Wednesday, September 14, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA BAMIA HIZI KWA UHARAKA NA LADHA SAFI


UMECHELEWA KUTOKA KAZINI NA UMETAMANI KUPIKA BAMIA JIFUNZE NJIA HII RAHISI NA NYEPESI YA KUPIKA KWA UBORA NA LADHA SAFI KABISA

MAHITAJI

500 gms bamia mbichi (Ladiesfinger)

2 vitunguu vikubwa kata slice
1 kijiko kidogo cha chai tangawizi iliyosagwa
1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu kilichosagwa
1 kijiko kidogo cha chacumin binzali nyembamba
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa manjani (turmeric)
1 kijiko kidogo cha chai unga wa giligilani -(coriander powder)
1 kijiko kidogo cha chai unga wa pili pili (chilli powder)
1/2 kijiko kidogo cha chai juisi ya limao (lemon juice)
1/21 kijiko kidogo cha chai Garam Masala
5 gram chumvi

MUDA WA MAANDALIZI

Muda wa kuandaa : Dakika 30

Muda wa kupika : Dakika 30
Idadi ya walaji : Watu 2



JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO HAPA CHINI


Osha, safisha kisha kausha bamia zako. Kisha kata ncha za mwisho na ukate tena kugawanyisha mara 2 kama uonavyo katika picha.

 

Katika kikaango cha moto weka 1/2 kijiko kidogoc ha chai mafuta ya kupikia, kisha ongezea binzali nyembamba. ikishakua ya brown, ongezea kitunguu maji kilichokatwa, pamoja na tangawizi na kitunguu swawumu cha kusagwa pamoja na chumvi. Endelea kukaanga mpaka vitainike.

 

Kisha weka bamia, hakikaisha hapa unaongeza moto uwe mkali kabisa na kaanga haraka ili bamia ichanganyike na viungo na kitunguu. Kisha punguza moto na acha bamia ichemke kwa dakika 5.



Chakula hiki kinakua tayari tu pale bamia zinapokua laini baada ya kupikwa kwa dakia 15 hadi 20..

 

HAzitakua rojo rojo zitakua na ugumu wa wastani (crunchy) na ni laini kwa mlaji. Just the right bite to it. Kabla ya kutoa unaweza ongeza moto na ukamalizia kiungo cha mwisho juisi ya limao na garam masala, koroga vizuri na kisha mpatie mlaji na Chapati pamoja na wali. 

 


 
CHAP CHAP UNAANDAA

CHAP CHAP IMEIVA

CHAP CHAP UNAKULA

8 comments:

  1. Ahsante maana nilikuwa juzi tu nimekutana na bamia dukani nikanunua nitajaribu mpiko huu.

    ReplyDelete
  2. No idea what you say on the blog, but love your dishes, I am just cooking off the photos!!!Keep it up, great blog

    ReplyDelete
  3. ndugu yangu mbona naona imekuwa kavu sana je nikiongeza nyanya na roiko mchuzi mix yaweza kuwa nzuri nikalia ugali?

    Rose

    ReplyDelete
  4. duh bamia nimezipika zimenogaje asante sana chef.halafu please soma emails zako chef

    ReplyDelete
  5. huwa sipendi bamia lakini leo nimezikung`yata hatariiiii.shurani sana chef

    ReplyDelete
  6. MHH HIYO KWELI NI CHAP CHAP, BIG UP BROZ

    ReplyDelete
  7. asante kwa kunifundisha mapishi ya bamia unanikumbusha sanga mwalugesha

    ReplyDelete
  8. duh umentamanisha,leo naenda pika hii chakula yani na ugali wa udaga+mahindi

    kweli waafrika tuna vyakula

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako