Sunday, December 5, 2010

JIFUNZE KUTENGENEZA PIZZA KAUKAU YENYE CHIIZI JUU NA PEMBENI


PIZA HII NI TAMU SANA NA NIRAHISI KUTENGENEZA KAA TAYARI KWA RECIPE

MAHITAJI

KWAJILI YA UNGA WA KUKANDIA
    Utaweza tengeneza 6 pizza  ( 23-30 upana wa cm ) 
1 kilo ya unga wa ngano 
1 kijiko kikubwa cha chakula chumvi
1 kijiko kidogo cha chai amira ya chenga
60 gram Olive oil au vegetable oil
420 gram maji baridi sana (40° F/4.5° C)
1 kijiko kikubwa cha chakula sukari


KWAJILI YA KUWEKA JUU YA PIZZA

600 gram sauce iliyopikwa kwa nyanya
1 kilo Mozarella cheese ( nusu kata slice na nusu kata umbo la mstatiri kama katika picha)
200 gram slice za nyanya fresh iliyoiva
1 fungu la majani ya basil


JINSI YA KUANDAA FATA MAELEKEZO NA PICHA HAPO CHINI



Katika bakuli weka unga wa ngano, humvi pamoja na amira au kama unatumia mashine basi weka katika mashine.



Kisha weka mafuta ya olive, sukari na maji baridi kisha kanda vizuri. kama unatumia mashine weka speed ndogo. 
 

Kanda kwa kutumia nguvu kiasi baada ya maji kushi unga vizuri ili upate mchanganyiko safi.




Kisha toa mchanganyiko huo wa unga na uweke juu ya meza kanda kwa dakika 5 mpaka 7, mpaka uhakikishe mchanganyiko wako umekua laini kabisa. kama bado limekua tepe tepe, ongeza unga kiasi na uendelee kukanda au kama kavu sana ongeza kijiko 1 au 2 vya maji baridi.



Kama unatumia kukandia mashine kama kwa muda huo huo nilioelekeza ila kwa speed ndogo. Mwaga unga juu ya mea unayokandia. Kisha kata unga wako katika vipande sawa 6 vyenye uzito sawa.  Mi nimekata katika vipande 4 kwakua nilikua nataka pizza kubwa.



Mwagia unga kiasi juu ya mchanganyiko wakow a unga. Hakikisha mikono yano ni mikavu kisha ipake pia unga. Kisha chukua vipande hivyo vya unga na viringisha katika maumbo ya duara.



 Kisha chukua hayo maumbo ya duara na weka katika sinia ulilolipaka mafuta weka na paka mafuta juu ya hiyo miviringi pia.



Kisha chukua plastic foil na funika kwa juu.  Kisha weka mchanganyiko wakow a unga katika friji acha ulale usiku kucha pia kama unataka kula pole pole unaweza hifadhi kwa siku 15 mpaka 30 katika freezer sio friji. kisha ukawa unapika pizza moja moja kila siku na kama umeziweka katika freezer kumbuka siku moja kabla ya kuipika pizza yako toa katika freezer na weka katika friji ili iyeyuke. Kama unataka kupika siku hiyo hiyo basi acha katika friji kwa masaa 3 mapka 4 kisha toa.




Siku ya 2 - siku uliyopanga sasa kula pizza, masaa 2 kabla ya kupika viza yako, Toa idadi ya miviringo ya pizza unazotaka kupika wewe. Kwanza unamwagia unga kisaha unapaka mafuta kiasi kisha weka juu ya meza kwajili ya kukanda tena. Kanda kwa dakika 2 kisha funika na plastic wrap Acha kwa masaa 2 nje.



Kisha chukua maumbo hayo ya mviringo na anza kusukuma upate umbo bapa maalumu kwajili ya pizza.



Kwakutumia rolling pin ( ubao wa kusukumia) zungusha pizza yako katika mpini na uibebe



Kisha weka katika pizza pan ambayo imemwagiwa unga na imemwagiw amafuta kiasi (Hii inasaidia pizza isigandie tyra ya kuchomea)
 


Kisha kwa kutumia mikono yako vuta mpaka ifike mwisho wa sahani



Hakikishs baada ya kuivuta mwisho wa sahani iwe na muonekano kama wa kwenye picha



Hakikisha unaweka chizi iliyo na umbo la mstatiri na uache nafasi kama ionekanavyo katika picha. .



Kisha kusanya mchanganyiko wako tokea nje na unaingiza ndani kwa kufunika cheese yote na ukandamize ili ishike. Hakikisha unakandamiza vizuri. Weka mtindo wa curl kama nilivyofanya mimi, Fanya hivyo kuzunguka pizza yote.



Chumua mchuzi wa nyanya ( tomato sauce) kisha pakaza pizza yako yote kwa juu.


 
Rushi majani ya basil juu ya sauce ya nyanya. Kisha weka slice za nyanya fresh, ziwe nyembamba. Kisha weka slice za fresh mozzarella cheese juu kabisa iwe mwisho.



Choma katika oven iliyokwisha washwa na inamoto wa 450-500F. Choma kwa dakika 15 mpaka 20 inategemea na uwezo wa oven yako. Kwa moto makali sana inaweza chukua hata dakika 10 tu. Hakikisha ikiwa katika oven unaichungulia.



Ikishaiva toa na rushia tena majani ya basil kwa juu. Joto kali toka katikapiza litaunguza majani hayo na kutoa harufu safi sana.
 


Kata katika vipande vidogo inakua rahisi kwa mlaji.



Hakikisha unampatia mlaji ikiwa yamoto. Unaweza rushia kwajuu Parmesan cheese ana pili pili manga kama unapendelea.




HUU NDIO MUONEKANO WA PIZZA YETU SAFI SANA UNAWEZA KUIONGEZEA LADHA KWA KUWEKA CHOCHOTE KILE UKIPENDACHO KAMA NYAMA AINA ZOTE NA UKAFURAHIA NA FAMILIA YAKO.



4 comments:

  1. Maelekezo chini ya wapi? mbona hatuoni hayo maelekezo..tunaona picha tu..au mi pekeyangu ndo siyaoni wenzangu wanayaona hayo maelekezi ya upishi?

    ReplyDelete
  2. maelezo plizzz, I would real like kulipika pishi hili...

    ReplyDelete
  3. Kaka Issa nashukuru kwa kulete pishi hili.Nakumbuka niliwahi kukuandikia kuomba utuwekee namna ya kuandaa pizza lakini hapo hujaweka melekezo( kwa maneno) Pia ningependa kujua tunaweza kutumia microwave oven za kawaida ama mpaka tuwe na zile Oven kubwa?
    Emmy

    ReplyDelete
  4. Maelezo kaka yangu hayaonekani. basi nimebaki kumeza mate na picha. hata ya tambi hakuna. Pliizz tuwekee

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako