Monday, January 31, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA PASTA HIZI ZA AINA YAKE


YAWEZEKANA UNAZIONA PASTA HIZI KILA UNAPOINGIA SUPERMAKET AU DUKA LOLOTE LA CHAKULA LAKINI HUVUTIWI KUZINUNUA SASA JIFUNZE MAPISHI YAKE NA FAMILIA YAKO ITAFURAHIA SANA.


MAHITAJI

1 paketi ya Jumbo Pasta Shells ( tumia 10-15 shells kwa watu 2)

360 gram sauce ya nyanya 
180 gram Cottage Cheese, low fat
240 gram Ricotta cheese, low fat
240 Mozzarella cheese ya unga unga 
60 gram parmesan cheese ya unga unga 
1 fungu la giligilani chop chop 
1 fungu la parsley chop chop
1 kitunguu maji chop chop 
5 gram kitunguu swaumu
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga

JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO HAPO CHINI KATIKA PICHA



Pika Pasta shells katika sufuria kubwa, ili zisiweze kugandiana. Pika kwa dakika 10 tu ili zisirojeke maana zitaenda kuiva zaidi katika oven.


Katika kikaango, pika kitunguu na kitunguu swaumu weka 1 kijiko cha mafuta ya Olive mpaka vilegee kidogo kisha ongeza sauce ya nyanya.




 Kisha ongeza chumvi na pili pili manga na acha iendelee kuchemka.




Changanya aina zote 4 za cheeses pamoja na giligilani na parsley


Paka mafuta katika baking pan kisha weka juu yake sauce ya nyanya kwa chini. Chukua mchanganyiko wako wa cheese kisha weka katika jumbo shells moja baada ya nyingine kisha zipange katika bakin pan. Ukishamaliza, mimina juu ya pasta zako sauce ya nyanya iliyobaki.


Choma katika oven kwa moto wa 350F kwa dakika 15 hadi 20 kisha mpatie mlaji ikiwa yamoto.



CHAKULA HIKI NI RAHISI KUPIKA NA NIKITAMU SANA SANA WAANDALIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE

4 comments:

  1. napenda mapishi yako sema hutuambii mahitaji tutajuaje kufantya mchanganyo hapo

    ReplyDelete
  2. tatizo kupika kwa picha mhh kazi kwelikweli

    ReplyDelete
  3. Jamani mahitaji si yamesemwa hapo juu au ni mahitaji gani kimora sidi uayaulizia!

    ReplyDelete
  4. Kilugha najitahidi sana kufuatilia mapishi hapa na kujaribu nyumbani katika kubadili mkenu ila saaa nyingine majina ya bvitu yanapiga chenga, ila tutajitahidi maana nakumbuka hata kwa kiswahili ndo inaweza kuwa balaa. Hongera kazi nzuri unatubadilishia ladha kwakweli maana wengine tulikuwa tunapika mazoea

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako