Monday, July 11, 2011

WEWE NI MPENZI WA CHOCOLATE NA MCHANGANYIKO WA KARANGA?


KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA KITAFUNWA HIKI KITAMU CHA MCHANGANYIKO WA CHOCOLATE NA KARANGA

MAHITAJI

175 grams Dark Chocolate, (chopped )

200 grams maziwa ya maji
15 grams siagi isiyo na chumvi
75 grams korosho za kuokwa au  ( Karanga za kukaangwa)
5 gram chumvi

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa kuandaa: 1 saa hadi  2

Muda wa kupika: chini ya dakika 15
Inatosha vipande kwa watu 32 hadi 36 




Kata kata chocolate, maziwa ya maji kisha changyana na siagi na chumvi katika sufuria kubwa.



Weka katika moto wa chini ili chocolate iyeyuke pole pole chocolate yako na kisha endelea kukoroga ichanganyike.



Changanya vizuri na uhakikishe imechanganyika vizuri na kua laini.



Baada ya chocolate kuyeyuka hakikisha una tupia ndani yake korosho, au karanga na wengine hutumia pistacho au walnuts.

 


Baada ya kuweka hizo karanga hakikisha unakoroga pia nazo zichanganyike vizuri pamoja na chocolate

Baada ya hapo mimina kwenye tray ya shepu yeyote upendayo wewe (mimi huwa natumia baking pan iliyowekwa karatasi au greased wax paper)



Hakikisha unaisambaza vizuri na upate uswa na umbo safi.



Acha chocolate yako ipoe, weka katika friji ipoe na igande. Kisha kata vipande vidogo vidogo unaweza kata 6X6 mistari ili upate vipande 32 hadi 36




Hapa ipo tayari kwa walaji kula au hata kuweka kwajili ya zawadi.Hakikisha inakaa kwenye ubaridi wa wastani ili isiyeyuke "Take a bite and experience chocolate heaven" :)

WAANDALIE FAMILIA ILI WAFURAHIE

3 comments:

  1. Sasa ndugu yangu ukishachanganya hivyo unaoka au unapakuwa tayari kwa kuliwa ?

    ReplyDelete
  2. Na mimi nauliza hivyo vyeupe hapo juu kwenye picha ya kwanza ni nini?

    Na ration ni kiasi gani...natamani nitengeneze hizi jumamosi....

    Na recipe ya mabumunda unaweza kutuwekea kama unajua jinsi ya kutengeneza?..LOL Mabumunda...yale popcorn tulikua tunauziwa during the break time primary school...Najiuliza walikua wanatengenezaje kila siku..Ilikua kama round bolls..Lakini popcorns sijui na nini tena ilikua tamu zana..

    ReplyDelete
  3. my bro ningefurahi zaid kama hayo mapicha ungekuwa unatuwekea na maelezo maana ukitwambia tukae mkao wa kula tunakuwa tunachelewa si unajua ramadan ipo karibu na watu tunataka tupike mahanjumati ili watoto wapende kufunga kwa kupata misosi minono.

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako