Thursday, December 23, 2010

NAWATAKIA KHERI YA SIKUKUU ZA KUFUNGA MWAKA PIA KHERI YA MWAKA MPYA 2011


JIFUNZE JINSI YA KUPAMBA KEKI HATUA KWA HATUA, FATILIA MPAKA MWISHO WAKE UONE ITAKAMILIKA NA KUPENDEZA VIPI.















Hapa natumia chocolate nyeupe kuandika katika chocolate block ya kilo 2 yote hii ni ubunifu na ilipendeza sana sana.











Keki ikiwa imekamilika imepambwa kwa matunda na chocolate nyeupe na nyeusi pia keki hii imekaa mfano wa mlima kilimanjaro na theruji yake inayopendeza sana.


Muonekano safi wa keki  yenye mfano wa mlima kilimanjaro kwajili ya kuwatakia kheri ya sikukuu ya noeli na mwaka mpya hapo kwenye muonekano wa maneno ni chocolate bloc ya kilo mbili na chocolate trifle kama mapambo hapo mbele staff wenzangu walikula na walifurahia sana sana.


 

Sunday, December 19, 2010

JIFUNZE KUPIKA PILAU SAFI NA RAHISI WAKATI HUU WA SIKUU


RECIPE SAFI KABISAYA PILAU KWA MSIMU HUU WA SIKU KUU ZA KUFUNGA MWAKA. UNAWEZA PIKA KWA KUTUMIA MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI TU AU UKAPIKA KWA AINA YEYOTE YA NYAMA KWA KUTUMIA MTINDO HUU HUU NA IKAPENDEZA SANA SANA.

MAHITAJI

  240 gram za mchele wa basmati au mchele wowote mrefu, Loweka katika maji kwa dakika 20
  1 kijiko kidogo cha chai mbegu za binzali nyembamba ( cumin seed)
   1 kitunguu kikubwa kata kata
  1 Nyanya kubwa kata kata
   3  spring onions ( majani ya kitunguu) 

  1 bay leaf
   3 cloves ( Mbegu za Karafuu )

3 cardamom ( mbegu za hiriki)
  1/2 kijiko cha chai kidogo turmeric powder ( Unga wa manjano)
   5 gram kitunguu swaumu
  1 pili pili mbuzi kata kata
    5 gram unga wa tangawizi au ya kusagwa
    1 kijiko kidogo cha chai garam masala
   600 gram coconut milk (Tui la nazi) sio lazima kama hutumii nazi basi weka maji kawaida
   5 gram chumvi
    1 fungu la giligilani kwajili ya kupambia
  1 jikiko kidogocha chai maji ya limao (sio lazima)




JINSI YA KUANDAA FATILIA HAPO CHINI



  Katika sufuria weka kijiko 1 kikubwa cha chakula mafuta kisha kaanga mbegu za binzali nyembemba, bay leaf, karafuu, mbegu za hiriki, kitunguu swaumu, pili pili mbuzi, tangawizi na chumvi.




 Kitunguu kikashalainika weka nyanya pamoja na unga wa manjano na  garam masala. Kaanga kwa dakika 2.










Pilau hii nimepika sio ya nyama, kwa wale wapenzi wa nyama wakati umeweka vitungu na vile viungo vyote weka pamoja na nyama kaanag vyote kwa pamoja kwa dakika 10 kisha ndio uweke nyanya na viungo vingine vinavyofatia.


Nyama yako ili iwe laini chukua papai lililoiva baada ya kukatakata nyama pondea papai katika bakuli lenye nyama kisha weka chumvi kidogo, soya sauce kidogo, kitunguu swaumu na tangawizi kwa ladha zaidi. Nyama hii iweke kwenye friji kwa dakika 45 tu iwe ndani katika mchanganyiko huu itakua laini sana na utaipika kwa muda mfupi sana na familia watafurahia.








   Kisha ongeza mchele hakikisha unauweka bila maji. Hakikisha una ugeuza geuza mpaka mchele ubadilike rangi na kutoa harufu safi baada ya kuukaanga.





 Kisha ongeza tui la nzai au maji kwa wale wasio tumia nazi endelea kukoroga ichanganyik vizuri.











 Funika na mfuniko kisha pika kwa dakika 10 au mpaka mchele wako utakapo iva na kua wali.






Kisha ugeuze wa chini uje juu na wajuu uende chini. Binafsi huwa napenda kuongezea njegere zilizochemshwa nikahifadhi katika friji mwisho kabisa pilau hii ikishaiva. 
 
 

Kwa kuipendezesha pilau yako sasa mwagia kwa juu majani ya kitungu na majani ya giligilani.  Kisha huwa na mwagia kwa juu maji ya limao kwa sababu kuu mbili. Moja ni kuongeza ladha. Pili inasaidia kupunguza kiwango cha sodium.


Hakikisha unampitia mlaji chakula kikiwa chamoto. Kwa wale wapenda samli unaweza weka kijiko kimoja pia itaongeza harufu na ladha safi katika pilau yako.




HUU NI MUONEKANO SAFI BAADA YA PILAU YETU KUIVA FURAHIA NA FAMILIA YAKO KWA MAPISHI SAAFI NA RAHISI KUANDAA KUMBUKA LIMAO AU PILI PILI SI LAZIMA KUWEKA NI PENDEKEZO LAKO TU HASA KAMA UNAMATATIZO USIWEKE TUMIA VIUNGO VINGINE NA BADO PILAU YAKO ITAPENDEZA SANA.



HABARI YA SIKU NYINGI WAPENZI WOTE WA CULINARY CHAMBER BLOG


SAMAHANI SANA WAPENZI WOTE WA BLOG KWA KUTOKUA NA MAWASILIANAO YEYOTE KATIKA BLOG KWA WIKI MBILI SASA.

HAPA NILIPO KWASASA NI KIJIJINI INTERNET ILINISUMBUA SANA NASHUKURU SASA IPO SAFI NA NITAENDELEA KUTOA MAFUNZA KAMA KAWAIDA. KAENI TAYARI KUPATA RECIPE NYINGI NA NZURI HASA WAKATI HUU WA SIKUKUU YA KUFUNGA MWAKA.

MOLA AJALIAPO SALAMA NITAKUA DAR ES SALAAM TAR 1/1/2010 MCHANA NA NITAONDOKA DAR ES SALAAM TAR 4/1/2011 KWA WALE WOTE WATAKAO KUA NA MASWALI KUHUSU CHAKULA TUNAWEZA KUWASILIANA KWA SIMU NAMBA NITAIWEKA TAR 28/12/2010.

"SURPRISE SURPRISE"

NAOMBA MBASHIRI NI TUKIO GANI MUHIMU LITAJIRI HAPA KATIKA BLOG HII KATIKA SIKU 10 ZINAZOKUJA? ZAWADI SAFI SANA ATAPATIWA MSHINDI WA KWANZA KUBASHIRI. TUMA MAONI HAPA HAPA KATIKA BLOG ILI WATU WOTE WAONE ISIJE KUA LAWAMA NIMEMPENDELEA MTU NA ANDIKA JINA LAKO BAADA YA KUTOA JIBU SAHIHI MPAKA SASA MSHINDI HAJAPATIKANA.

NAWATAKIA SIKU NA KAZI NJEMA

CHEF ISSA


Sunday, December 5, 2010

JIFUNZE KUTENGENEZA PIZZA KAUKAU YENYE CHIIZI JUU NA PEMBENI


PIZA HII NI TAMU SANA NA NIRAHISI KUTENGENEZA KAA TAYARI KWA RECIPE

MAHITAJI

KWAJILI YA UNGA WA KUKANDIA
    Utaweza tengeneza 6 pizza  ( 23-30 upana wa cm ) 
1 kilo ya unga wa ngano 
1 kijiko kikubwa cha chakula chumvi
1 kijiko kidogo cha chai amira ya chenga
60 gram Olive oil au vegetable oil
420 gram maji baridi sana (40° F/4.5° C)
1 kijiko kikubwa cha chakula sukari


KWAJILI YA KUWEKA JUU YA PIZZA

600 gram sauce iliyopikwa kwa nyanya
1 kilo Mozarella cheese ( nusu kata slice na nusu kata umbo la mstatiri kama katika picha)
200 gram slice za nyanya fresh iliyoiva
1 fungu la majani ya basil


JINSI YA KUANDAA FATA MAELEKEZO NA PICHA HAPO CHINI



Katika bakuli weka unga wa ngano, humvi pamoja na amira au kama unatumia mashine basi weka katika mashine.



Kisha weka mafuta ya olive, sukari na maji baridi kisha kanda vizuri. kama unatumia mashine weka speed ndogo. 
 

Kanda kwa kutumia nguvu kiasi baada ya maji kushi unga vizuri ili upate mchanganyiko safi.




Kisha toa mchanganyiko huo wa unga na uweke juu ya meza kanda kwa dakika 5 mpaka 7, mpaka uhakikishe mchanganyiko wako umekua laini kabisa. kama bado limekua tepe tepe, ongeza unga kiasi na uendelee kukanda au kama kavu sana ongeza kijiko 1 au 2 vya maji baridi.



Kama unatumia kukandia mashine kama kwa muda huo huo nilioelekeza ila kwa speed ndogo. Mwaga unga juu ya mea unayokandia. Kisha kata unga wako katika vipande sawa 6 vyenye uzito sawa.  Mi nimekata katika vipande 4 kwakua nilikua nataka pizza kubwa.



Mwagia unga kiasi juu ya mchanganyiko wakow a unga. Hakikisha mikono yano ni mikavu kisha ipake pia unga. Kisha chukua vipande hivyo vya unga na viringisha katika maumbo ya duara.



 Kisha chukua hayo maumbo ya duara na weka katika sinia ulilolipaka mafuta weka na paka mafuta juu ya hiyo miviringi pia.



Kisha chukua plastic foil na funika kwa juu.  Kisha weka mchanganyiko wakow a unga katika friji acha ulale usiku kucha pia kama unataka kula pole pole unaweza hifadhi kwa siku 15 mpaka 30 katika freezer sio friji. kisha ukawa unapika pizza moja moja kila siku na kama umeziweka katika freezer kumbuka siku moja kabla ya kuipika pizza yako toa katika freezer na weka katika friji ili iyeyuke. Kama unataka kupika siku hiyo hiyo basi acha katika friji kwa masaa 3 mapka 4 kisha toa.




Siku ya 2 - siku uliyopanga sasa kula pizza, masaa 2 kabla ya kupika viza yako, Toa idadi ya miviringo ya pizza unazotaka kupika wewe. Kwanza unamwagia unga kisaha unapaka mafuta kiasi kisha weka juu ya meza kwajili ya kukanda tena. Kanda kwa dakika 2 kisha funika na plastic wrap Acha kwa masaa 2 nje.



Kisha chukua maumbo hayo ya mviringo na anza kusukuma upate umbo bapa maalumu kwajili ya pizza.



Kwakutumia rolling pin ( ubao wa kusukumia) zungusha pizza yako katika mpini na uibebe



Kisha weka katika pizza pan ambayo imemwagiwa unga na imemwagiw amafuta kiasi (Hii inasaidia pizza isigandie tyra ya kuchomea)
 


Kisha kwa kutumia mikono yako vuta mpaka ifike mwisho wa sahani



Hakikishs baada ya kuivuta mwisho wa sahani iwe na muonekano kama wa kwenye picha



Hakikisha unaweka chizi iliyo na umbo la mstatiri na uache nafasi kama ionekanavyo katika picha. .



Kisha kusanya mchanganyiko wako tokea nje na unaingiza ndani kwa kufunika cheese yote na ukandamize ili ishike. Hakikisha unakandamiza vizuri. Weka mtindo wa curl kama nilivyofanya mimi, Fanya hivyo kuzunguka pizza yote.



Chumua mchuzi wa nyanya ( tomato sauce) kisha pakaza pizza yako yote kwa juu.


 
Rushi majani ya basil juu ya sauce ya nyanya. Kisha weka slice za nyanya fresh, ziwe nyembamba. Kisha weka slice za fresh mozzarella cheese juu kabisa iwe mwisho.



Choma katika oven iliyokwisha washwa na inamoto wa 450-500F. Choma kwa dakika 15 mpaka 20 inategemea na uwezo wa oven yako. Kwa moto makali sana inaweza chukua hata dakika 10 tu. Hakikisha ikiwa katika oven unaichungulia.



Ikishaiva toa na rushia tena majani ya basil kwa juu. Joto kali toka katikapiza litaunguza majani hayo na kutoa harufu safi sana.
 


Kata katika vipande vidogo inakua rahisi kwa mlaji.



Hakikisha unampatia mlaji ikiwa yamoto. Unaweza rushia kwajuu Parmesan cheese ana pili pili manga kama unapendelea.




HUU NDIO MUONEKANO WA PIZZA YETU SAFI SANA UNAWEZA KUIONGEZEA LADHA KWA KUWEKA CHOCHOTE KILE UKIPENDACHO KAMA NYAMA AINA ZOTE NA UKAFURAHIA NA FAMILIA YAKO.



JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO


TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI
TAMU SANA KWA LADHA KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA


MAHITAJI

2 paketi za spaghetti 
60 gram olive oil 
1kitunguu maji kikubwa, chop chop
5 gram kitunguu swaumu
240 gram nyanya ndogo ndogo kata nusu
1 kijko cha chai unga wa coriander
1 kijiko kidogo cha chai unga wa cumin
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa turmeric 
240 gram za chickpeas (Kumbuka kuhifadhi maji utakayochemshia) 
1 kijiko kikubwa cha chakula tomato paste 
6 au 7 mbegu za green olives(sio lazima) 
1 fungu la majani ya giligilani na majani ya mint kwajili ya kupambia
60 gram  korosho au karanga
5 gram chumvi

    JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAELEKEZO HAPO CHINI




    Chemsha chickpeas ziive kabisa ziwe laini kisha chuja maji na . Zichemshe spaghetti fuata maelekezo katika paketi yake. Kisha kaanga vitunguu katika mafuta pamoja na kitunguu swaumu mpaka vilainike.



    Ongezea zile nyanya ndogo ndogo ulizokata nusu, tomato paste pamoja na viungo vyote kaanga mpaka upate harufu nzuri ya mchanganyiko wako kuiva na kua rojo rojo .



    Kisha ongezea chickpeas na kaanga kwa dakika 2 au 3



    KIsha weka spaghetti zilizochemshwa, olive oil, olives na korosho kisha endelea kukoroga pole pole.



    Kisha juu yake pamba kwa kutumia majani ya gili gilani na mint. Majani haya yanaongeza harufu safi na ladha nzuri sana, korosho au karanga zinakupa crunch safi sana.




    FURAHIA MLO HUU RAHISI MTAMU NA SAFI SANA KWA AFYA YA MLAJI



    JIFUNZE KUTENGENEZA SALAD HALISI AINA YA KACHUMBARI


    UHALISIA WA SALAD HII UNATOKEA INDIA IKIWA INAJULIKANA KWA JINA MAARUFU LA Kachumber HAPO ZAMANI ILIKUA INATENGENEZWA KWA MCHANGANYIKO WA KITUNGUU TU NA MAGANGO KWA LUNGHA YA KIHINDI NENO Kachar ni mbichi au haijapikwa RECIPE RAHISI NA SAFI KABISA


    MAHITAJI

    1 kitunguu kikubwa kata slice nyembamba sana
    1 Tango kubwa, menya na katakata
    1 au 2 pili pili mbichi (Sio lazima ingawa inaongeza ladha safi sana)
    2 Nyanya kubwa za kuiva, Kata kata
    1/2-kijiko kidogo cha chai cumin powder (sio lazima)
    2 limao kamua kisha hifadhi maji yake
    5 gram Pili  pili manga
    5 gram chumvi
    1 fungu la gili gilani kwa kupambia na kuongeza ladha


    JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPA CHINI



    Kata kata mboga mboga zote weka katika bakuli moja kisha kamuli maji ya limao.



    Kisha weka unga wa cumin,chumvi na pili pili manga.
     


    Kisha chuku mwiko wa mbao au kijiko cha chakula na koroga vizuri ichanganyike.  Onja uone kama viungo vimekolea. Kisha funika salad yako na weka katika friji. Kuweka katika friji inasaidia salad yako ipoe na viungovyote viingie vizuri na kukolea katika salad.



    Mpatie mlaji ikiwa yabaridi. Unaweza kula na chakula chochote wengi hupendeea kula na nyama choma.




    HUU NI MUONEKANOSAFI KABISA WA KACHUMBARI YETU RAHISI NA TAMU KWA LADHA HALISI.