Friday, February 11, 2011

JIFUNZE KUPIKA SAMAKI TIKKA TAMU KULIKO ZOOTE

KAA TAYARI KWA KUJIFUNZA JINSI YA KUPIKA FILLET YA SAMAKI KWA KUTYUMIA SAUCE AINA YA TIKKA

MAHITAJI

 (Chakula hiki kinatosha watu 4 mpaka 5)



Salmon, Changu, Red snapper, Sangara au Sato - ½ kg fillet toa ngozi
Siagi - 1 spoon (Sio lazima)


 Mahitaji kwajili ya tikka sauce

 1 Kijiko kidogo cha chai unga wa pilipili
 ½ Kijiko kidogo cha hai unga wa manjano
1 Kijiko kidogo cha chai Garam masala
 1 Kijiko kidogo cha chai pili pili manga
 1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu cha kusagwa
1 kijiko kidogo cha chai tangawizi ya kusagwa
 1 Limao kubwa kamua maji yake
5 gram chumvi



JINSI YA KUANDAA FATA MAELEZO HAPA CHINI

1. Changanya katika bakuli viungo vyote kwa pamoja kwajili ya Tikka sauce utapata mchanganyiko mzito sana ili uweze kushika katika fillet ya samaki.

2. Chukua fillet ya samaki uliokwisha kata kata vipande na uzitumbukize kwenye mchanganyiko wa tikka.

3. Baada ya vipande vyote vya samaki kuenea mchanganyiko huo kisha chukua cling film au plastick wrap funika vizuri bakuli kako.

4. Kisha weka katika friji kwa masaa 5 au 6 ili ule mchanganyiko wa tikka ukolee katika fillet ya samaki .

5. Baada ya masaa 6 toa katika friji mchanganyiko wa tikka utakua umeshika vizuri sana samaki wako.

6. Pole pole toa kipande kimoja baada ya kingine na weka katika oven au kama unajiko la mkaa juu ya waya wa kuchomea tayari kwa kuchoma au kuoka.

( Pia unaweza tumia microwave oven kwajili ya kuchomea maelezo yapo hapo chini namba 7.)

7. Choma pole pole kwa moto wa 100⁰C dakika 12 moto wa kawaida kisha badilisha ongeza moto wa  (200⁰C) choma kwa dakika 2 mpaka 3 kisha zima oven yako ila usitoe samaki nje ya oven.

8. Baada ya kuzima oven acha kwa dakika 15 samaki akauke vizuri baada ya hapo unaweza mpatia mlaji.

9. Hapa sasa unatakiwa uyeyushe siagi kisha mwagia kwa juu ili kuongeza ladha.

 


MBINU ZAIDI:

 
Ili uweze pata ladha safi ya tikka jitaidi kata fillet ya samaki wako kwa upana wa inchi 1 tu.



1 comment:

  1. habari yako kaka nimependa sana website yako inahusika sana kwa afya ya binadamu na kutufanya tule vyakula aina tofauti tofauti...
    nlikua naomba utuekaa na vyakula vya watu wanaofanya diet itasaidia sana

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako