Thursday, March 24, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA WAFFLE YENYE LADHA YA ZAFARANI AU SAFRON


KITAFUNWA HIKI NI SAFI SANA WAKATI WA CHAI ASUBUHI NA CHIMBUKO LAKE NI NCHINI BELGIUM KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA

MAHITAJI

480gram whole wheat graham flour ( au tumia unga wa ngao wa kawaida)

4 mayai vunja tumia ute mweupe tu
1 lita ya maziwa
30 gram olive oil
3 kijiko kikubwa cha chakula sukari ( Pia unaweza tumia asali badaya la sukari na inapendeza sana na unga graham)
2 kijiko kidogo cha chai baking powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
2 gram ya saffron ( weka kidogo sana)


JINSI YA KUANDAA FATILIA Ă…ICHA NA MAELEZO HAPO CHINI



Huu ni muonekano wa unga wa ngano anina ya Graham


Katika bakuli changanya unga, sukari, chumvi na baking powder.



Chemsha maziwa yawe ya vugu vugu pamoja na saffron hakikisha unakoroga vizuri kisha weka pembeni katika bakuli

Kumbuka: Kama umetumia asli badala ya sukari, Basi hutakiwi kuweka sukari katika unga unatakiwa uweke asli katika haya maziwa.



Piga ute mweupe wa mayai mpaka uwe na mapovu



Kisha chukua mchangayiko wa maziwa na changanya katika unga.




Kisha ingezea mafuta ya olive.


KIsha ongezea ule ute mweupe wa mayai kisha tumia mwiko na changanya pole pole mpaka unga wote uchanganyike vizuri.


Koroga pole pole mpaka mchangayiko wooote uchangayike vizuri.



Hakikisha unawasha jiko lakupikia wafle kama maelezo ya kiwandani yanavyoelekeza, kisha weka mafuta kiasi na mwagia juu mchanganyiko wa unga.Hakikisha unaweka mchnaganyiko kiasi isijae kabisa maana inaumuka pia sambaza ienee jiko lote.




Muda wa kupika ni dakika 3 mpaka 5 lakini inategemea na maelekezo toka kiwandani. Muonekano huu safi wa rangi ya kahawia ni kua waffle yako imeiva na inaonekana safi sana.

 

Kawaida lazima iwe crispy unapotafuna kw amara ya kwanza kisha ukiendeleea inakua laini. Saffron sio kwajili ya kuongeza rangi ya njano tu au ya rangi ya chungwa lengo hasa ni kuongeza ladha.Unaweza kula kama ilivyo wakati wa chai asubuhi au  uka sliced matunda kama strawberries au blueberries, pia unaweza nyunyiza icing sugar au maple syrup. And oh yes kisha ukinywa na kikombe cha freshly orange juice ukawa umeanza siku na yummy breakfast



 Pia unaweza zikata katika muonekano huu hasa unapompatia mtoto




NI TAMU SANA HII WAFFLE WAANDALIE FAMILIA WAFURAHIE CHAI YA ASUBUHI




JIFUNZE KUTENGENEZA WALI WA KUKAANGA WA KITUNGUU SWAUMU


KAA TAYARI KWA MAPISHI YA WALI HUU SAFI WENYE LADHA YA KITUNGUU SWAUMU NI MAARUFU SANA KWA WENZETU WAPHILIPINO.

MAHITAJI

500 gram za wali ulio iva au wali uliopikwa ukalala ( Huwa natumia mchele wa Basmati)

2 kijikjo kikubwa cha chakula kitunguu swaumu kilichosagwa
4 mbegu nzima za kitunguu swaumu kilichomenywa (sio lazima)
4 miti ya majini ya kitunguu maji chop chop
5 gram chumvi
 1 kijiko kikubwa cha chakula siagi ( butter)
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI



Katika kikaango weka siagi kisha iyeyuke kisha tupia mbegu za kitunguu swaumu ziendelee kuiva.




Kaanga mpaka iwe ya kahawia hakikisha haiunguwi. Hii hatua sio lazima ila mimi nimeongezea tu kwakua huwa napenda sana ladha ya kitunguu swaumu (garlic lovers) kisha toa hizo mbegu na weka pembeni.


Katika kikaango hicho hicho, weka kitunguu swaumu cha kusangwa na majini ya kitunguu maji mabichi yalio katwa katwa



Mchanganyiko wako ukishalainika na kutoa arufu nzuri, kisha chukua wali wako na weka katika kikaango.




Hakikisha una changanya haraka haraka ili iweze changanyika vizuri.


Kisha rushia zile mbegu za kitunguu swaumu ulizokaanga mwanzo na uendelee kuchanganya.





Hakikisha unampatia mlaji haraka chakula kikiwa cha moto chakula hiki unaweza kula na mchuzi au mboga ya aina yeyote.





AINA HII YA MAPISHI INATUFUNDISHA KUA TUNAWEZA AMSHA LADHA ILIYOPOTEA KATIKA WALI ULIOPIKWA JANA UKALALA BADALA YA KUTUPA TUNAONGEZA LADHA NA MLAJI ANAFURAHIA KAMA UMEPIKWA LEO. NI DHAMBI KUTUPA CHAKULA CHYUKUA UTAALAMU HUU NA FAMILAI YAKO ITAFURAHI SANA.


Thursday, March 17, 2011

WAPENZI WA PASTA NA NOODLES HIKI HASA NDIO CHAKULA CHENU

WAPENZI WA KUPIKA BIRIYANI ANGALIA MWISHO KABISA CHINI YA BLOG UTAONA RECIPE SAFI YA BIRIYANI

 PIA KAA TAYARI KW AMAFUNZO YA KUPIKA NOODLES HIZI KWA KUTUMIA MBOGA MAJANI

MAHITAJI

1 paketi ya noodles au spaghetti

1 kitunguu maji kata slice
360 gram ya mushrooms ( uyoga) kata slice
2 Tangawizi mbichi kata slice nyembamba sana
 5 gram kitunguu swaumu
1 fungu la spinach
150 gram njegere zilizochemshwa
1 pili pili hoho kata vipande vidogo
2 kijiko kikubwa cha chakula Oyster sauce
5 kijiko kikubwa cha chakula soy sauce
2 kikiko kikubwa cha chakula sesame oil ( mafuta ya ufuta)



JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI


Andaa noodles kama maelezo yanavyosema katika paketi. Kawaida huwa nachemsha pamoja na chumvi kisha nachuja maji ya moto na ninazipoza katika maji baridi baada ya kuiva. Kisha nazichuja tena na kuzikausha kisha naweka mafuta ya ufuta kijiko kimoja ili kufanya zisishikane.




Hakikisha wakati umemaliza kuchemsha noodles au spagheti mboga majani zote uweme umeshaanda na kuzilkata kwani tunaanza kupika kwa moto mkali sana na kwa haraka. Katika kikaango weka kijiko kimoja cha mafuta ya ufuta kisha weka moto mkali sana yapate moto kisha ongeza kitunguu swaumu, tangawizi na kitunguu maji.




Vitunguu vikishaiva ongeza pilipili hoho na mushrooms




Hakikisha pilipili hoho zinaiva kiasi tu na kutoa harufu nzuri zisipondeke kisha weka majani ya spinach na endelea kukaanga.




Majani ya spinach yakishapata moto na kuanza kulainika weka noodles pamoja na njegere.


Kisha weka soy sauce na oyster sauce haraka haraka hakikisha unachanganya noodles zako zichanganyike pamoja na sauce na mboga majani.




Kisha toa chakula chako katika moto na muhudumie mlaji haraka. Kuongeza ladha zaidi unaweza weka chilli sauce au tomato ketchup.



CHAKULA HIKI NI RAHISI KUPIKA PIA NI NAFUU KWA GHARAMA YA MANUNUZI PIKA CHAKULA HIKI FAMILIA YAKO IFURAHIE TOFAUTI YA MAPISHI.



WAPENZI WA PANCAKE JARIBU HIZI ZA UNGA WA MCHELE NA CHOROKO NA UTAFURAHIA


HABARI NJEMA KWA WALE WASIOTUMI NAFAKA AINA YA NGANO NA WALE WASIOTUMIA MAYAI NA WANGEPENDA SANA KULA CHAPATI HIZI ZA MAJI KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI SANA UFURAHIE NA FAMILIA YAKO.

MAHITAJI

180 gram za mchele uliochemshwa

180 gram za mchele uwe wenye mbegu fupi nene
120 gram za choroko zilizotolewa ngozi
1/2 kijiko cha chai Fenugreek seeds ( angalia chini hapo katika picha)
1-1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi




JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO HAPA CHINI



Loweka choroko pamoja na  Fenugreek katika bakuli moja kisha loweka mchele katika bakuli jingine kwa masaa matatu tu.



Nahuu ni muonekano wa mbegu za  Fenugreek 


Huu ni muonekano wa choroko



Unaweza tumia blenda au ukalowanisha grinder kusaga mchanganyiko wako. Kama unavyoona katika picha hapo mimi natumia grinder ndogo naiweka juu ya meza na huw anatumia kusagia vitu vingi kwa urahisi zaidi. Kwasasa weka mchele na maji kisha washa amshine iendelee kusaga au blenda

 

Saga mapaka upate uji mzito. Hata baada ya kusaga kwa muda mrefu unaweza ona chenga chenga usikate tamaa ni kawaida na mchanganyiko wako uko safi kabisa. Mimina mchanganyiko wako katika bakuli pembeni.

 


Kisha usioshe blenda yako au mashine ya kusagia weka choroko na mbegu za fenugreek katika grinder pamoja na maji kiasi.




Saga tena upate mchanganyiko mzuri na mzito.




Kisha chukua mchanganyiko huo na changanya katika ule mchanganyiko wa mchele uliosagwa pia.




Hakikisha mikono yako ni safi na salama weka chumvi katika mchangayiko na changanya vizuri kwa kutumia mikono yako.Sio lazima kutumia mikono unaweza tumia mwiko pia, Lakini kumbuka joto la kwenye mikono yako linasaidia kufanya unga uchachuke vizuri pale unapouacha usiku mzima kabla ya kupika.




Weka mchangayiko wako katika bakuli safi kwa usiku mzima. Kama unaishi nchi au miji yenye joto unaacha tu nje itaumuka na kuchachuka safi sana ila kama unakaa nchi za baridi basi iwashe oven yako na kisha izime ipoe kiasi chukua unga wako na uweke humo ukae usiku mzima hakikisha oven imezimwa na joto ni dogo sana.
 

Siku inayofuata, changanya mchanganyiko wako safi. Kisha changanya vizuri tena mchanganyiko wako. Weka kikaango chako katika moto na kisha paka mafuta kiasi.Huwa natumia kitunguu kilichokatwa kuenezea mafuta katika kikaango hii husaidia mchangayiko wako wa unga usigandie wakati unakaanga.





Chukua upawa na chota mchanganyiko anza kumimina kati kati ya kikaango.




Baada ya kumimina kiasi hakikisha unasambaza kwanza uone kama inatosha au uongeze



Kiwango ni iwe nyembemba ili iweze kuiva kwa haraka

 

Acha iive kwa dakika 3 au mpaka uone mwisho mwa chapati kuna jikunja na kuacha kikaango na kua na rangi ya kahawia. Hapo itakua rahisi kugeuza na kuivisha upande mwingine.





Geuza na pika tena kwa dakika 2.




Huu ndio muonekano saafi wa chapati yako ya maji na mchanganyiko wa mchele na choroko.

 


Baada ya kuiva ikunje nusu na mpatie mlaji ikiwa ya moto.Inakua na ubora wake endapo utampatia mlaji mara tu baada ya kuiva. Enjoy chapati yako na Coconut Chutney, Tomato Chutney, Onion Chutney, Jam ya ladha yeyote au Asali.


Friday, March 11, 2011

JIFUNZE KUPIKA UJI WA ULEZI KWA KUONGEZA LADHA YA VIUNGO


MWANAO ANASUMBUA AU HAPENDI KUNYWA UJI WA ULEZI? BASI JITAIDI KUUFANYA UJI HUU UVUTIE KWA KUONGEZA LADHA YA VIUNGO NA MWANAO ATAUPENDA SANA SANA. HATA WALE WENYE MATATIZO YA DIABETES WANAWEZA KUNYWA SAFI KABISA.

MAHITAJI

120 gram unga wa ulezi
240 gram ya maziwa ya maji
480 gram maji masafi
1/4 kijiko kidogo cha chai cardamom powder ( Unga wa hiriki)
2 kijiko kikubwa cha chakula sukari

 

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAFUNZO  HAPA CHINI

Jinsi ya kutengeneza uji wa chumvi – badala ya kuweka maziwa weka siagi yenye maziwa ( buttermilk ) kisha badala ya kuweka sukari unaweka chumvi. Kwa mtindo huu basi hutatakiwa kuweka cardamom powder. Mtindo huu wa kupika ni maalumu kwajili ya watu wanaoumwa Diabetes.




Chukua unga wa ulezi kisha weka katika kikaango kikavu kabisa weka katika jiko na uanze kukaanga mpaka upate harufu nzuri aka aroma kwa dakika 3 au 5 inatosha hakikisha haiungui. Lengo hasa ni kutoa harufu ya ubichi wa nafaka katika unga kisha weka pembeni.

watu wengi wakiwa wanapika uji huu huwa wanapika mpaka uunghulie kwa chini ndio wanajua umeiva lakini kwa kutumia njia hii ya kukaanga unga inaokoa muda na hutakiwi tena kupika mpaka sufuria iungue maana ule ubichi na harufu ya nafaka unakua umeshaiunguza.

 


Chukua sufuria kisha weka maji chemsha mpaka yawe ya vugu vugu kisha weka unga na uanze kukoroga maji yakiwa ya vugu vugu yanasaidia unga wako usishikamane na kuweka mabonge mabonge.


 

Endelea kukoroga mpaka unga uchanganyike vizuri kisha ongezea unga wa hiriki ndani yake.

 


Acha iendelee kuchemka.





Kisha ongezea maziwa. Unaweza kuongeza zaidi maziwa au ukapunguza kulingana na ladha unayopenda wewe.





Kabla ya kutoa katika jiko weka sukari ili iyeyuke haraka kisha mpatie mlaji uji ukiwa wa moto. A hearty and very nutritious breakfast and that which keeps me full until lunch. (Uji huu unavirutubisho safi sana vya kutosha kwa afya ya mlaji iwe mtu mzima au mtoto )






HATA KWA WATU WAZIMA UKINYWA UJI WA ULEZI KILA SIKU KWA LADHA ILE ILE UTAUCHOKA TU LAKINI UKIUBADILISHA KWA KUONGEZA LADHA YA VIUONGO UTAUFURAHIA SANA SANA NA HAUTAUCHOKA