wako wa Naan weka katika (baking sheet) chombo cha kuokea, paka juu ya mkate naan siagi kiasi na kisha weka katika oven. Ukisahona tu unaanza kubadilika rangi toa geuza na paka tena siagi upande wa pili.


Ukiona muonekano huu basi ujue upande wa chini tayari umeiva hapa ndio unatakiwa sasa kugeuza na kupaka siagi upande wa pili kisah rudisha katika oven.



Huu ni muonekano wa upande wa kwanza ulivyoiva hakikisha unapaka siagi safi kabisa ya kutosha na jina halisi la kate huu ni butter Naan kwakua unapata ladha safi toka katika siagi.



BAADA YA KUPIKA PANDE ZOTE MBILI NA UKAPATA RANGI SAFI KABISA YA KAHAWIA BILA KUUNGUZA MAKATE WAKO HAKIKISHA UNAMPATIA MALAJI HARAKA BADO UKIWA WAMOTO ATAFURAHIA SANA NA UNAWEZA KULA NA MCHUZI AU SUPU AU MBOGA YEYOTE ILE IWE YA MAJANI AU NYAMA.

FURAHIA NA FAMILIA YAKO.



7 comments:

  1. Asante chef mie nasubiri hiyo recipe kwa hamu

    ReplyDelete
  2. hi, nimeona picha za naan, lakini mbona maelezo za ingredients na method hamna?

    ReplyDelete
  3. Shukrani kwa picha nzuri lakini mi naona kuna jambo muhimu unasahau au mi sijaelewa jinsi ya kuperuzi mtandao wako.
    Picha huwa unatuwekea hatua kwa hatua lakini sijaona ukitoa recipe and njia ya kupika mapishi unayoonyesha. Macho hayawezi kutambua kila recipe, mi huwa naishia kuangalia tuu.

    ReplyDelete
  4. duh...yaani fanya fastaaa chef Issa UNIPE HII KITU ,maana mie nina kazi ya kwenda kula kwa wahindi ....hebu nipe shule nami niwe nazipika tu kwangu ....

    mama iqra

    ReplyDelete
  5. shukran chef issa,pls jinsi ya kuandaa pls

    mama taqqiyyah

    ReplyDelete
  6. KAKA UPO JUU, HII SIMPLE BUT SEEMS TAMU SANA.
    BE BLESSED

    ReplyDelete
  7. asante chef kwa hii naan,mungu akujaze imani inshallah

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako